Uchawi na kilimo

Uchawi na kilimo

Hamjui tuu asee haya mambo yapo na ndio maana wachungaji deile wanahubiri huko
 
Sio kilimo tu chief, mafanikio yoyote makubwa ukiyataka iwe biashara, kilimo , nafasi hiz za kazi, itafute kwenye kichaka Cha uchawi, tofauti na hapo UTAPATA TABU SANA, mm mwenyewe nikipata mtaalam mzuri Niko tyr kufunga safar kwenda kumuona.
 
Hapo kwenye mambo ya kazi naona wengi wamepitia changamoto hizi unajua kwenye kilimo mi nimekutana na hizi changamoto sana na sio kwenye mpunga tu nniliingia kwenye ufuta huko kusini ndio nilikoma kabisa
 
Inaonyesha kuwa hao watu wanaona kuwa unaonyesha upo serious kushinda wao kwa hiyo wanakupa discipline kidogo ukiogopa unakimbia.
If you can't fight them join them
 
Imani yako iliko ndio itakayotoa matokeo, unaweza ukafanikiwa kwa kumtegemea Mungu au mungu
 
Hapo kwenye mambo ya kazi naona wengi wamepitia changamoto hizi unajua kwenye kilimo mi nimekutana na hizi changamoto sana na sio kwenye mpunga tu nniliingia kwenye ufuta huko kusini ndio nilikoma kabisa
Mkuu tupe story ya uliokutana nayo katika kilimo Cha ufuta
 
Dah hiyo ya kwenye ufuta nitakua na story kamili ya utafutji wangu tangu nimemaliza la saba.Pengine wale vijana ambao wamekuwa wakiomba misaada humu watajifunza Jambo
 
Kilimo cha baadhi ya sehemu ni changamoto kwa kweli... kuna utaalamu wa kuhamisha mazao ndo unatumika sana huo.. unakuta shamba limenawiri kabisa huku ukiwa umejaa matumaini na bashasha kumbe wazee wa kazi wanakusubiria kwenye mavuno tu..ukianza tu na wao ndo wanahamishia kwao hivo.. kabla hujapiga jembe sehemu husika ni vizuri kuwaona wenyeji wako.. mambo ya kiafrika haya ukiyadharau kamuulize mzungu aliyeshindwa kupitisha umeme wa gridi ya taifa kule iringa hadi akahamia upande wa pili wa barabara...
 
Sio kilimo tu chief, mafanikio yoyote makubwa ukiyataka iwe biashara, kilimo , nafasi hiz za kazi, itafute kwenye kichaka Cha uchawi, tofauti na hapo UTAPATA TABU SANA, mm mwenyewe nikipata mtaalam mzuri Niko tyr kufunga safar kwenda kumuona.
Mimi nilikuwa na Imani ya Kidini sana, ila sasa Imefubaa, nimepata uelewa tofauti sana.
 
Mzee wangu alilima heka 3 za mpunga kule mbalali nilipokuwa darasa la pili.
Sasa baada ya kupiga mpunga vizur akapata gunia kumi na sita tu, na wakati wengine hizo ni kwa heka moja ti.

Siku anatoa tukubai, chini yake alitoka kenge mkubwa sana, na yule kenge hakuwa anakimbia wala nini. Alikuwa anatembea taaaaratibu. Wenyewe wakaropoka tu TAYAAARI .
 
Ni kweli uchawi upo ila ukikuta mtu anaamini uchawi na kuutegemea, jua tu ya kuwa ukoo wao hata wazazi wao wana Mambo ya mazindiko na uchawi, ukweli ni kuwa Duniani hapa huwezi kufight alone, lazima uwe na nguvu ya ziada, na nguvu zipo mbili tu Nguvu ya Mungu na Ya Shetani (ushirikina), Kwa sababu kumtegea Mungu kunahitaji kujinyima na kujitoa hasa na uvumilivu, wengi hukimbilia cheap option upande wa pili yaan upande wa shetani, Kwa shetani utafanikiwa ndio lakni Kwa mda mfupi na Kwa mateso Sana, kukosa uhuru na kulazimika kutoa makafara na kila adha, na finally kushuka kaburini bila tumaini .....

