Uchambuzi wa habari: CUF sio tu imefanya kosa, imefanya kosa kubwa kisiasa

Uliyeleta ujumbe huna Facts maana unaelewa mawazo yako bila facts au evidences zozote. Ni nani aliyemwambia ajiuzulu chana ? na aliona nini wakati anajiuzulu? Na je kaona nini au nini kimebadilika cha kumfanya arudi tena? Kwa hvyo kwa akili ya mtoto mdogo tu aliyefanya mtihani wa dalasa ya saba hv karibuni .ukimweleza atakuambia hv "huyo anakuja ila hana nia nzuri na ujio wake"

Sasa kama mtoto wa dalasa la saba atasema hvyo vipi aliye pal za form four na vipi mtu mzima atasemaje ?

Hapana sio hvyo tu na vipi wasomi wenye Uweleza zaidi na maalifa.

Hyo ni movie ili ujue movie imetengezwa vipi

Please look behind the scene of lipumba to Come against his quitting from the party.

Sent from my TECNO-Y6 using JamiiForums mobile app
 
Naona kama taaluma yako ni ndogo kama sivyo bas kuna kaupande ka siasa kanakusukuma
Hamna uchambuzi ulofanya na sijui tuiteje ulichoandika
 
Ndugu zangu,

Kuna mtangazaji wa redio moja ya Arusha amenipigia simu mchana huu kutaka maoni yangu juu ya CUF kumfuta uanachama Profesa Lipumba.

Nikamwambia, kuwa kwa mtazamo wangu, CUF sio tu imefanya kosa, bali imefanya kosa kubwa la kisiasa.

Siasa ni kama mchezo wa mpira, timu moja inaposhinda ni kwa sababu nyingine kuna kosa imefanya. Na hiyo nyingine ikifanya makosa makubwa ya kiufundi, huwa ni tatizo zaidi.

Inasikitisha, kwamba CUF, chama kikubwa na muhimu kwa kukua kwa demokrasia yetu kinafanya maamuzi ambayo yana gharama kubwa ya kisiasa kwa chama hicho.

CUF bado ilikuwa na nafasi ya kutanguliza busara na hekima na kuyapa nafasi mazungumzo kwa kumshirikisha Profesa. Na kama mazungumzo ya usuluhishi, na hapa ni baina ya Maalim Seif na Profesa Lipumba, yangeshindwa, bado, CUF ingeonyesha ukomavu kwa kumpa Profesa nafasi kwenye mkutano mkuu, ajieleze na mkutano mkuu uamue hatma yake.

Na kuna tatizo gani kwa CUF kuwa na Profesa kama mwanachama? Kikundi kidogo cha watu kwenye Chama kinapojenga mazoea ya kuwafukuza wanachama wake na hususan viongozi kwa kutofautiana mitazamo, basi, ni tatizo kubwa.

CUF wamekutana Zanzibar na kumfukuza Profesa. Kwenye karatasi inaonekana kama ni jambo jepesi. Lakini, kwa Profesa huyu huyu , Lipumba, kutangaza hadharani kumfukuza uanachama, kimsingi, CUF wakubali kuwa wachache miongoni mwao wamekiandalia chama chao mazingira ya kuingia kwenye mgogoro mkubwa na hata mgawanyiko.

Demokrasia ya vyama vingi tunayojitahidi kuijenga inaihitaji CUF kama chama imara, na cha pili kwa ukubwa baada ya CCM, Bara na Visiwani.

Bila shaka, CUF haijaishiwa watu wenye busara na hekima, wenye ujasiri wa kuwaambia wenye kukiendesha chama hicho kwa kasi ya kutisha wakiwa kwenye mteremko mkali, kuwa " Mnakosea".

Maggid.

Katiba ndiyo imemfukuza; Katiba lazima Iheshimiwe na kulindwa kwa gharma yeyote!; Mungu ndio ametuonyesha kwamba kiongozi kama lipumba angepewa nchi ingekuwa balaa tupu...
 
KWANZA NIANZE NA HIZI REDIO ZETU UCHWARA ZINAOENDESHWA NA MAPRESENTA DARASA LA SABA KWAMBA SI KILA MTU MAARUFU BASI ANAUWEZO WA KULISEMEA JAMBO. UPEO NA UWEZO WAO NI MDOGO SANA NA HAWANA FIKRA PEVU HATA KUCHAGUA NANI WA KUULIZA NINI ILI JAMII IELIMIKE.

