The Iron
JF-Expert Member
- Apr 7, 2017
- 1,397
- 1,473
🤣....Mzee anaogopeka balaaKilenga [emoji3]
🤣....Mzee anaogopeka balaaKilenga [emoji3]
Kweli Makanya ndio kwenu, hiyo iko jimbo gani?Nimezaliwa Makanya
Nimekulia na Kusomea Makanya kuanzia chekechea, shule ya msingi mpaka Kidato cha nne,
Niliondoka Makanya nilipofaulu Kidato cha nne.
Makanya ndio kwetu, Makanya ndio watu wangu, nami ni mtoto wao.
Hayo unayosema yapo Kwa kiasi,
Makanya Ushirikina na Uchawi upo na unaathari labda Kwa wageni wasio wazawa.
Makanya inamchanganyiko wa Makabila kutokana na kilimo cha zao la Mkonge.
Wenyeji wengi ni Wapare,
Lakini pia kuna
Wamasai, wasambaa, Wachaga kidogo, Warundi, Wanyambo, Wasukuma, NK.
Pia wapo wanyiramba.
Uchawi Kwa kiasi kikubwa unapatikana Milimani ambapo ipo Mashariki mwa kamji Ka Makanya.
Wasambaa na watu wa Tanga wameongeza nafasi ya UCHAWI katika mji huo wenye ukame.
Makanya ndio Makao makuu ya Biashara ya Mirungi Afrika Mashariki.
Mirungi hiyo itokayo Milimani hasa Tae, Suji, Parane na Chime ina ladha inayopendwa na watumiaji ukilinganisha na Mirungi ya Kenya na Somalia.
Uchawi pia unaisaidia Biashara hiyo ya Mirungi kuendelea kuexist mbali na Rushwa.
Polisi Wanoko wasiotaka Rushwa hukipata cha mtema kuni wakifuatilia Wauza Mirungi huko Milimani.
Hivyo hujikuta wanapata madhara na kuamua kuacha au huamishwa kabisa kituo cha kazi.
Kipindi nakua, baadhi ya ajali za barabarani zilihusishwa na Uchawi na Ushirikina.
Makanya pia ni moja ya miji iliyojaliwa Madini ya Mawe ya Nasi(Gypsum stone) ambapo hutumika kutengeneza Saruji(Cement).
Ipo dhana katika mji huo kuwa Migodi ya Jasi inaathiri unyeshaji wa Mvua.
Watu wa Makanya kipindi nakua waliamini kuwa Mvua inahamishwa na wenye Migodi ya Mawe Jasi.
Ni kawaida Makanya Wingu Jeusi kutanda lakini upepo ukatokea na kupeperusha mawingu hayo na mvua kugoma kunyesha.
Hata hivyo, kitaaluma Tabia nchi ya Makanya na tambarare ya magharibi ya wilaya ya SAME ni SEMI-ARID DESERT.
Hivyo sifikiri uhaba wa Mvua Makanya unaotokana na uchawi na Ushirikina Bali ni tabia ya nchi ya eneo hilo
AINA ZA UCHAWI ULIOPO MAKANYA KULINGANA NA ASILI;
1. Uchawi wa Wapare wenye asili ya Milimani sio Tambarare
2. Uchawi wa kisambaa
3. Uchawi wa kizigua na Kibondei
4. uchawi wa Kimasai unaotokea magharibi ya Mji wa Makanya ambapo kuna Mji wa Ruvu.
5. Uchawi wa Kirundi kutokana na Wakazi wa Makanya wenye Asili ya Burundi ambao wengi walikuja kufanya vibarua kwenye mashanba ya Mkonge
6. Uchawi wa Wanyambo na Wasukuma. Hawa pia walikuja Kama vibarua vya Mkonge.
7. Uchawi chotara
Ambao kutokana na mchanganyiko wa Makabila Makanya kuna uchawi chotara.
Wachimba Jasi wanaotaka Maeneo mengine ya Tanzania wamechangia kiasi katika uchawi huu.
Msamiati Kama Zongo ni moja ya maneno ya kawaida Makanya.
Kuvunja Jungu, n.k
Makanya na Hedaru ni moja ya miji Maarufu wilayani Same na pia inaongoza Kwa ujanja ujanja.
Sisi Wana Makanya tunapendana mno,
Mshana nikuulize kidogo, inakuwaje washirikina wanazidiana ujanja, ni kipi kinachosababisha hiyo?Kuna ajali ilitokea nikiwa kule. Ilitokea pale Makanya karibu na stand fuso iligongana na gari dogo. Fuso iliumia sana. Lakini siku 2 kabla kuna mzee alikuwa keshatoa onyo (alitapeliwa na dereva asiyemfahamu) Akasema huyo dereva hatakatiza hapa makanya na nataka asife bali avunjike mikono na miguu tu. Na niishuhudie hiyo ajali.
Wakati ajali husika inatokea mzee alikuwa pale stand na dereva alivunjika mikono na miguu yote.
Wala sijamlazimisha mimiKwa hiyo unamlazimisha aamini ushirikina kama wewe?
Kwahiyo Mimi ni dada wa mama yako leo?? Mm sio dada tuheshimiane naweza kuoa ukoo wenu wote Kwa mahali ndogo sanaMbona umeguswa sana na suala hili ?umepanic sana dada . [emoji16]
Unaniombea tena?? Mm siendi kuwachokoza naenda kupata msaada kuna Mambo hayako sawa hata kidogo mkuuNenda tu ila nakuombea sana[emoji2]
Kweli Makanya ndio kwenu, hiyo iko jimbo gani?
hivi yule mzee mwnye mabasi bado yupo?Kule ni full package
najua unaogopa kumtaja tu usije ukaganda kama barafu..uchawi upo zaidi ugweno,usangi na lomwe..
muulize rais wa awamu ya 2.
nadhani hata kwenye kitabu chake hakusalimia na hataki kukumbuka!
aliporudi pwani akatafuta wataalam waliobobea akawatuma kule wakasafishe vijiji vya kishirikina!
ilitokea kasheshe kubwa sana wakati huo ikawa ndio habari ya mjini kipindi hicho!
kuna mzee ana mabasi yatokayo moshi-usangi (sitamtaja)huyo mzee ni fire.
ametesa sana matrafiki waliokuwa wanasumbua basi zake.
kuna trafik alizoea kupiga mkono basi zake hadi leo mkono umebakia kauunyosha juu.hapana chezea huyo mzee!
hiyo ni ruti yake na kila ijumaa usafiri ni bure ole wako konda uchkue nauli unajikuta secret parts hazipo...!
Mkuu Mshana acha kutudanganya bana na picha za Canada ukidai ni upareni.Haya ndio mazingira ya Tae. Ni milimani kwenye baridi kali lakini kukiwa na greenish nzuri na vijito vinavyotiririsha maji meupe masafi.. Hizi picha niliwahi kutupia hapa JF kule SELFIKA[emoji2]
View attachment 1828124View attachment 1828125View attachment 1828126
kuna trafik alizoea kupiga mkono basi zake hadi leo mkono umebakia kauunyosha juu.hapana chezea huyo mzee!uchawi upo zaidi ugweno,usangi na lomwe..
muulize rais wa awamu ya 2.
nadhani hata kwenye kitabu chake hakusalimia na hataki kukumbuka!
aliporudi pwani akatafuta wataalam waliobobea akawatuma kule wakasafishe vijiji vya kishirikina!
ilitokea kasheshe kubwa sana wakati huo ikawa ndio habari ya mjini kipindi hicho!
kuna mzee ana mabasi yatokayo moshi-usangi (sitamtaja)huyo mzee ni fire.
ametesa sana matrafiki waliokuwa wanasumbua basi zake.
kuna trafik alizoea kupiga mkono basi zake hadi leo mkono umebakia kauunyosha juu.hapana chezea huyo mzee!
hiyo ni ruti yake na kila ijumaa usafiri ni bure ole wako konda uchkue nauli unajikuta secret parts hazipo...!
Asante...!Mshana umezingua sana, Tae kuna ushirikina kiasi hicho..sikubaliani na wewe hata kidogo Ila najua unaaminika zaidi so sitatumia nguvu nyingi kupinga hoja yako ya ushirikina huko juu milimani. Yaani kifupi ni kuwa Tae, Chome, Suji, Vudee nk hakuna ushirikina kwa level uliyoongea, umefanya bonge la exaggeration... lakini tukubaline hivyo tu kwamba ushasema hivyo...
Mimi najua ushirikina upo zaidi pare ipi, Ila sio upande uliotaja!
Panda gari za makuyuniNikitaka kufika TAE kwa kutokea Arusha napanda gari za kwenda wapi?
Kuna nyumba za wageni za kulala (Guest house)?
Tae Kuna kipindi mkuu wa wilaya ya Same wa zamani anaitwa Kapufi kama sikosei,alijifanya mjuaji anataka kupambana na mirungi. Alichukua askari akaongozana nao kwenda kukata miti ya mirungi yote. Kufika hapo kijijini mara hawaoni nyumba wala mashamba... wakati wa kurudi sasa wakapotea. Waliteseka hao mpaka wakakoma..Hawakuthubutu kurudi tenaHuwa nacheka sana baadhi ya watu wakipinga kwa nguvu zote kuwa hakuna uchawi. Hawa hawajatembea wakajionea kwa macho yao na kushuhudia live kabisa, SIO KUSIMULIWA.
Last week kuna picha ilitrend mitandaoni ikionesha gari la Landcruiser pickup likiwa limekita pua juu ya paa la nyumba ya udongo na kudumbukia ndani. Achana na ubora na uimara wa nyumba ambayo pamoja na kuathirika kwenye paa lake lakini kuta zimebaki salama licha ya kuangukiwa na gari lenye uzito wa tani hivi.
Baada ya picha ile kuzagaa mitandaoni kuna wanahabari walichukua muda kwenda kupata ukweli na uhalisia wa tukio zima na wakatuletea na video! Katika video husika mashuhuda wakalihusisha tukio zima na imani za kishirikina! Mwenye gari kampuni ya minara ya Arusha kaingia mitini na kulitelekeza gari lake ambalo liliserereka lenyewe likapata support ya waya za umeme na kwenda kuishia kujikita kwenye nyumba husika. Hakukuwa na vifo wala majeruhi licha ya kwamba wakati wa tukio kuna mtoto alikuwa kalala ndani.
Mimi nilikuwa mitaa ya huko mwanzoni mwa mwaka huu. Nilienda kwenye mishe zangu personal. Nilienda Milima ya kati ya Hedaru na Same eneo linaitwa makanya Kijiji cha TAE. Kwa hakika kule niliukuta ushirikina katika uhalisia wake.
Kule mahakama ya haki ni ushirikina hakuna dhuluma, hakuna wizi, hakuna kugeukana hakuna kusalitiana. Ukizingua kwenye hayo moto utakuwakia. Kule ni heshima, adabu, ukweli na uaminifu.
Wizi wa bodabida ni tatizo kubwa Tanzania lakini sio Makanya wala Tae. Wakati naelekea Tae tukapita mahali porini kuna bodaboda imeegeshwa kwenye mti nikaambiwa ina wiki mbili hapo na mwenyewe alitoa tu taarifa kwa ndugu zake kuwa ilimuishia mafuta. Akaiacha hapo akauchapa mpaka Makanya akaenda zake aendako.
Safari yangu ya Tae ilinikutanisha na mambo ya ajabu lakini mengine ya kutisha. Kwa kifupi Tae kunaogopeka kati ya vijiji vyote vya kule. Tae mpaka leo hakuna usafiri wa Jumuiya kwenda na kurudi Makanya licha ya kwamba kuna umbali wa kama Kilometers 20 hivi huko ni boda au kuuchapa na ni kupanda ama kushuka milima na vilima.
Magari yaendayo Tae ni kwa ajili ya waendao kwa waganga wa kienyeji, misiba, shughuli za kiserikali na miradi.
Tae kuna vilinge maarufu vya kuua, kuharibu, kutengenezwa mambo yako. Na wakuu wake hawaingiliani bali wanashirikiana. Nikiwa kule nilishuhudia nyumba zilizoachwa na wahanga wa usaliti kwenye siasa.
Wahanga wa usaliti kwenye biashara (mirungi, bhangi na gongo)
Wahanga wa wizi mbalimbali
Wajuaji nknk
Nilikaa Tae siku tatu tuu lakini niliyoyaona kule yanafaa kuandikiwa kitabu kizima!
Tukirudi kwenye ajali husika tujihoji haya. Kwanini mmiliki kaamua kuitelekeza gari yake ya mamilioni pale?
Je, dereva wake kakimbilia wapi?
Je, wafanyakazi wa kampuni kuna mahali waliharibu?
Bado natafuta wasaa nifike eneo la tukio. Na nikienda huko nitawaletea mrejesho.
View attachment 1828122