Kumtumaini Mungu ni option bora kabisa, itakuweka huru sana, Siri yake kuu ni kuacha dhambi, kuomba Mungu, kufanya kazi Kwa bidii na kufanya kila uwezalo kutatua changamoto zinazokukabili kwenye kazi unayofanya alafu sehemu inayobak mwachie Mungu amalizie....
Shida kubwa tuna maisha ya Dhambi, wazembe wa kutatua changamoto, uzinzi, uasherati, utapeli, ufisadi, Roho mbaya n.k, asikudanganye mtu haya Mambo huwa yanazuia nguvu ya Mungu na ndo mana wengi hukimbilia Kwa shetani mana anakupa mafanikio hata kama we ni mzinzi na tapeli,...
Mimi nililima mpunga mwaka 2015, hekari moja, nikascore gunia 18 za dede 10...ndo kijana niliyepiga zaidi kijiji kizima huko usukumani, watu waliniulizia mganga wangu ni yupi...wengine waliniambia ukoo wangu upo strong sirogeki ovyo, nikawaambia Mimi ni Mungu tuu na hakuna kingine....

Mwaka Jana nilikuwa Tabora , nyumba niliyopanga ilikuwa imeshindikana kupangika, ilisemekana ni nyumba yenye mashetani, watu walishangaa kuniona natoka na kuingia kwenye nyumba ile bila was was, siku moja watu wakaniambia hvi una mganga gani anayekufanya uishi kwenye hyo nyumba nikawaambia mi naamini Mungu na hawez kunitupa kwenye ujinga kama huo, waliniogopa Sana , walikuwa wanadai huko nyuma hyo nyumba ilikuwa inawaka Moto usiku ...

Mwaka huu hali ya ukame imeleta shida sana, nililima kidogo tu na sikuvuna sana, nilishia kulima robo hekar nikapata kama nusu gunia, mwaka huu nataka ninunue mashine ya kumwagilia alaf nitafute eneo zuri ili kukabiliana na hali ya ukame alafu na kiwasha tena , nitawapa mrejesho mwaka kesho, Mimi siogopi uchawi, nitashindwa Kwa sababu zingine za kawaida kama ukame na sio uchawi....

Wale manotaka kulima we lima tu usiogope mtu na mtumaini Mungu, achana na Mambo ya kutoa makafara watoto na wazazi au kufanyiwa mambo ya ajabu na waganga, mara utembee usiku huku umebeba mabundi, au kulala na nyoka, ili upate mafanikio, huko ni kujidhalilisha tu.....

Pambana upande wa Mungu ushindi ni hakika cha msingi uwe mvumilivu na uache dhambi
 
Ni kweli kuna vitu lazima tumtegemee Mungu ila katka hili la kilimo kuna vitu vingine niliona niliona naendelea kupoteza mda nitakupa mfano mdogo tu wa yaliyonitokea kule malinyi napo kwenye mpunga .baada ya kulima heka 3 mpunga ulianza kusinyaa na hapo nilikuwa nimeweka na maji ya balaka mule shambani baada ya kwenda kanisani na kueleza matatizo yangu ndio nilipewa hayo maji lakini mpunga ulisinyaa ndipo nikaona isiwe tabu nikaenda sehemu hapa dar nikapewa dawa na kwenda kuweka shambani cha ajabu baada ya wiki mpunga ukanyooka kiasi kwamba kila mtu akawa ananiuliza mi nikawa kimya na kwenye kuvuna nilitoa gunia 75 za debe Saba Saba kitu ambacho kiliwashangaza wakulima wengi sana pale na hata wengine wakawa nikiwasemesha wananuna hasa wenyeji.Sasa vituko siku nimeanika mpunga akaja Mzee akasrma dah mpunga umetoka vyema huu halafu hapo hapo akaanza kuluka salakasi juu ya mpunga niliouanik
 
Back
Top Bottom