Ndumbayeye
JF-Expert Member
- Jan 31, 2009
- 7,333
- 3,896
Nna hamu ya kuona wanavoachiana majimbo unguja na pemba. Au watagawana mapande, cuf wataachiwa zanzibar, chadema na nccr bara!
Ukawa ni ndoa ya ghalfa u sina hakika kama wanampango wakuendeleza upinzani kwa hali hiyo
Wana JF
Kwa hali ilivyo sasa kisiasa Tanzania, matumaini makubwa ni kuiombea UKAWA isimame imara... ni kete pekee ya kuiondoa CCM madarakani uchaguzi ujao. Ni kete pekee kwa sababu ni nguvu ya upinzani iliyounganishwa, na ikiwa haitaingiliwa na ibilisi wa tamaa ya madaraka, basi ni wazi CCM hawana lao tena uchaguzi ujao. Ni vema basi nguvu hii ikadumishwa kwa kuanza kupanga mikakati ya kuachiana nafasi ya kugombea kutoka ngazi ya madiwani, ubunge hadi kumweka mgombea moja tu wa Urais.
Hofu ni kuwa CCM sasa matumbo moto wanaweza kupenyeza mapandikizi wa kuchafua hali ya hewa katika UKAWA.
Ila ni imani yangu kuwa kama hawataingiliwa na uchu wa madaraka, na kama mikakati ya kuachiana kata, majimbo, na hata ngazi ya urais. Matumaini ya kuingia kwenye Nchi ijaayo maziwa na asali yapo karibu kuliko ilivyokuwa utitiri wa vyama vya upinzani kuwagawana kura.
Ni maoni yangu tu, msomaji uko huru kukubaliana nami au la.
Mungu ibariki UKAWA.
kama ndivyo, kwanini basi ccm inakosa usingizi?
hata viongozi wa Roma empire walifikiri kama wewe!! shughulisha akili yako - CCM inaondoka.Hata mkakeshe kwa kalumanzila bado hakuna mwenye ubavu wa kuiondoa CCM.
UKAWA muda si mrefu wataanza vita ya wao kwa wao, katika kugombea nyadhifa mbalimbali.