Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,777
Ni nani ameweka fedha hapa? Tamasha la bure kabisa, hii jeuri wanaitoa wapi kwa usawa huu?
====
Mkesha wa muziki wa taarabu utakaohusisha mastaa na wakongwe wa muziki huo nchini utarajiwa kufanyika Agosti 28, mwaka huu katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila.
Akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa Kampuni ya Chocolate Princess Limited waandaaji wa tamasha hilo, Mboni Masimba amesema tamasha hilo ni bure na limeandaliwa mahsusi kwa wadau wa Chama cha Mapinduzi CCM, likibeba kauli mbiu
“Wanamwambao tunatamba na Mama”.
Amesema limepangwa karibu na kampeni kwasababu limelenga kutoa hamasa kwa wapenzi wa muziki huo kushiriki pamoja kwa burudani lakini pia, kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan.
“Hili ni tamasha la kishua lenye ladha ya taarabu ya kipekee. Tutaanza saa 10 jioni hadi majogoo, kisha kwa pamoja tutaelekea kwenye uzinduzi wa kampeni,” amesema Mboni.
Tamasha hilo linatarajiwa kuvuta mashabiki lukuki kutokana na orodha ndefu ya wakongwe wa taarabu akiwemo Khadija Kopa, East Afrika Melody, Sabah Muchacho, Khadija Yusuf, Isha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’, Mwanahawa Ally, Mzee Yusuf, Zanzibar One na Leila Rashid.