Uchepukaji

Hazard CFC

JF-Expert Member
Apr 7, 2015
16,620
38,656
Mama mkwe kamkuta mkwe (mume wa bintiye) sebuleni akiwa kafura na kapandisha hasira anadai ataua mtu.

Mama Mkwe: Mwanangu kwani kuna nini jamani?
Jamaa: Leo namuua mwanao, mshenzi sana.

Mama Mkwe: Tulia jamani, kimetokea nini?
Jamaa: Mwanao mshenzi sana, nilikuwa nimesafiri, nikamtumia meseji kuwa nakuja, eti bado leo nimefika nimemkuta na mwanaume kwenye kitanda chetu, dharau gani hii, sikubali leo tunagawana majengo ya serikali, yeye anaenda kulala Muhimbili mi naenda kulala Segerea

Mama Mkwe: Subiri kwanza, mwanangu hayuko hivyo lazima kuna maelezo fulani kuhusu hili ngoja nimuulize...
Mama mkwe akamfuata mwanawe na baada ya muda akarudi sebuleni.

Mama Mkwe: Unaona, nilijua mimi lazima kuna sababu. Kumbe mwenzio hakupata ile meseji uliyomtumia.
:D:D:D:D:D:D:D:D
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom