Uchawi na kilimo

Uchawi na kilimo

ngulukizi

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2018
Posts
637
Reaction score
1,779
NIkiwa katika mihangaiko yangu kipindi flani niliamua kuwekeza katika kilimo cha mpunga hapo maeneo ya Mlandizi ila Sasa niliyokuja kuyaona niliamini hakuna Mungu kwenye kulima mana wakati wa kupanda kila Mkulima alikuja na njia zake za kufanikisha kupanda.

Jilani yangu yeye alikuja na vijana wake wakalizunguka Shamba huku wapo uchi na kichwani walikuwa wamebeba chungu kilichojaa majimaji.

Kuangalia upande mwingine wa Shamba naona mtu anaandikiza hilizi kiukweli niliamini kuliacha lile Shamba mana ni mashamba ya kukodi na niliamua kuondoka kabisa baada ya kuulizia habari za eneo lile kipindi cha kilimo inakuwaje nikapewa mkanda mzima
 
walikuja kishirikina au kibinadamu kawaida je ulikuwa unawaona au nawewe umejizindika mkuu?
 
kuna jamaa yangu kilwa huko nae alinunua shamba the akawa anapanda mahindi hayaoti, kuulizia majirani wakamwambia hilo eneo kuna panya sana. akajiuliza panya wanakula mbegu shamba zima?? akaona isiwe tabu akawa baada ya kulima anachimba mashimo then anafukia huku mbegu kaweka pembeni ya shimo ili kuwapoteza hao panya lakini waapi! hamna kitu kinaota. akabadili kilimo na kuanza kupanda mihogo, aisee ile inaanza kuchipua tuu nguruwe wanafyeka yote............ kuna mzee akamfuata na kumwambia KIJANA UNALIMA KITOTO SANA na ndio ukawa mwisho wa mchizi kulima maeneo yale.
 
nasikiaga wakulima wa korosho wanahamisha Maua na matunda, waeza ona mkorosho wako una mauaa mengi ukajuwa mwaka huu umwe win..... ikifika wakati wa mavunoooo unatoka KAPAAaaaa
 
mumuombe mshana akawaombee kibali cha kulima kwa wenzake pengine mtatoboa kwenye kilimo.Wachawi wakubwa huko vijijini wana mamlaka
 
bimkubwa wangu alilima heka 3 za mpunga aliambulia gunia 10 tu wakati bibi wa jirani alikuwa hana hata haka 2 alikuwa anakuja kuvuna na mafuso dah kudogo awe chizi
Unaweza usiyaamini hayo mambo mpaka yakukute.

Balaa hilo lilinipata mimi pia nilipoamua kuingia kwenye kilimo cha matikiti, hapo Mabwepande.
 
Halafu kuna mtu anasema uchawi ni pesa tu asikwambie mtu Hawa wakulima wengi tunaowaona ni wakubwa Wana Siri kubwa nyingi sana kwa sisi tuliowahi kuishi na kulala mashambani tumeyaona mengi sana ya ajabu
 
Ushirikina hupo sana katika kilimo japo si kila sehemu. Nilishuhudia sana usukumani, ukilima na kupanda kitaalamu kabisa bila kutambikia kwa kuwatumia wenyeji unatoka kapa wakati jirani yako atavuna sana. Hata hivyo kama umejikita katika kilimo kikubwa (large scale) hakuna haja ya kukimbia, unafuata maelekezo ya wenyeji na kusonga mbele. Dawa ya moto ni moto.
 
NIkiwa katika mihangaiko yangu kipindi flani niliamua kuwekeza katika kilimo cha mpunga hapo maeneo ya Mlandizi ila Sasa niliyokuja kuyaona niliamini hakuna Mungu kwenye kulima mana wakati wa kupanda kila Mkulima alikuja na njia zake za kufanikisha kupanda.

Jilani yangu yeye alikuja na vijana wake wakalizunguka Shamba huku wapo uchi na kichwani walikuwa wamebeba chungu kilichojaa majimaji.

Kuangalia upande mwingine wa Shamba naona mtu anaandikiza hilizi kiukweli niliamini kuliacha lile Shamba mana ni mashamba ya kukodi na niliamua kuondoka kabisa baada ya kuulizia habari za eneo lile kipindi cha kilimo inakuwaje nikapewa mkanda mzima
Uongo hamna kitu kama icho, mchawi ni akili yako.
 
Back
Top Bottom