NDUGU YANGU maggid UNATUANGUSHA WANA-TAMBAZANI, NENO LANGU LA HEKIMA KWAKO NI MOJA TU SIKU NYINGINE UKIPIGIWA SIMU WAAMBIE JAMANI HAPA SINA FACTS ZOTE KUHUSIANA NA JAMBO HILI ILA PINDI NITAKAPOZIPATA NA KUFANYA UCHAMBUZI YAKINIFU NITAWAPIGIA NIWAPE MTAZAMO WANGU.

KUKAA KIMYA JAPO MOYO UNAMVUTO NA UPANDE WAKE NI HEKIMA PIA. UKIACHA KICHWA KIENDESHWE NA MAPENZI YA MOYO AU NA TUMBO LA NJAA UNAJIHARIBIA NDUGU YANGU. NAJUA ELIMU KUBWA NA HEKIMA HUNA ILA KILE KILE KIDOGO ULICHOKIPATA PALE TAMBAZA KITUNZE ILI KIKUTUNZIE HESHIMA YAKO NDOGO ULIYONAYO KWA JAMII NA KWA FAMILIA YAKO.

NAWASIKITIKIA SANA WATOTO WAKO, KAMA NINGEKUWA NA BABA KAMA WEWE NINGEJISIKIA AIBU SANA IKIWA KAMA ANGEKUWA ANATOA MATAMKO KAMA HAYA. UNAZIDI KUDHIHIRISHA KWAMBA SI KILA SIKU UMRI UNAKUJA HEKIMA KUNA NYAKATI UMRI UNAKUJA PEKE YAKE.

MTU AMEJI HUDHURU KWA MAANDISHI (BLACK AND WHITE), TENA RASMI TOKA TAREHE 05/08/2015, MTU MZIMA KAMA YULE LEO HII UNAKUJA KUONGEA UPUUZI KAMA HUU. UNAWAFUNDISHA NINI WATOTO WAKO AU JAMII INAYOKUZUNGUKA. SIKUTEGEMEA UNGEONGEA UJINGA KAMA HUU MAGGID UMENISIKITISHA SANA NA UMEWAANGUSHA WANA-TAMBAZANI. SIKUTEGEMEA KAMA UMEFIKIA MJINGA WA KIASI HIKI MAGGID.

NIKIKUSIKIA SIKU NYINGINE UNATAJA TAMBAZA TUTAKUKANA SABABU TAMBAZA (TAZAMA MBELE ZAIDI) HAITOI WATU WAJINGA WENYE AKILI ZINAZO ENDESHWA NA NJAA ZA TUMBO AU MAPENZI YA MOYO.

GROW-UP MAGGID AND SET AN EXAMPLE OF EXCELLENCE TO YOUR KIDS,

"The first is setting an example of excellence for our children — because if we want to set high expectations for them, we’ve got to set high expectations for ourselves." Barack Obama




 
inaonekana siasa ndo maisha yako!! hutaki kuamini hivyo. Siasa za nchi hii ni udini udini mtupu that's why Mimi binafsi sina chama nasubiri mnichagulie raisi nimpelekee shida zangu
Lipumba ni Mwislamu, Maalim pia, udini unakujaje hapa? Mgogoro ni kati ya Lipumba na CUF, hata kama sababu ni watu
 
Jinsi ulivyoliona suala la prof Lipumba ni kama vile ulikuwa nje ya nchi bila kujua chochote kinachoendele!..halafu ukakrupuka tu na kuandika haya!maana ninauhakika kama unajua kuwa alijiuzulu mwenyewe kabla ya uchaguzi na alibembelezwa kutokuchukua uamuzi huo na viongozi wenzake muda huo!!..nilitegemea usingeandika au unamapenzi naye au unatumiwa au upeo wa kuchambua ni mdogo.. Ila tu nashukuru kwa mtizamo wako kama mtanzania mwenzetu!
 
Mwandishi anataka Seif na Lipumba wajifungie chumbani wafanye mazungumzo ya makubaliano.
Nilipofikia hapo sijaendelea kusoma tena hiyo post nasoma comments tu

Hata mimi niliishia hapo hapo nikaacha kusoma maana nilielewa mtoa post hana nia njema kabisa.
 
Mkuu,
Hili neno '..kwa profesa huyu huyu...' linaonesha wazi kwamba huamini kwamba profesa Lipumba mtaalamu wa uchumi anaweza kufukuzwa unachama.
Lakini unasahau 'Profesa huyu huyu..' ambaye ni mtaalamu wa uchumi,aliwasaliti wenzie baada ya kupewa 'rupia' kwa kujiuzulu uenyekiti ili kukipa CCM nafasi ya kushinda uchaguzi.Wakati yeye ndiye aliwakaribisha ndani ya UKAWA wale aliowaita 'wana makandokando mengi' ya kupewa uongozi wa kitaifa.
Pia ni 'profesa huyu huyu..'ambaye aliahidi atakuwa mwanachama wa kawaida ndani ya CUF ndiye anayepigana kufa na kupona,hata kutumia mbinu zisizo halali(msajili wa vyama vya siasa) ili arudi kwenye uenyekiti wake.
Sasa 'profesa huyu huyu...' ambaye ni mtaalamu wa uchumi mbona anatumia nguvu nyingi kurudi kwenye nafasi hiyo ya uenyekiti?Kuna nini?Kwani hawezi kuisadia nchi kiuchumi bila ya kuwa mwenyekiti wa chama?

Mimi ninachokiona huyu Profesa anaonekana utaalamu wake wa uchumi umelalia kwenye kuneemesha tumbo lake.Na nafikiri hatua waliyomchukulia CUF ni sahihi kwa ustawi wa chama hicho.Huyu ndiye aliyesababisha upinzani ushindwe Zanzibar na Bara.Kumpa uenyekiti ndani ya CUF ni kuikaribisha CCM ndani ya upinzani.Nani anataka hilo?

Kama vipi si aanzishe chama chake?Ili wanaoona anawafaa wajiunge naye?

Hebu tutoleeni ,'utaalamu wenu wa uchumi' wa kuneemesha matumbo,kaanzisheni chama chenu!!!
 
Lipumba alikosea zaidi kukiacha chama alichokiongoza kwa miaka,kwa ulafi tu,kama ni Edward bado yupo ukawa,na kama ni nafasi ya kugombea urais si lazima asimame yeye,kiongozi MUOGA wa aina ya Lip-lip hafai kuongoza mageuzi.
Udhaifu wa Lip-lip hautaweza kuipeleka CUF wala UKAWA ikulu,unafiki wake mkubwa sana na msimamo wake ni finyu sana.
Naona CUF kumfukuza kutakijenga chama na upinzani kwa ujumla,kuliko mtu mwenye dalili ya umamluki kuwa kiongozi katika siasa za ushindani.
Aende tu,nenda Lip-lip,nenda,nenda,nenda.


Mwambieni lipumba aje H2i njaa zake zitaisha mpeni namba zangu 0622670160/0762670160/0683670160au whatsap 0629114315 au aingie website ya HELPING HANDS INTERNATIONAL. www.helpinghandsiternational.biz hata mimi njaa iliisha nilipoingia humo kwenye biashara ya mtandao. Mwambieni amuulize Lowasa kwa nini hatetereki kiuchumi? Kama hajui aje tumpe somo.

www.helping hands international.biz
 
Lipumba ametumwa kuja kuiondoa cuf kwenye ukawa ili ijitegemee, lengo la waliomtuma ni kudhoofisha ukawa ili Pia kupunguza kura za Lowasa kwenye urais 2020. Jiulizeni yeye mwenyewe ndo alisema anapumzika siasa, na wazee na mashehe walimshauri asijiuzuru akakataa, eti leo anasema wazee wale wale wamemshauri arudi ndio amekubali. Cuf ya Lipumba ilikuwa na mbunge mmoja tu bara, miaka yote ya uongozi wake. Leo cuf ya akina Mtatiro ina Wabunge 10 wa majimbo, inaongoza halmashauri kadhaa, halafu ndo anataka kujitenga na ukawa!! Ashindwe kwa jina la Yesu. Mungu amkemee. Umoja wa ukawa ni tishio sana kwa ccm. Na hakuna wa kuuvunja umoja huu wa ukawa, not even Lipumba. Lipumba anadhani cuf ni mali yake anaiweka mfukoni na kuitoa wakati wowote, na kuigeuza geuza kama samaki kikaangoni,NO!! Cuf ni chama cha watu, ni taasii, and no one is bigger than cuf itself.

Sent from my GT-I9060I using JamiiForums mobile app
 
Ccm na ACT wanamuunga mkoo lipumba ili aibomoe ukawa wakitaraji kwamba ACT ndio itashika chat, kalaghabau Ukawa haifi ng'oo, na lipumba amenyoosha maelezo leo ameomba poo eti anaomba maridhiano na Maalim waongee kutafuta muafaka, 'too late propesa just gooo.

Sent from my GT-I9060I using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom