Uchawi ni Janga la ULIMWENGHU

Uchawi ni Janga la ULIMWENGHU

Bahati yako. Kwenye daraha hili kuna kibao kilichoandikwa "USIPIGE PICHA". Kuhisu uchawi nakubaliana na wewe maana kwenye picha zako ulizopiga kuna ungo unalinda daraja hilo. Huo mwekundu.

Mie kibao sikukiona, niliporejea ofisini nilimwambia isue hii injini mmoja akanamibia wakati anaenda kule, aliona kibao hicho na yeye alishuka na kuipiga picha vizuri.

Hicho chekundu kwenye picha siyo ungo, ni uwa lililopo kwenye kioo cha mbele ya gari. Kwa kuwa nilipiga picha hizo nikiwa ndani ya gari, ndio maana uwa hilo likatokea, siyo ungo mkuu.

anyway, kwa nini wanapiga mkwara upigaji wa picha kwenye daraja hilo?
 
Mashetani yako kweli nasikia kuna Jumba moja kuuubwa jeupe lipo jirani na Soko la Samaki huko Dsm,nalo lina mashetani,hivyo kumfanya Mkaazi wake kuli avoid kwa kusafiri ili kukwepa vibweka vya hayo mashetani
 
Hapo palipo jengwa Daraja sio kwa sababu ya Uchawi mkuu hapo palipo jengwa Daraja pana Mashetani wabaya wa huo Mto ndio waliowazuia hao Wa China na Wa korea

kujenga hilo daraja, mpaka akaja huyo Mrumi aliyejenga usiku Daraja na kutoa Kafara ya mbuzi wengi yaani Damu kamwaga. Zipo baadhi ya nyumba hatu huku ulaya Watu hawawezi kukaa kwa sababu kuna Mashetani ndio

wanaoishi ukilala usiku kwenye hizo nyumba kama ulifunga maji chooni basi utakuta maji yanamwagika kama ulifunga TV kwenye chumba chako cha kufikia wageni Sitting room utakuta TV yako imefunguliwa hiyo TV kwa sauti kubwa,

ukienda kuangalia huko kwenye TV hakuna aliye funguwa hayo sio mambo ya kichawi ni Mambo ya Mashetani wabaya Pepo wabaya waliomo ndani ya hiyo nyumba. Mkuu tofautisha Mchawi na Mashetani. Mchawi ni ni Binadamu anayeonekana ni yule mtu

anayefanya huo Uchawi na Shetani au Mashetani ni Viumbe aliowaumba Mwenyeezi Mungu, wasio onekana kwa macho yetu ingawa tupo nao kwa wakati wowote ule wapo tunaishi nao hao viumbe wa ajabu Mashetani na binadamu na wapo wanaoishi hao mashetani porini kwenye

Miti mikubwa kwenye bahari au mito au chooni au sehemu inayotupwa takataka, sasa mkuu tofautisha mambo ya uchawi na mashetani nakuacha hapo kwa leo.

Mzizi mkavu, UCHAWI na MASHETANI are side of the same coin, kwangu mimi naamini hivo. Zote ni kazi za ibilisi tu. Sasa ibilisi anapotaka kufanya mamo yake, anaweza kufanya mwenyewe au akapitia kwa watu, ndio tunaoamini kuwa ni WACHAWI.

Swali la msingi, kwani hao jamaa pamoja na teknolojia yao wafanye shughuli usiku? Je ni kutafutwa uungwaji mkono na mashetani hao uliowasema?

Kwa nini wakorea na wachina walichemka lakini warumi wakapeta?
Siyo uthibitisho kuwa warumi ni wachawi zaidi ya hao wakorea na wachina?
Tujazane mkuu, kwani kuna falasafa kuwa uchawi haupo, sasa tunachokiona baadhi ya miradi haifanikiwi mpaka ushirikina/uchawi utumike kama daraja la mto mara na nyumba za hao wazungu huko ulaya.
 
Mashetani yako kweli nasikia kuna Jumba moja kuuubwa jeupe lipo jirani na Soko la Samaki huko Dsm,nalo lina mashetani,hivyo kumfanya Mkaazi wake kuli avoid kwa kusafiri ili kukwepa vibweka vya hayo mashetani

una maana ya IKULU kwa J.K?
 
Mchawi ni nani? mchawi ni mtu asipenda maendeleo ya mwenzake. badala ya yeye kujifunza mwenzake ameendeleaje yeye angependa mwenzake afe. mfano wa mchawi wa Tanzania ni CCM. post yako isingesema duniani maana wenzetu walioendelea hawalogani ili kuzuia maendelea bali wanashikana bila kujali tofauti zao na kuleta maendeleo kwa nchi zao. kuhusu tarime na daraja mimi siamini hizo story maana kama wako fiti ki hivyo si watulogee yanga tusiwe tunatolewa round ya kwanza?

HA HA HA Umenichekesha mkuu.
Anyway, yawezekana nilikosea tofasiri ya uchawi, lakini nizungumzie USHIRIKINA unaoambatana na uchawi, kuroga
 
...........hivyo hupata muda mwingi wa ku-concetrate kuliko mchana na si suala la uchawi maana uchawi sidhani kama unachagua mchana wala usiku
 
Sikujua kuwa ni hadithi za kubuni. Ukiamini kitu usidhani wote wanakiamini kama ufanyavyo. Kirumi na warumi wapi na wapi kama siyo yale ya mfalme wa Oman ana asili ya Kigoma. Wabongo bwana, michosho!

Jina la mtu au kitu huwa ni historia fulani. Eneo hilo kabla ya kujengwa daraja, lilikuwa haliitwi KIRUMI, ila baada ya kujengwa daraja ndo likaitwa hivyo. Liliitwa hivyo kuhifadhi historia ya ujenzi wa daraja au kuonesha uwezo wa taifa la kirumi katika masuala ya teknolojia.
 
Uchawi na ushirikina ni suala ambalo lipo kila kona ya dunia hii. Nimetembelea TARIME, wakati naenda kule nilipita DARAJA LA MTO MARA ambalo kabla ya kujengwa kwake, ilikuwepo PANTON=KIVUKO kilichokuwa kinatumika kuvusha watu toka ng'ambo hadi nyingine.

Serikali iliamua kutengeneza daraja la mto huo, ambapo wakazi wa eneo hilo wanabainisha kuwa WACHINA walichukua kandarasi, lakini kila wakijenga, kesho hawakuti hata nguzo moja waliyoisimamisha, hawakuiti hata alama za ujenzi wowote kufanyika. walijaribu mara kadhaa kabla ya kurudisha tenda kwa serikali wakikiri kushindwa kujenga daraja hilo.

baada ya wachina kushindwa, kandarasi ilichukuliwa na WAKOREA, ambao nao kama wachina walishindwa kujenga daraja hilo kwani yaliyowakuta hayakuwa na tofauti ya yale wachina waliyokumbana nao, hivyo nao walirudisha kandarasi.

Ndipo wakaja WARUMI, hawa kama walivyokuwa wenzao, shughuli zote za ujenzi zilifanyika usiku. Lakini tofauti na wenzao, walinunua mbuzi wengi na kondoo na walikuwa hawaliwi, bali wanachinjwa na damu yake inatolewa sadaka hadi ujenzi wa daraja ukakamilika. Darja walilolijenga WARUMI, ni bora sana, na linaswing endapo kitu kizito kimepita juu.

Baada ya warumi kufanikiwa kujenga daraja hilo, eneo hilo hadi leo panaitwa KIRUMI. Baadhi ya picha kuelekea daraja la kirumi ni kama ifuatavyo:-

View attachment 49989

View attachment 49990

View attachment 49991

View attachment 49992
watu wengi walipoteza maisha hadi daraja hilo kusimama unavyoliona.

Suala la watu kupoteza maisha katika ujenzi wa Daraja hilo siyo issue ngeni, kwani mimi ni mkazi wa jirani na eneo hilo Kiagata. Na baadhi ya ndugu/jamaa waliokuwa wakienda kutafuta kazi/vibarua hawakurudi. Na fununu zinasema walitoswa na manyampara= wazungu,na ikitokea mtu akibaini kuwa kuna mtu kadumbukia utasikia siyo mtu ni karai limetumbukia acha liende; hadi ujenzi unakamilika hali ilikuwa hivyo.
 
Hilo daraja lilikamilika ujenzi wake lini?
 
Suala la watu kupoteza maisha katika ujenzi wa Daraja hilo siyo issue ngeni, kwani mimi ni mkazi wa jirani na eneo hilo Kiagata. Na baadhi ya ndugu/jamaa waliokuwa wakienda kutafuta kazi/vibarua hawakurudi. Na fununu zinasema walitoswa na manyampara= wazungu,na ikitokea mtu akibaini kuwa kuna mtu kadumbukia utasikia siyo mtu ni karai limetumbukia acha liende; hadi ujenzi unakamilika hali ilikuwa hivyo.
Ina Maana kwa wakti huo kulikuwa hakuna kitu kinachoitwa Serikali? mpaka ikafika Watu wanaoomba kazi kutoswa kwenye Mto? Hayo ni ya Ukweli au porojo tu za mitaani.?
 
Hapo palipo jengwa Daraja sio kwa sababu ya Uchawi mkuu hapo palipo jengwa Daraja pana Mashetani wabaya wa huo Mto ndio waliowazuia hao Wa China na Wa korea

kujenga hilo daraja, mpaka akaja huyo Mrumi aliyejenga usiku Daraja na kutoa Kafara ya mbuzi wengi yaani Damu kamwaga. Zipo baadhi ya nyumba hatu huku ulaya Watu hawawezi kukaa kwa sababu kuna Mashetani ndio

wanaoishi ukilala usiku kwenye hizo nyumba kama ulifunga maji chooni basi utakuta maji yanamwagika kama ulifunga TV kwenye chumba chako cha kufikia wageni Sitting room utakuta TV yako imefunguliwa hiyo TV kwa sauti kubwa,

ukienda kuangalia huko kwenye TV hakuna aliye funguwa hayo sio mambo ya kichawi ni Mambo ya Mashetani wabaya Pepo wabaya waliomo ndani ya hiyo nyumba. Mkuu tofautisha Mchawi na Mashetani. Mchawi ni ni Binadamu anayeonekana ni yule mtu

anayefanya huo Uchawi na Shetani au Mashetani ni Viumbe aliowaumba Mwenyeezi Mungu, wasio onekana kwa macho yetu ingawa tupo nao kwa wakati wowote ule wapo tunaishi nao hao viumbe wa ajabu Mashetani na binadamu na wapo wanaoishi hao mashetani porini kwenye

Miti mikubwa kwenye bahari au mito au chooni au sehemu inayotupwa takataka, sasa mkuu tofautisha mambo ya uchawi na mashetani nakuacha hapo kwa leo.

Shetani au Mapepo wanaangalia TV?, Sielewi vizuri hapa. Wanaangalia taarifa ya habari,catoon, au pono?. Fafanua kwa ulivyopata taarifa kwa watu waliokuta tv's zao zimefunguliwa.
 
...........hivyo hupata muda mwingi wa ku-concetrate kuliko mchana na si suala la uchawi maana uchawi sidhani kama unachagua mchana wala usiku

kwa hiyo concentration inakuwa kwenye miradi ya madaraja lakini barabara, majengo hawahitaji concentration?
 
Mashetani yako kweli nasikia kuna Jumba moja kuuubwa jeupe lipo jirani na Soko la Samaki huko Dsm,nalo lina mashetani,hivyo kumfanya Mkaazi wake kuli avoid kwa kusafiri ili kukwepa vibweka vya hayo mashetani

...tihiiiiiii tihihiii!!
 
kwenye ubongo wako, katikati umeshaweka imani hiyo, the way you comment, inathibitisha hilo....... conspiracy
 
Miaka ya 80 mwishoni nikiwa mdogo almanusra nitumbukie kwenye maji kwa sababu nilichelewa kuingia kwenye panton thanks mama alinivuta.

Nalifahamu hilo daraja ni moja ya madaraja bora kabisa afrika ya mashariki, nafikiri nyakati hizo hakukuwa na uchakachuzi.Limejengwa takribani zaidi ya miaka 20 lakini ukiliona utafikiri ni la mwaka jana tu.

Kwa kumbukumbu zangu lilijengwa na wataliano na kirumi ni jina la eneo hili...Mnaweza kunisahihisha.Labda kama mnaunganisha Italy na warumi kwa kungalia historia.
 
i once saw in discovery channel na walielezea kuwa madaraja yanajengwa usiku kutokana na mifumo ya upepo..upepo unaovuma usiku nadhan hauna nguvu kubwa kama wa mchana na hii inasaidia katika kulifanya daraja liwe straight,,ni long time sana siwez kuelezea yote waliyosema bt upepo ndio main reason

waliosoma pressure principle watakataa kwa nguvu zote. mchana kutokana na jua, upepo wake si mkubwa ukilinganisha na wakati wa usiku.
 
Miaka ya 80 mwishoni nikiwa mdogo almanusra nitumbukie kwenye maji kwa sababu nilichelewa kuingia kwenye panton thanks mama alinivuta.

Nalifahamu hilo daraja ni moja ya madaraja bora kabisa afrika ya mashariki, nafikiri nyakati hizo hakukuwa na uchakachuzi.Limejengwa takribani zaidi ya miaka 20 lakini ukiliona utafikiri ni la mwaka jana tu.

Kwa kumbukumbu zangu lilijengwa na wataliano na kirumi ni jina la eneo hili...Mnaweza kunisahihisha.Labda kama mnaunganisha Italy na warumi kwa kungalia historia.

ukiitaja RUMI EMPIRE, ndiyo italy ya leo. Na wao hujitambua/hutambulika kama WARUMI
 
Back
Top Bottom