Uchu wa Viongozi Wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchu wa Viongozi Wetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Companero, Sep 6, 2008.

 1. Companero

  Companero Platinum Member

  #1
  Sep 6, 2008
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wajuvi wa mambo wanasisitiza kuwa riwaya makini hasa zile zilizoandikwa na watu walio karibu na Serikali huwa zinakuwa na taarifa nyeti zilizofichwa kisanii ili kuwafikishia ujumbe wasomaji, yaani wananchi, bila Serikali kushtuka kirahisi. Sasa kuna hii riwaya ya A. E. Musiba inayoitwa 'Uchu' iliyotoka mwaka 2000. Riwaya hii inamuongelea kiongozi mmoja kwa jina JKS na jinsi alivyopatwa na mshtuko huko Ughaibuni baada ya kukuta akaunti yake ya fedha katika benki ya huko imefungwa bila yeye kujua. Kuna mtu yoyote anaelewa nini hasa Musiba ambaye kwa sasa yuko karibu sana na JK katika masuala ya kuinadi Tanzania kwa wawekezaji anajaribu kutueleza hapa? Yafuatayo ni maelezo ya awali katika kitabu hicho ambacho yanaonesha kuwa hii haikuwa riwaya ya kawaida tu bali, kama ilivyo riwaya ya 'Makuwadi wa Soko Huria' au 'Miradi Bubu ya Wazalendo', ilikuwa ni utafiti mpana wa kile kinachoendelea nyuma ya mapazia ya viongozi wetu na wawekezaji wao:

  "Kitabu hiki kimeandikwa kwa heshima ya marehemu Abdool Karrim Essack, mwanamapinduzi wa Afrika. Karrim Essack ndiye aliyenichochea kufanya utafiti wa kukiandika kitabu hiki. Siku chache kabla ya kifo chake alipitia ofisini kwangu na kumwuliza katibu shaksia wangu kama nimemaliza kukiandika kitabu hiki. Alipojibiwa bado aliniandikia maneno yafuatayo, ambayo namnukuu kwa kutafsiri: 'Bwana Musiba, Afrika inaingia katika kipindi kipya, kipindi cha ukombozi wa pili. Ukombozi huu ni ukombozi wa fikra na upiganaji wake utakuwa wa kuwaelimisha Waafrika watambue kuwa wao ni taifa lililo kamili na ambalo litakuwa na nguvu kubwa ya kuiongoza dunia katika karne ijayo. Hivyo, kuanzia sasa lazima Afrika iwe na uwezo wa kujiamulia mambo yake yenyewe, ijenge uchumi wake imara ili iondokane na dhana ya misaada. Mwandishi kama wewe una wajibu mkubwa wa kupigana vita hii kwa kalamu. Bwana Musiba andika, na sasa andika zaidi. Punguza shughuli zingine. Afrika inakuhitaji kwani kalamu sasa itakuwa na nguvu kuliko mtutu wa bunduki.'"

  Hivi riwaya za huyu 'Willy Gamba' vinapatikana wapi hasa ile ya 'Hujuma'?
   
 2. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2008
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Point ni nini hapa?
   
 3. M

  Mutu JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hawa mabwana mbona walikuwa na wazo jema sana ,tumuunge mkona ambayo bado yu hai.
   
 4. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,624
  Likes Received: 2,002
  Trophy Points: 280
  Elvis Musiba na Joram Kiango walikuwa ndio the best...yani nilipokuwa bwana mdogo kuanzia miaka 9 hivi...Nilikuwa sizikosi hizo riwaya hata iweje.

  Kuanzia riwaya zenye maudhui ya ukombozi wa Afrika...Na mpambano na Kaburu...Hawa watu ni wa kuwa enzi...Na vitabu vyao vichapishwe upya vina ujumbe mkubwa sana na muhimu.

  Namkumbuka sana jamaa yangu mmoja anaitwa Immanuel Shuma...Huyu alikuwa akiniletea karibu kopi zote mara baada ya yeye kuzisoma.
   
 5. Companero

  Companero Platinum Member

  #5
  Sep 6, 2008
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Pointi ni: Kama ni kweli ukitaka kumficha Mwafrika/Mtanzania kama wewe na mimi kitu kiweke katika Maandishi/Kitabu, je, sisi tunawezaje kuelewa haya wanayojaribu kutufunulia kina Musiba, kuhusu Uchu wa kina JKS, kwa kutumia sanaa ya uandishi/utunzi?
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kiongozi ninayemjua ambaye alikuwa account yake tupu ni Marhemu Kigoma Malima. Kama kuna mwingine sina habari zake. Tuendelee na mjadala.
   
 7. Companero

  Companero Platinum Member

  #7
  Sep 6, 2008
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kweli inawezekana kuzifrizi hizi akaunti za viongozi? Sasa wameshavifungia vijisenti kule Jezi? Au ndio yale ya hotuba ya Kikastro iliyodai kule Idodomya kuwa ni vigumu sana kufuatilia hizo akaunti kama suala haliwahusu na kuwagusa moja kwa moja wenzetu wa huko Ughaibuni?
   
 8. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  It because waliku brain washed na vyakula vya misaada kutoka NJE miaka ya sitini na mwanzoni mwa sabini. Akili zao sasa zimekuwa manipulated kuwa na ubinafsi na umimi. Bado naendelea kutafiti na nimalizapo hili nitamwaga jamvini data
   
 9. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Jasusi,

  Si unakumbuka ni nani aliyefunga akaunti ya Kighoma Malima ndiye anayetoa misamaha kwa wakwapuaji wa EPA?
   
Loading...