Uchambuzi wa Hukumu ya Kesi ya Tigo Vs Mwana FA na AY

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,570
2,000
Uchambuzi huu ni kwa mujibu wa Wakili wa Mahakama Kuu, Hamza (jina la Twitter, @hamzaalbhanj)

Kitu cha kwanza kufahamu hapa ni kitu kinaitwa jurisdiction". Hili neno limetawala sana kwenye hukumu ya Mahakama Kuu ya Mheshimiwa Jaji De Mello. Jursidiction ni ule uwezo wa Mahakama kusikiliza shauri. Uwezo huu wa mahakama umewekwa kisheria kabisa na sio kwa kukurupuka. Wakili kabla ua kufungua shauri lolote anapaswa kutambua jurisdiction ya shauri lake. Jursidiction imegawanyika kwenya mambo mengi kama Fedha, maeneo. Pecuniary Jursidiction ni ile ambayo inahusiana na fedha.

Kwa minajili hyo kutambua jurisdiction ni muhmu sana na mara kwa mara jursidiction imekua ikifanyiwa mabadiliko. Kwa mfano Mahakama ya Wilaya haina uwezo wa Kusikilizia kesi inayozidi kiasi cha Milioni 300 kwa mujibu wa Sheria

HISTORIA YA SHAURI HILI: mnamo mwaka 2011 AY na FA walifungua shauri lao dhidi ya TIGO katika Mahakama Kuu ya Tanzania, TIGO walikuja na pingamizi kuwa kwa mujbu wa kifungu cha 4 cha sheria ya Copyright Mahakama Kuu haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo, hivyo likapigwa chini.

1607413993301.png

Wazee wa habari ndo hyo wakaona isiwe shida ndipo wakasogea Mahakama ya Wilaya ya Ilala na kufungua shauri lao kwa mujbu wa kifungu cha 4 na 36 cha Sheria ya Copyright. Shauri likasikilizwa na Wazee wakashinda kesi yao dhidi ya TIGO na wakalamba billions.

1607414024312.png

TIGO hawakuridhishwa wakakataa rufaaa Mahakama Kuu, Rufaa yao ikapigwa chini kwa sababu hawakuambatanisha kikazia hukumu katika rufaa yao.

1607414052882.png

TIGO wakajipanga tena wakati huo utekelezaji hukumu umeshafanyika na mifuko ya Wazee wa Habari Ndio hiyo na Usije Mjini ilishatuna kwa kitita cha pesa na Wakili alishakula chake. TIGO wakakataa rufaa Mahakama Kuu, uamuzi wa rufaa hii ulitolewa Ijumaa iliyopita katika Mahakama Kuu

1607414087984.png
Uamuzi wa rufaa hii ukawapa ushindi TIGO Jaji alisema"Kifungu cha 4 cha sheria ya Copyright lazima kitumike kwa kuzingatia uwezo wa mahakama kifedha,na hvyo shauri hili limekaa kibishara zaidi na Mahakama ya Ilala ilijipa madaraka ambayo haikua nayo kusikiliza shauri hilo.

Mwisho wa siku Mheshimiwa Jaji akafuta uamuzi wa Mahakama ya Ilala na kuamuru TIGO walipwe gharama za kesi pia. MABADILIKO YA SHERIA Mnamo 2019 yalifanyika Mabadiliko madgo ya sheria ambayo yalibadili kifungu cha 4 cha sheria ya Copyright kwa kuondoa Neno Mahakama ya Wilaya na kuongeza neno Mahakama yenye uwezo wa kushughulikia shauri hlo.

UAMUZI WA MAHAKAMA YA KUU UNA MAANA GANI?

1. Wazee wa usije mjini walipe pesa walizochukua
2. Kifungu cha 4 cha Sheria ya Copyright ya Mwaka 1999 Kina makosa.
3. Mahakama ya Ilala ilikosea kushughulikia kesi ile
4. Mahakama Kuu ilikosea kushughulikia kesi hyo hyo mwaka 2011. RUFAA IMEFUNGULIWA Kwa mujibu wa comment moja ya wakili wa wazee wa usije Mjini amesema kuwa wameshaanza kuandaa utaratbu wa kukata rufaa mahakama ya Rufani.

MASWALI TATA KWA MAWAKILI NA WANASHERIA?
1. Maamuzi ya Mahakama ya Rufani yatakua ya aina gan pale Mahakama kuu na maamuzi yanayobishana.
2. Je, ipi tafsiri sahihi ya kifungu cha 4 cha sheria ya Copyright?
3. Je, TIGO watatumia njia gan kurudisha fedha ambayo ilishalipwa kwa wadaawa?

MWISHO
 

secret file

JF-Expert Member
Sep 10, 2019
3,679
2,000
Mbona unaweka vipisi vipisi vya hukumu!!?
ilitakiwa umwage judgements zote ili tujadili...
alafu punguza utani sentesi zako zinajichanganya......
"Mzee usije mjini"
ndio kitu gani?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom