ntamaholo
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 12,906
- 6,909
Uchawi na ushirikina ni suala ambalo lipo kila kona ya dunia hii. Nimetembelea TARIME, wakati naenda kule nilipita DARAJA LA MTO MARA ambalo kabla ya kujengwa kwake, ilikuwepo PANTON=KIVUKO kilichokuwa kinatumika kuvusha watu toka ng'ambo hadi nyingine.
Serikali iliamua kutengeneza daraja la mto huo, ambapo wakazi wa eneo hilo wanabainisha kuwa WACHINA walichukua kandarasi, lakini kila wakijenga, kesho hawakuti hata nguzo moja waliyoisimamisha, hawakuiti hata alama za ujenzi wowote kufanyika. walijaribu mara kadhaa kabla ya kurudisha tenda kwa serikali wakikiri kushindwa kujenga daraja hilo.
baada ya wachina kushindwa, kandarasi ilichukuliwa na WAKOREA, ambao nao kama wachina walishindwa kujenga daraja hilo kwani yaliyowakuta hayakuwa na tofauti ya yale wachina waliyokumbana nao, hivyo nao walirudisha kandarasi.
Ndipo wakaja WARUMI, hawa kama walivyokuwa wenzao, shughuli zote za ujenzi zilifanyika usiku. Lakini tofauti na wenzao, walinunua mbuzi wengi na kondoo na walikuwa hawaliwi, bali wanachinjwa na damu yake inatolewa sadaka hadi ujenzi wa daraja ukakamilika. Darja walilolijenga WARUMI, ni bora sana, na linaswing endapo kitu kizito kimepita juu.
Baada ya warumi kufanikiwa kujenga daraja hilo, eneo hilo hadi leo panaitwa KIRUMI. Baadhi ya picha kuelekea daraja la kirumi ni kama ifuatavyo:-
watu wengi walipoteza maisha hadi daraja hilo kusimama unavyoliona.