Uchambuzi wa hotuba ya Rais kwa wahandisi

Zawadi Ngoda

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
3,020
2,000
Nimeisikiliza kwa makini sana hotuba ya Rais Magufuli wiki iliyopita kwa wahandisi. Raisi kawatupia mawe sana wahandisi na kuwaona kama hawafai na waliojaa nadharia wanazoshindwa kuzitekeleza kivitendo. Kalaumu mengi ikiwa pamoja na makisio feke ya gharama za ujenzi wa miradi mbali mbali. Kifupi kasema mengi ambayo binafsi nimeyaona kama siasa za maji taka, siasa nyepesi zenye kuhitaji kuzoa umaarufu kwa wananchi hasa wasio na utaalam katika taaluma hiyo. Nitaeleza kwanini nayasema hayo.

Siasa ndio dira kubwa ya maendeleo ya nchi ikiwemo na fani ya uhandisi. Unaponadi ILANI ya chama, kifupi unaeleza jinsi dira ya maendeleo itavyoelekezwa ikiwepo pamoja na sekta ya uhandisi. Wahandisi hata wakiwa maprofesa na ujuzi wote katika taaluma hiyo hawawezi kufanya lolote kama ILANI za vyama tawala haviwabebi. Zingatia kuwa kwa bahati nzuri tumekuwa na chama kimoja kikitawala Tanzania kwa zaidi ya miaka 50 na Rais magufuli akiwepo katika uwaziri kwa takribani miaka 20. Je ILANI za CCM chaguzi hata chaguzi ziliibebaje taaluma ya UHANDISI? Ilikuwa na mipango gani ya muda mrefu kwa wahandisi kwa maendeleo ya nchi? Hivi ni wahandisi ndio walioingia mikataba ya kuchimba dhahabu na wageni, ujenzi wa bara bara ya Mtwara korido na nyinginezo?

Rais Magufuli amekuwa waziri wa Ujenzi kwa miaka mingi ya uwaziri wake. Na ni wizara hii iliyo na wahandisi wengi kuliko wizara nyingine zote. Na ni wizara hii yenye Miradi mingi katika taaluma ya uhandisi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa bara bara. Je alianzisha kampuni yenye high tech ya watanzania katika kufanya shughuli hizo? Si ndio hawa hawa CCM wakigawa miradi ya ujenzi wa bara bara za mijini na vijijini kwa wana CCM ambao hata hawakuwa na Magreda (vijiko) kama caterpillar. Ukweli ni kwamba miaka 50 yote ilikuwa ni ya ulaji tu katika sekta hiyo, huku wakibadilisha majina tu toka TRM (Watanzani tuliita- Tule Raha Mijini) mpaka leo Tanroad. Katika hali hiyo ya chama chashika hatamu unatarajia wahandisi wafanye nini? Nao waliamua kula na kipofu. Mfano Songambele (darasa la nne) alikuwa mwenyekiti wa CCM TANESCO, Molell (mhandisi) meneja wa TANESCO. Maamuzi ya Molell yalikuwa hayapita bila kukubaliwa na Songambele- Kiutendaji ni kama Songambele ndio alikuwa Meneja. Hiyo ni picha tu ya sehemu moja katika 100.

China (Mao) ilipoamua kujitegemea, kitu cha kwanza kabisa iliwaita wahandisi wake wote maarufu wa ndani na waliokuwa nje ya nchi na kuwauliza hivi hiki na hiki tunaweza wenyewe. Kama mnaweza kufanya huko nje ni nini kinachofanya mshindwe hapa? Wote wakamjibu tunaweza! Ila tusaidie hiki na kile. Akatekeleza na nchi ikaenda. Hali kadhalika Urusi, Vietnam n.k.

Kwa mantiki hiyo, Rais magufuli hana udole wa kuwalaumu wahandisi katika mipango mibovu ya miaka 50 ya chama chake. Kinyume chake ni ukweli inabidi awaombe msamaha wahandisi kwa chama chake CCM kutowajali wasomi ikiwa ni pamoja na wahandisi. Tena afanye hivi mara moja ili wahandisi waweze kufanya kazi. Wahandisi wetu leo wamejaa Botswana, Namibia, Swaziland na Afrika kusini na wanasifa nzuri sana huko. Iweje leo wakija katika ardhi ya Tanzania wanakuwa wabovu. CCM ijisafishe kwanza ndani kabla ya kupaka matope wengine.
 
Misterdennis

JF-Expert Member
Jun 4, 2007
1,748
1,500
Msimu huu misukule ya ccm itazinduka kwa wingi.
Hivi ni wewe Leo hii unayeandika haya kama mtu anayejitambuwa?? Naona huko mliko JPM kawakaba makoo kisawasawa. Mlikuwa mmezoea kula vya bure enzi za jk, sasa mmeshikishwa adabu hadi serikali ya ccm mmeigeuka!
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
22,298
2,000
..kwenye hotuba hiyo Raisi alidai Tz inaibiwa kwa kuruhusu mchanga wenye madini kusafirishwa nje ya nchi.

..sasa waTz wakumbuke kwamba Magufuli alikuwa serikalini wakati mikataba ya madini inasainiwa. Je Magufuli hakujua kwamba mikataba waliyokuwa wakiipitisha ni wizi mtupu kama anavyodai sasa hivi?

..vilevile Raisi alipiga marufuku mchanga huo kusafirishwa nje. Baadaye serikali/wizara ya madini wakatoa tangazo kuwa mchanga huo utaendelea kusafirishwa nje.

..kwa msingi huo Raisi aache kulalamika achukue hatua.
 
Zawadi Ngoda

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
3,020
2,000
Msimu huu misukule ya ccm itazinduka kwa wingi.
Hivi ni wewe Leo hii unayeandika haya kama mtu anayejitambuwa?? Naona huko mliko JPM kawakaba makoo kisawasawa. Mlikuwa mmezoea kula vya bure enzi za jk, sasa mmeshikishwa adabu hadi serikali ya ccm mmeigeuka!

Siasa si upenzi kama wa mpira. Yaani ukiwa mpenzi wa Yanga ndio mpaka kufa, ukihamia Simba wewe ni msaliti. Katika siasa ni lazima uweke nchi kwanza na chama baadae. Aliyekuwa Rais wa Marekani toka Republican "Bush" katangaza juzi kuwa atampa kura yake Clinton wa Democrat. Si kwa sababu yeye alifanya makosa kuwa Republican, laghasha ni kwa sababu hamuelewi mgombea uchaguzi wa Republican "Trump". Kitendo hiki kinaitwa - nchi kwanza.

CCM imefanya madudu sana, lakini wakati ule vyama pinzani ndio havikujipanga kabisa, kulikuwa na wasiwasi kuwa wao wangefanya vibaya sana. Sasa unapochagua cha afadhali na kibaya sana unajua utafanya nini.

Lakini kwa hili siwezi kumsamehe Rais Magufuli, ni lazima awombe msamaha waandisi.
 
Zawadi Ngoda

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
3,020
2,000
..kwenye hotuba hiyo Raisi alidai Tz inaibiwa kwa kuruhusu mchanga wenye madini kusafirishwa nje ya nchi.

..sasa waTz wakumbuke kwamba Magufuli alikuwa serikalini wakati mikataba ya madini inasainiwa. Je Magufuli hakujua kwamba mikataba waliyokuwa wakiipitisha ni wizi mtupu kama anavyodai sasa hivi?

..vilevile Raisi alipiga marufuku mchanga huo kusafirishwa nje. Baadaye serikali/wizara ya madini wakatoa tangazo kuwa mchanga huo utaendelea kusafirishwa nje.

..kwa msingi huo Raisi aache kulalamika achukue hatua.

Hapa sikumuelewa kabisa, kwasababu ni yeye mwenyewe alizuia na nafikiri ni yeye mwenyewe aliyeruhusu. Kwa maana Waziri hawezi kutengua maamuzi ya rais bila kupewa ruksa na Rais mwenyewe.

Na ni vizuri angetoa maelezo kwanini ameruhusu kabla ya kuendelea kulaumu suala ambalo alishalichukulia hatua. Atajikanyaga sana mwaka huu.
 
bigonzo

JF-Expert Member
Feb 23, 2016
2,917
2,000
Hapa sikumuelewa kabisa, kwasababu ni yeye mwenyewe alizuia na nafikiri ni yeye mwenyewe aliyeruhusu. Kwa maana Waziri hawezi kutengua maamuzi ya rais bila kupewa ruksa na Rais mwenyewe.

Na ni vizuri angetoa maelezo kwanini ameruhusu kabla ya kuendelea kulaumu suala ambalo alishalichukulia hatua. Atajikanyaga sana mwaka huu.
Alichemka tz hatuna mitambo ya kuzalisha dhahabu kutoka kwenye hiyo michanga..hiyo mitambo iko Canada .
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom