Uchimbaji wa uranium kuna nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchimbaji wa uranium kuna nini?

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by haki na usawa, Feb 26, 2012.

 1. h

  haki na usawa JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 476
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  naomba kuuliza je kuna nini katika uchimbaji wa uranium katika nchi hii
  maana hata dhahabu uzingatiaji wa afya za wananchi hakuna lakini tunataka kuchokoza madini hatari yaliyokaa chini na uwezo wa kuchimba hatuna ila kuweka wakezezaji tena sababu eti umeme mimi nalia kwa uchungu na nashindwa kuelewa je nchi hii ina nini? na wanataka nini kitokee ndipo watu washituke tunapokwenda? na je viongozi wetu madini mengine yameisha? au kuna mgawanyo wa madini fulani ni fulani kokote yapopatikani nchini ni lazima kamisheni ale yeye? naomba wachangiaji wanielimishe nashindwa kujua sababu ya nchi masikini kuamuru/kutaka kuchimba madini hatari kwa kutegeme wawekezaji na je kweli tutafika salama? Dsm hawana habari lakini maji ya uranium watakunywa wapende wasipende je wananchi wanajua ecolojia? au umeme ni kila kitu kwetu? hata anayelazimisha ajue ndugu zake wataumia tu wapende wasipende maana madhara yana mlolongo mrefu." NAOMBA TUSHIRIKI KUWAELEZA WATOA MAAMUZI NA BILA HIVYO TUSUBIRI MAAFA NA NI MAKUBWA KULIKO YA NORTH MARA YA KIMAZINGIRA" wazoefu waeleze madhara yake wazi na bila hivyo twajirushia bomu wenyewe na hakuna wa kutulipa wenzetu Japani walipigwa mpaka sasa wanalipwa fidia na waliyewapiga." UCHUNGU KUHALALISHA MADHARA KWA WANYONGE NA WANYONGE WAFE ILI MTU APATE ASILIMIA YA KAMISHENI" HAKUNA KIONGOZI MWENYE MACHUNGU NA WANYONGE KAMA UONGO ANGALIA MAENEO YA MIGODI NA SEHEMU WALIKO WAWEKEZAJI. NAOMBA JE TUFANYEJE TUNAKOKWENDA SI KUZURI KILA ZURI LA MWEKEZAJE BILA KUJALI TUNAPATA NINI HATA KIBAYA SAWA KWA NCHI YAKO MAANA WEWE UMEPATA FUNGU LAKOLISILO NA MADHARA NA JE MAREKANI HAYAPO? JE WAMEYACHIMBA? KWANINI HAWATAKI KUCHIMBA? NA KAMA KWANINI KWETU NA SI KWAO? NA JE WATU WAO WATAINGIA KUCHIMBA AU WATANZANIA? JE WAMEJIANDAA KUKABILI MADHARA NA NEMC YA NORTH MARA? KUPEWA TIKEKI NA UNAYEENDA KUMWANGALIA KAAMUZAJE WATU WAKO? KUKODISHA NDEGE KWA WABUNGE ILI WASAIDIE KUFUNGA MJADALA WA MADHARA? kumbuka siasa ni mpito maamuzi yako leo yatakuumiza na wewe pia kesho maana hutakuwa na siku zote."KILA NAFSI ITAPITA ILA JEMA/BAYA LA NAFSI LITABAKI MILELE"
   
 2. PENDING'ULA

  PENDING'ULA JF-Expert Member

  #2
  Feb 29, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku chache za nyuma niliwahi kuandika kitu cha kufanana na chako na kuhoji nchi zilizoendelea kiteknolojia wanapiga vita ili hali sisi tunakimbilia kuchimba madini hatari haya kulikoni! Australia, Urusi na Ujapan ni mataifa ambayo yameendelea sana katika matumizi ya urani.(kwa nishati na silaha) Huko yametokea maafa yakutisha. Hivi hatuyaoni yale? Kwa maoni yangu tunachokiendea ni maafa ya kitaifa!
   
 3. K

  Kidzude JF-Expert Member

  #3
  Feb 29, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 2,725
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 180
  wao watakuwa wamehamia marekani na vitukuu vyao hawataacha kamwe mtu wa ukoo wa TZ
   
 4. m

  mtafungwa Member

  #4
  Feb 29, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 74
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Cha maana ni uangalifu katika suala zima la uchimbaji uranium na mchakato wote unaohusiana na madini haya. Madini haya si hatari kama kuna uangalifu wa kutosha na utaalam unazingatiwa. Pia tuzingatie kwamba nchi yetu inahitaji sana nishati na pia kujihadhari na maadui wa baadaye. Nguvu ya kiuchumi inahitajika sambamba na usalama wa nchi. Usipoonesha nguvu yako duniani kiuchumi na maguvu ya kiusalama hata Israel itakudharau tu maana wewe ni sawa na "kitu kisikuwepo duniani" . Hao unaowataja (wajapan nk.) wanajua sana uzembe waliokuwa nao hadi maafa ya kinuklia yakawakuta. Mtanzania ni sharti ajiamini...asidhani kuwa kwa kuwa walioendelea walishindwa kuzuia maafa ya kinukia basi hata sisi tutashindwa. Wao ni wao na sisi ni sisi. Hatuwategemei wao maana busara tulizojaliwa na mola wetu zipo na zinatutosha....Lakini baada ya kusema hayo, nasema hivi: tupige vita ufisadi, ubinafsi, uzembe, na mambo mengine hatari kama hayo.
   
 5. m

  mzawahalisi JF-Expert Member

  #5
  Feb 29, 2012
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Mtafungwa unaongela busara za kusadikika??? Maana hayo ya sasa yametushinda, kama hao walioendelea wamefanya uzembe cc tutafanya nini? Embu tembea tembea kidogo uijue Tanzania yako bana. Hakuna watu wazembe zaidi yetu kila kitu ni zimamoto. tunafikiria matumbo tu. Hivi sasa watu wako active kidogo kwasababu gharama za maisha kiujumla zimepanda na wengi wa watanzania wanazifill. Akitokea mjanja mmoja akashusha bei za vyakula utaona watanzania tunavyo jisahau.
   
 6. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2012
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nafikiri Uranium ndo gharama wanazolipwa Wamarekani kwa kumficha Balali huko kwao. Sidhani kama walikubaliana na uongo wa serikali yetu kwa bure tu.
   
 7. mkwapuaji

  mkwapuaji Member

  #7
  Mar 4, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 5
  Mafisadi wanatakiwa kufahamu kuwa hakuna mtu mbaya kama mtu anayranza kujitambua na kutambua haki zake
   
 8. PENDING'ULA

  PENDING'ULA JF-Expert Member

  #8
  Mar 4, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu Elimu ya watu wetu katika uwanja wa urani peke yake, hata kabla hayajaanza kuchimbwa ni janga la kiaifa! Watanzania tumewashuhudia wakichimba na kuhujumu mkongo wa Taifa hata ule wa Tanesco unaopita juu ya nyaya zao za umeme kwa kudhani ni coper wakauze kwenye chuma chakavu! pamoja na uhamasishaji na elimu kuwa ile optic fibre ni hatari kwa maisha ya binadamu! Hudhani kwamba yale mabaki ambayo hufukiwa ardhini kwenye makasha maalumu ili kuzuia mnunurisho hayataibuliwa na watu kuanza kuchakura humo?
   
 9. d

  dav22 JF-Expert Member

  #9
  Mar 6, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 1,902
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  inawezekana...lakini hata tukichimba sisi sio watumiaji watumiaji ni wao wenyewe
   
 10. k

  kidonge ki1 Member

  #10
  Mar 7, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  serikali ya Kikwete inataka kuitia hii nchi ya katka matatzo makubwa hiyo urinium tunaichmba ili nini?
   
 11. Nang'olo Ntela

  Nang'olo Ntela Member

  #11
  Mar 7, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 98
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Sambi sao wenyewe!
   
 12. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #12
  Mar 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Duh watanzania kwa woga hata kunguru wa Zenji cha mtoto. Tunaogopa hata EAC kana kwamba mayo inatoa radiation, alafu kibaya tuna ujuzi wakuandika yote yanayo support woga wetu. Tumeivalia njuga urani kana kwamba sisi ni nchi ya kwanza Africa kuchimba urani. Congo na Malawi vimekuwa vikichimba miaka sasa, na hizo ni nchi ambazo haziko politically stable kuliko Tz. Tuna tabia za ajabu sana.

  Alafu tuko mstari wa mbele kushutumu bila kujifunza na kuelewa tunachokiongelea. Na ajabu ni kwamba wanaojuwa ndio wanaongoza katika kupotosha umma. Bado wengi wetu tunazani mchanga unaotoa miozi tulionao kusini mwa Tz ndio sawa na nyuklia iliyomwagika Japan. Nadhani ifike wakati Tz ijitoe kwenye fikra za ujima na ujamaa zinazotufanya tushindwe kupata faida za rasilimali kwa woga.
   
 13. m

  mtafungwa Member

  #13
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 74
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapana. Mbona ukichimba urani na hedhuru wengine hupati dhambi yoyote.
   
 14. m

  mtafungwa Member

  #14
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 74
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo kubwa ni pale tunapopenda kuangalia kila jambo kisiasa. Humu mwetu Tanzania ukiangalia kila kitu kwa mtazamo wa kisiasa hufiki popote. Utajenga conspiracy theories weee hadi mwisho wa dunia ufike. Tutumie umakini zaidi katika kuyaangalia mambo. Tunataka kuendelea sana sisi ktk nyanja zote ikiwa ni pamoja na nyanja ya madini. Jambo la msingi tunalotakiwa kufanya ni kuchanganua jinsi uchimbaji huo unavyotakiwa kufanywa, Namna ya kuongeza wataalam wetu ktk nyanja hii, namna ya kuepuka hatari zinazoweza kuambatana na uchimbaji huo, namna ya kudhibiti mapato yatokanayo na shughuli hiyo, namna ya kunufaika na mapato yatokanayo na uchimbaji huo, nk. Hayo ndiyo tuyafikirie na kuyafungia mkanda kweli kweli. Tukumbuke kwamba nia yetu sisi waTz ni kuwa na uchumi mkubwa na kuiweka Tz iwe miongoni mwa nchi zinazojitegemea na ambazo zinategemewa na mataifa mengine kiuchumi...tunataka tufike huko haraka iwezekanavyo.
   
 15. Nkamu

  Nkamu JF-Expert Member

  #15
  Mar 10, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 206
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nakupongeza Mgonjwaukimwi kwa kujitahidi kutupa shime watanzania wenzetu ili tuweze kujiamini ktk kufanya mambo yetu! Ni jambo la maana kwa kila mtanzania kujiamini ktk kufanya jambo lolote kwa ajili ya mustakabali wa nchi yetu na maendeleo yetu binafsi.

  Jambo moja ambalo nataka kukufahamisha kuhusu Uranium ni kwamba, ule mchanga wa njano ulio kule kusini ni hatari sana. Mimi binafsi niliwahi kuhusika wakati wa utafutaji wa Urani, lakini kitu ambacho tulikuwa tunaambiwa ni kwamba haipaswi kudondosha hata punje ya mchanga ardhini au hata ukigusa kwa mkono ilipaswa unawe sana mikono kwa sabuni. Sababu ni kwamba kama hata kiasi kidogo ulichogusa mkononi ukishika kitu ukala kwa mikono hiyo utaumwa sana tumbo! Sasa jaribu kufikiri kama mvua ikinyesha na kuchukua sehemu ya mchanga huo hadi mtoni hali itakuwaje?
   
 16. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #16
  Mar 11, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Nkamu, naomba nikuondoe wasiwasi juu ya madhara ya mchanga Wa urani.

  Nimefika kwenye machimbo ya urani na nimeshika na kuchezea udongo huo na hadi sasa ni mzima. Huko Namtumbo hapa naposema kuna takriba vijana 200 wakifanya kazi ya kuchimba, kuhoka, na kupaki samples za urani na hakuna japo mmoja anaumwa. Mwaka wa pili sasa. Of course hata unapokuwa unalima na kushika udongo unatakiwa unawe kwa sabuni, unapokuwa mfanyakazi Wa mgodini na viwandani kwenye vumbi na source za radiation unatakiwa unawe mikono kwa sabuni.

  Ule mchanga utakudhuru tu endapo utaula kwa kiasi kikubwa au kwa kuvuta radons kutoka kwenye unstable uranium trioxide. Na ni uvutaji ndio unaolazimisha wafanyakazi wavae chips maalumu kinachosoma kiasi cha miozi ambayo wako exposed nacho over time na kuna standard limit ya exposure over time, I think ni 500 ms over 3 years period ambayo ni ngumu mno kuifikia. Simu yako ya mchina inaku expose kwenye miozi mingi kwa siku kuliko miozi anayoipata mchimbaji urani kwa siku!

  Itakulazimu ubwie mchanga wa urani mwingi mno ili upate madhara Kama matatizo ya figo, cancer ya ubongo, na kuzaa watoto tahaira. Sio kweli kwamba ukigusa tu ule mchanga unadhurika; nisingekuwa duniani leo. Tatizo la kuudondosha mchanga ule ni kwamba ipo mifugo inayokula mchanga mfano kuku na samaki ambao wanaweza kudhurika, vile vile maji ya mto yakiuzoa na kutumika na binadamu upo uwezekano wakuliwa na binadamu. Na ndio maana kampuni inafanya radioactive analysis kwenye chakula na mifugo na maji kabla ya uchimbaji, wakati Wa uchimbaji na baada ya uchimbaji ili kujiridhisha kwamba kiwango cha radioactive material ambacho kinaliwa na wanyama na binadamu kabla ya uchimbaji hakijazidi kiwango cha kawaida na kwamba kinakuwa maintained wakati Wa mgodi.

  Tatizo ni Kama alivyosema mchangiaji Moja hapo juu: SIASA. Viongozi wetu wasipopata ulaji wanaponda, kadhalika wataalamu wetu, utashangaa wataalamu Wa Tz atomic energy commission ambao wanajali matumbo yao na hawakupata mshiko ndo wanaouwa kifua mbele kushawishi wananchi wakatae mgodi. Siasa, ujinga, na njaa ni mafuta yanayoendesha gurudumu la milele la umaskini wetu.

   
 17. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #17
  Mar 11, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Mtafungwa upo sahihi kwa asilimia 100. Siasa Tz amegeuka kuwa adui badala ya kuwa rafiki wa maendeleo ya kiuchumi.

  Faida na hasara za machimbo au bihashara yeyote zinahitaji tafiti za kiuchumi. Cha ajabu Tz mashine za utafiti katika nyanja mbalimbali ikiwemo uchimi hazipo na zilizopo zinafanya tafiti ili kukidhi predetermined political decision au kunufaisha matumbo ya watafiti. Mfano, watafiti kutoka NIMR walikuja na utafiti ulioonyesha kikombe cha babu kinatibu wakati sio kweli, na waliofanya utafiti huo ni " waliobobea" na hadi sasa hawajafunguliwa mashtaka hata baada ya serikali kukubali kwamba kikombe cha babu kilikuwa ni ujasiliamali na si tiba.

  Matokeo ya kukosa vyombo vya uhakika vya utafiti ndio sababu ya mwingiliano wa siasa na uchumi. Mbunge anakua mchumi na mwanasiasa mara tume ya uchaguzi inapomtangaza au anapoteuliwa na rais. Kadhalika mawaziri manaibu na wakurugenzi. Wabunge leo wanategemea maneno ya vijiweni kupeleka mswada na wengine wanategemea uchunguzi wamagazetini, na wengine wanakurupuka na kulivamia jambo.

  Katika hali kama hii ni vigumu kwa wananchi kujuwa ukweli juu ya faida na hasara ya vitega uchumi vyetu maana hata hao viongozi hawajui kwani hawana reliable source of information. Haishangazi mbunge anapokwenda kwenye maeneo ya machimbo ya urani na kusema ati urani inasababisha ushoga na upotevu wa nguvu za kiume na kuomba watu wa maeneo hayo wasusie kazi za machimbo. Hii yote ni ukosefu wa vyombo vya utafiti kwa umma vinavyoaminika.

  Vilevile kuna dhana ya kuabudu siasa na kuwaona wanasiasa ndio wanaojuwa kila kitu. Tuna jumuia kadhaa za wasomi watafiti lakini kamwe hutasikia wakitoa tamko juu ya maamuzi ya kisiasa katika fani zao. Sijasikia Tz atomic energy wakuandika gazetini juu ya madhara ya kweli ya urani na yale yakufikirika, kadhalika sijasikia tamko la wataalamu Wa vyuo vikuu. Lakini matamko ya wabunge ambao wala hawajui urani ikoje utayasikia!!

  At the end of the day, wajanja wanajitokeza kula kile wanachoweza maana wananchi wamebaki gizani sambamba na viongozi wao. Na hii inafanya uvunaji wa faida ya migodi uwe mgumu maana huwezi kuvuna kitu ambacho hakieleweki kwa mvunaji.
   
 18. s

  soledad Member

  #18
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 76
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Jamani madhara mengine ya uranium ni long term , kuna short term effects na long term effects. Tumechomba dhahabu almasi tanzanite n.k but bado hali ya nchi na wanchi ni mbaya do u think this dangerous uranium will make changes to tanzania? kuna mambo mengi ya kufanya nchi ikaendelea sio lazima uranium, tunatakiwa tulinganishe environmental and social impacts za hii project ya uranium na faida zake bwana. Hivi mazingira yakiharibika i.e land water and air tutahamia sayari gani?
   
 19. NullPointer

  NullPointer JF-Expert Member

  #19
  Apr 19, 2012
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 3,483
  Likes Received: 709
  Trophy Points: 280
  Hatuna imani kbs na serikali yetu na hivi tutabaki kulaumu na kuona kila wanalofanya ni ufisadi hata kama sio.. Tujitahidi tuwe tunauliza bac tupate elimu na c kulaumu kila jambo, mi ntabaki kucheka tu.. Sisemi kila kitu wanafanya viongozi wapo sawa lakini sio kwa yale walokosea tuyakuze na tuanze kujaza conspiracies kwenye kila jambo... Mashuleni wanafunzi ndo kabisaaa hawaamini serikali yao... Tujiamini watanzania sio kulalamikia kila jambo... Uclolijua uliza, Uranium mtu aanalalamika huku hata Physics au Chemistry hajasoma, uliza kwanza then uone ka unastahili kulalamika au la... I love Tanzania forever.... We are one tushirikiane
   
Loading...