Uchawi: Kwanini Nigeria na sio Misri?

Primary255

Member
Mar 23, 2021
16
45
Ukikagua mabango ya waganga utaona "Mganga hatari kutoka Nigeria".

Tunasikia uchawi mwingi ni kutoka Nigeria.

Manabii wachawi nao utasikia kabla ya kufanikiwa lazima aanzie nigeria kuwaona wazee wa jadi. Manabii wakubwa wenye pesa na uwezo wa kuoshabongo za wafuasi hata bila neno wako Nigeria. Yaani top ten ya wenye fedha wachungaji duniani zaidi ya saba ni wanigeria. Nao wanatuhumiwa kutumia juju.

Wachawi wanaokamatwa uswahilini, wakipewa mfweni au mkong'oto wanafunguka, tumekuwa tukienda Nigeria.

NAJIULIZA, KWA NINI NIGERIA NA SIO MISRI.

1: Uchawi wote duniani asili yake ni Misri.

2: Miujiza ya kutisha na kuogofya ilifanyika misri. Kumbuka kile chama cha wqchawi kikiongozwa na Yane na Yambre walivyoonyesha show hatari hadi nabii Musa akapanic.

3: Library ya vitabu vya kichawi, acha hutu dhaifu unakuta mtu anapewa vikaratasi vya maneno ya kiarabu kama hirizi kwenye bahasha, vyenyewe vilikuwa misri. Kwenye maktaba kubwa kuliko zote na nzee kuliko zite duniani huko alexandria. Hata napolion Bonapatre alipotaka kutawala dunia alituma kikosi kwenda kubeba hayo magombo ya kichawi alexandria ili kuongeza nguvu.

Sasa kwa nini watu hawaendi misri, wala hawaizungumzii kabisakabisa katika uchawi.

Sifa wanapewa wahindi, wachina,wacongo, wanigeria, na tumefika mbali tunawaogopa wasumbawanga kuliko wamisri.

Nini kilitokea hapo wakuu

Siku moja kiongozi wetu wa madhabahu alikuwa anatoa ushuhuda kuhusu mambo aliyo kutana nayo Nigeria,hapo nilawa na mashaka nae.
 

bolivia

JF-Expert Member
Mar 3, 2021
608
1,000
Kwa afrika makao makuu ya wachawi ni Nigeria kwa tza ni gamboshi. Milango ya kuingilia kuzimu ni salenda bridge, mapango ya amboni mengine nimesahau
Tupe. Zaidi ya mlango wa kuingilia upo pale salenda unaonekana unajua vzur mkuu
 

jonnie_vincy

JF-Expert Member
Feb 8, 2014
300
500
Kwa afrika makao makuu ya wachawi ni Nigeria kwa tza ni gamboshi. Milango ya kuingilia kuzimu ni salenda bridge, mapango ya amboni mengine nimesahau

IMG_1042.jpg

Una hakika na unachokisema ?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom