Uchawi wa macho. Upo na unaishi

Uchawi wa macho. Upo na unaishi

Huo msosi ulikuwa na hamira nyingi, tatizo kama hilo mm lilinipata pale mabibo hostility habari za kula kwa mama ntilie nje nikaachaga. Mana kupata choo inakuaga mtihani kwelikweli na ukipata ni kidogo sana
 
Kule kwa Wajaluo mkoani Mara wanaita hiyo kitu 'Picha ng'ada'. Ujaluoni huwezi kumuona mtu anakula hadharani unless hajipendi.

Halafu kuna mjinga anakuja kukwambia uchawi haupo. Mamaaaee hivi mtu huyo anajua kwanini Prof.Sarungi hakujenga huko kwao Tarime?
 
Zamani ulikuwepo huko kyela sijajua kama mpaka Leo upo
Sio Kyela tu. Hiyo ipo sehemu mbalimbali. Kyela wanaita ijoka. Kuna wengine wamezaliwa hivyo halafu hajui. Mpaka wanaojua wamtapishe. Wapo wengine ndio wanaenda kununua huo uchawi. Japo kwa siku hizi hayo mambo siku hizi yamepungua sana,kama sio kuisha. Niliyasikia zamani miaka ya 90 huko. Naona kama yameisha
 
Singa singa huwezi kumkuta anakula hadharani.kuna mmoja wao aliwahi kuniambia kuwa moja ya sababu inayowafanya wasile hadharani ni kuwa kuna wakati unapokuwa unaonekana na watu ukila,kuna baadhi yao wanaweza kuwa hajala na wana njaa hivyo huwa wanatamani unachokula na wengine wanakuombea vibaya make ni kama unawaringishia ili hali wao wana njaa na huwajali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom