Dunamist
JF-Expert Member
- Aug 13, 2018
- 474
- 689
Hiki ni kisa cha kweli kilichotokea kwenye familia yetu miaka 18 iliyopita.
Ilikuwa mwaka 2000, wakati huo nikiwa na miaka 12. Familia yetu ilikuwa inaishi huko Tarime vijijini kwenye eneo (plot) ambayo haikuwa yetu ila ya jirani yetu ambaye tulikuwa tunaishi naye kama majirani japo kulikuwa na mgogoro wa chini chini a.k.a vita baridi . Back 1999 mdogo wangu alifariki akiwa mchanga kama mwezi m1 na ilisemekana kuwa yule jirani yetu amehusika na kifo chake kichawi. Mwaka 2000 katikati, mdogo wangu wa pili akaanza kuugua. Aliugua sana na kufariki kama miezi 4 baadaye, kwa kuwa yule dogo alikuwa amerithi jina la babu yetu,basi kaka zake baba wakasema hawawezi kukubali baba yao auwawe kirahisi hivyo, wakaamua kufuatilia kupata ukweli wa kifo cha yule dogo.
Wakiwa wamejidhatiti kutaka kujua ukweli juu ya kifo cha yule bwana mdogo waliangukia mikononi mwa mganga mmoja wa kienyeji maeneo ya Nyamongo(sitamtaja jina ila namkumbuka). Walipoeleza shida yao waliulizwa kama wanataka kujua chanzo cha kifo cha yule dogo ili iweje. Wakasema wanataka kama kuna binadamu awaye yote amehusika, NAYE AFE. Wakakubaliana kuwa hata kama ni mmoja kati ya wanafamilia au mmoja kati ya wale walioenda kwa mganga, AFE TU. Mganga akafanya mambo yake na akamtambua aliyehusika na kifo cha dogo na akawatajia kuwa ni yule jirani yetu. Akawaeleza kuwa kuna siku yule bwana mdogo alienda kuchunga pamoja na mtoto mkubwa wa yule jirani yetu kwa mtindo maarufu kule ukuryani wa kuchanganya mifugo, na ndipo yule jamaa aliwapelekea kinywaji a.k.a togwa almaarufu kama OBOSARA kule machungani na kwenye kikombe cha yule bwana mdogo kuliwekwa sumu iliyotafuna ini lake na kupelekea mauti yake. wazee wakiwa na hasira wakakazia kuwa AFE TU. Basi mganga akawaomba zana za kazi ili akamilishe kazi yake chap. Zana zenyewe zilizohitajika ni KINYESI CHA TEMBO na mizizi ya miti kadha wa kadha... Kwa kuwa wazee hawakuwa wataalamu wa mambo waka-opt kutoa pesa watafutiwe zana. Wakatoa keshi laki na ishiirini tii shilings na kazi ikaanza baada ya mganga kumtuma kjana wake ambaye ndiye alikuwa msaidizi wake kwenda porini Serengeti kusaka zana za kazi. Wakaahidiana kuwa baada ya wiki mbili mganga atafika nyumbani kwetu kukamilisha kazi.
Kweli baada ya wiki mbili mganga alitua maskani kwetu usiku wa manane, wakachinja kuku mkubwa jogoo na mganga akapiga na ugali wa mhogo uliochanganywa na mtama akalala. Kesho yake tukaamka na mganga akaanza show kwa kupiga tambiko moja kali sana pale maskani. Tambiko liliambatana na kafara kadha wa kadha na utabiri juu ya maisha yetu pale nyumbani kwa mtu mmoja mmoja. Binafsi mganga alinisimulia kuhusu habari zangu za shule na jinsi nlivyokuwa mkorofi na mgomvi shuleni Kumwika Primary school.
Usiku huo mganga alitia timu kibabe nyumbani kwa yule jirani yetu na kufanya vitu kadha wa kadha bila kuonekana na akapotea kama watu wasiojulikana.
Mganga aliondoka siku iliyofuata kwa ahadi kuwa tutapata majibu ndani ya siku chache..
Baada ya wiki kama mbili, siku moja alfajiri sana mama yangu pamoja na kaka na dada zangu wawili waliamka na kwenda kufuata majani ya kuezekea nyumba eneo la kama kilomita tatu kutoka nyumbani. Asubuhi sana mimi na baba tukaenda kulima kwa jembe la kukokotwa na ng'ombe pale pale jirani na nyumbani. Eneo tulilokuwa tunalima lilikuwa ni kwenye mpaka kabisa wa eneo letu na eneo la yule jirani yetu. Kitu cha ajabu ni kwamba ng'ombe walikuwa hawafiki mwisho wa shamba, walikuwa kama wanaogopa hivi na wakikaribia mwisho wanakimbia kama wameona kitu cha kutisha. Mara ghafla tukasikia mlio mkali sana kutoka vichakani jirani kabisa na pale tulipokuwa tunalima na ni jirani na makazi ya mke mdogo wa yule jirani yetu. Kufumba na kufumbua tukaona tembo mkubwa na mkonga wake akitoka mle vichakani na kuondoka kwa kasi kelekea Serengeti porini.
NINI KILIKUWA KIMETOKEA?
Ni kwamba kuamkia siku ile, yule jirani yetu alilala kwa mke wake mkubwa na kwa sababu mifugo yake ilikuwa inalala kwa mke wake mdogo ambaye ndiye alikuwa anaishi karibu sana na nyumbani kwetu, ilibidi asubuhi sana jamaa awahi kwa mke mdogo apige zake bangi (alikuwa mvutaji wa bangi ya kiko) na kufunga ng'ombe kwa ajili ya kwenda shamba kulima. Alipofika nyumbani aligonga mlango na kumsisitiza bi mdogo amfungulie mlango maana ana kiu ya jani sana na asichelewe shambani. Yule bi mdogo alikasirika sana kuamshwa mapema vile kwa sababu tu eti jamaa anataka kula mmea. Akamjibu kwa jeuri kuwa ''Kwani huko ulikotoka hakuna bangi?, mi sifungui mlango alfajiri yote hii".
Jamaa kwa hasira akaondoka kwenda kichakani kukata (alikuwa na sime yake) fimbo ama mjeledi ama kiboko kwa ajili ya kuja kumshikisha adabu yule mwanamke. Akamuahidi kuwa anarudi na atapata tabu sana. Inasemekana kuwa jamaa alipofika kule vichakani alijisikia kama anahitaji kuachia mzigo almaarufu kama kujisaidia, na alipochuchumaa kukata gogo ghafla bin vuu alitokea tembo mbele yake na ndipo jamaa aliposimama kwa taharuki. Yule tembo alim-mwaga utumbo baada ya kumpiga na jino lake maeneo ya mbele. Kama kawaida tembo huwa ni mstaarabu, alikata majani kadhaa akamfunika na kukojoa juu yake kisha akatoa mlio ule tuliousikia kama taarifa kuwa kazi imeisha. Tembo akachikichia serengeti akipita vijiji kadha wa kadha huku nyuma akiacha msiba mzito kitongojini na kwenye familia ya yule ndugu. Tembo hakusababisha madhara zaidi katika safari yake ya kuelekea porini..
Kama unaaminishwa na sayansi kuwa uchawi sio real, endelea tu mpaka utakapopigiwa show kali ya kibabe na wazee wa kilingeni..