Kitabu.Tough Times Never Last, But Tough People Do!
Mwandishi.Robert Schurler
Mchambuzi.Nanyaro EJ
Chapter 1 Tough Times Never Last…
Hata nyakati ambazo umefanya kila njia na kila mbinu..kumbuka kuwa…………bado kuna njia
Mwandishi anasema kuwa mwaka 1982 ilikuwa kama Dunia imerudi kwenye miaka 1920 wakati wa Great Depression,makampuni yalikuwa yanafungwa,biashara hakuna,ajira hakuna.Wakati haya yakitokea huko USA wanasiasa walitumia kama njia ya kujitengenezea,Democratcs walikuwa wanalaumu Republican ambao ndio walikuwa na serikali.Republican walirudisha lawama kuwa ni tatizo waliloridhi kutoka Utawala uliotangulia wa Democratic .
Hapa kila mmoja hakujishughulisha na tatizo bali lawama.Hivo tatizo liliendelea kuwepo na kwa kuwa hakuna kinga kila mmoja aliadhirika kwa kiwango chake
Kila mtu alijua na aliona kuwa Nchi ilikuwa inapitia kipindi kigumu.Tatizo kubwa ilikuwa attitude ya kukabiliana na tatizo la uchumi.Fikra hasi zilikuwa ndio zinaongoza jamii…hapa kila mwanajamii alilaumu badala ya kushughulika na tatizo..fikra hasi zinaenea kwa kasi kuliko moto wa kifuu kupitia neno la mdomo na njia nyingine za mawasiliano ya kijamii
Mwandishi anasema hii mitazamo hasi na fikra hasi za kijamii ndio aliziona kama fursa na akaanza kutoa semina,na mihadhara kwa watu wa kada mbalimbali.Alianza kwa ugumu ila taratibu watu walianza kumwelewa na kubadilika,kuna kipindi alikuwa anahutubia zaidi ya watu laki tatu kwa mara moja,kwenye hotuba zake aliwafundisha kuhusu mtazamo chanya,fikra chanya…mtazamo/fikra chanya ni moja ya njia bora kabisa za kutatua changamoto ya maisha.Hata hivyo mwandishi anakiri ilikuwa nyakati ngumu sana kuwahubiria matumaini watu ambao wamekata tamaa na hawaoni njia yoyote mbele yaohata hivo hakukata tamaa(ni kama vile unaandika jambo la muhimu kwenye ukurasa wako wa FB hupati likes hata moja ila usikate tamaa tamaa wewe usitazame like,endelea kusonga mbele)
Mwandishi anasema ushuhuda una nguvu kubwa sana, mwandishi anasema alikuwa na tabia ya kuandika changamoto na jinsi alivozitatua,njia,na muda wa utatuzi,kisha aliandika ushindi jinsi alivoshinda,hivo alitumia ushuhuda huu kama njia ya kuwatia watu moyo!(hapa tunaona umuhimu wa maandishi).Anashauri jamii kuwa na tabia ya kuandika na ku share na wengine kama mojawapo ya njia za kuhamasisha ujenzi wa fikra chanya.
Mwandishi anasema alikuwa mkulima mdogo ambaye anafahamu changamoto za ukulima,ikiwepo mvua,na bei isiyo na uhakika.Kilimo hakijawai kuwa rahisi lakini haikufanya wakate tamaa,bali kutafuta njia ya kuboresha zaidi.Anasema mchakato wa kilimo ulimbadili fikra sana,kile kitendo cha IMANI cha mkulima kutupa mbegu chini na kuamini kuwa mvua itanyeesha na hiyo mbegu itazaa,kilikuwa kitendo cha IMANI kubwa na kitendo cha kishujaa.Wakulima ni kundi la kijamii lenye imani kubwa sana na fikra chanya.Alimuuliza baba yake mbona unafanya pata potea? Baba yake alimjibu binadamu asiyekuwa na udhubutu wa jambo daima hubaki hapo hapo alipo bila kusogea mbele(Ndugu msomaji wangu chukua hatua,dhubutu kama mkulima haki utavuna)Mkulima anaweza akaotesha mbegu yake ya mwisho kabisa akabaki hana chakula lakini ana matumaini ya kuvuna baada ya muda fulani,ni kwa kuwa ana imani kuwa Tough times never last but tough people do!anasema anakumbuka mwaka fulani ambao mvua hazikunyeesha hivo ikawa vigumu kuvuna,bahati mbaya mwaka huo baba yake alikuwa amekopa bank na kama hawajavuna maana yake wangefilsiwa,ila baba yake alikuwa mtu wa imani kubwa,akaenda bank kuomba nyongeza ya muda wa marejesho,akiwa na matumaini pengine mavuno ya msimu ujayo yatakuwa makubwa,ghafla ikatokea balaa jingine la kimbunga,ilibidi watoroke na gari yeye na wazazi wake kuelekea mwelekeo kinyume cha Kimbunga,walifanikiwa kuokoa maisha yao,ila mazao na nyumba ziliharibiwa vibaya na kimbunga,hii ni nyumba ambayo iliwekwa dhamana bank,na mazao tarajiwa yakawa yameharibiwa.Hata hivo Baba yake hakukata tamaa,ni baba aliyekuwa na imani ya kuhamisha Mlima,imani ya kutembea juu ya Bahari,Imani ya kutatua kila changamoto,Baada ya miaka mitano Baba yake alijenga na kulipa madeni yote……Je tough times ilidumu? Jibu lake hapana…Usiogope
Mwandishi anasema akiwa ni mtu aliyelelewa katika maisha ya ufukara uliopiytiliza yaani chini ya mstari wa ufukara,hakuruhusu hali hiyo iwe mtego kwake,bali aliifanya kuwa sehemu ya historia ya maisha yake yenye mafanikio makubwa.Anasema wakati fulani wazazi wake walikosa hela ya kununua mkaa ili kupasha nyumba joto wakati wa baridi kali huko kwao.Alilazimika kwenda kuokota magunzi na takataka zingine ambazo walizichoma kama njia ya kupasha moto nyumba.
Mwandishi anakuuliza,je unapitia wakati mgumu?kumbuka maisha yako ni mwanga kwa mtu mwingine,hivo usikubali kukaa gizani muda mrefu.Kuna njia inaitwa “The Possibility Thinking Path.” Njia hiiimekuwa na mafanikio makubwa maishani kwa kila anayeitumia.Hakuna mtu wala binadamu aliyeandikiwa kushindwa tu,wanaoshindwa ni wale ambao hawachukui hatua kudhubutu!Udhubutu ni tiba na suluhisho la changamoto za maisha
Mwandishi anasema kuwa kila binadamu ana tatizo/changamoto yake,hakuna maisha bila changamoto.Lazima ujifunze kuelewa changamoto yako na jinsi ya kutafuta suluhisho,hakuna suluhisho linalofanana kwenye kila changamoto,suluhisho hutegemeana na mazingira mahalia.Jambo la msingi ni kuhakikisha kuwa una control changamoto yako,kamwe usiruhusu changamoto yako iku control.Maisha ya wengi yamekuwa na utata mtupu kutokana na watu husika kushindwa ku control changamto zao na kuendeshwa na presha za nje.Lazima uonyeshe uongozi pale unapokuwa kwenye changamoto
Kitabu.Tough times never last,Tough people do!
Mwandishi.Robert Schurller
Mchambuzi.Nanyaro EJ
Chapter 2: Here’s How You Can Be Tough Too!
Kamwe usiruhusu tatizo/changamoto kuwa sababu au uhalali wa kushindwa kwako
Nini siri ya mafanikio ya watu wanaofanikiwa?Je huwa wanashindaje changamoto ambazo wengine hushindwa?Kwani nini hushinda wakati wengine hushindwa?kwa nini hawazami wakati wengine huzama?
Jibu la maswali yote hayo ni rahisi sana, ni jinsi wanavyotazama tatizo,kwa mtazamo chanya…………….wanalitazama tatizo katika uhalisia wake,na wanaelewa kanuni sita za kutatua changamoto.Hizi ni kanuni sita ambazo ukizizingatia utalishinda tatizo na kuwa mshindi wa maisha yako mwenyewe
1. Every living human beings has problems. Tatizo ni nini? Je unatafuta ajira na hujapata?kama ukiwa na mtazamo hasi utafikiria kuwa kazi ni suluhisho la matatizo yako yote…yaani ukipata ajira utakuwa umemiliki Dunia na Ulimwengu wote.Ukweli ni kuwa walioajiriwa wana matatizo/changamoto pia.Waajiriwa wengi hulalamikia kuwa wanapaswa kuwahi kazini kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa(Baadhi ya Sekta ya Umma)hawana muda wa kufanya jambo lolote,hawa huishia kufanya kazi ili waishi..kazi ya ujira mdogo,They work to live rather than live to work.Matokeo yake hawa waajiriwa huwa hawafanyi kazi kwa weledi wala ubunifu
Je waastafu ndio ambao hawana changamoto? Hapana hata waliostaafu wana changamoto nyingi hasa baada ya kustaafu hutamani kurudi tena kazini,yaani anatamani aamke asubuhi akimbizane…maisha ya kustaafu nayo yana changamoto zake
Je waliofanikiwa?Kimsingi mafanikio ya kiuchumi hayaondoi changamoto,bali huzalisha changamoto mpya
Hakuna mtu wala binadamu ambaye hana changamoto za Maisha
Mwandishi anasema yeye alikuwa na ndoto ya kumiliki kanisa kubwa kabisa,lenye uwezo mkubwa,kwa hesabu zake aliona itamchukua miaka 40 kumiliki hilo kanisa lenye uwezo wa kukaa watu 6000 kwa mara moja.Akaanza kufanyia kazi ndoto yake,ndani ya miaka mitano tayari alikuwa na watu zaidi ya 6000 waumini wa kanisa lake.Anasema hii ilimfundisha kufanyia kazi ndoto yake kwa bidi,na ilimpa somo kuwa kadri unavofanikiwa ndio mahitaji yanaongezeka,alijikuta ana waumini wengi kuliko uwezo wake,na kuliko ndoto yake ya msingi,waumini walifika na kukosa maegesho hali iliyofanya aondoke hata kabla ya kushuka kwenye gari…….Mafanikio huvuta watu zaidi na hivo hitaji huongezeka……
Mfano unaweza ukaanzisha kampuni ya bidhaa fulani,soko likakuendea vizuri sana,ukapata mauzo makubwa,ukajikuta saa tisa mzigo umeisha sokoni,kule kuisha sokoni kutafanya uanze kutafuta njia ya kuongeza uzalishaji na masoko mapya.Hivo hakuna kilele cha mafanikio,kila mara utahitaji zaidi na zaidi
Maisha bila changamoto hayapo na sio maisha,kubali changamoto na songa mbele……………
2. Every problem has a limited life span.
Kila mlima una kilele chake,na kila bonde lina kina chake,ndivo maisha yalivo na mabonde na milima yake,hakuna atakayekaa juu daima,wala hakuna atakayekaa chini milele.Changamoto huisha,na kutoweka.Hakuna hali ya kudumu kwenye maisha,
3. Every problem holds positive possibilities.
Mwandishi ananukuu Bibilia takatifu Mithali 25-2 ambayo inasema Ni Utukufu wa Mungu kuficha jambo,.Kila changamoto huwa na mazuri yake,sio kila chanagmoto ni laana.Shilingi ina sehemu mbili,jambo ambalo ni changamoto kwako ni fursa ya kibiashara kwa mwingine,mfano ukiumwa Malaria ni changamoto kwako,ila kwa mmiliki wa hospital ni fursa ya kutengeneza hela.Kuna vitu kwenye maisha yetu vinalenga kutatua changamoto lakini lazima mtu apate shida,
4. Every problem will change you.
Changamoto huwa haikuachi vile imekukuta,lazima italeta mabadiliko chanya kwenye maisha yako,kuna funzo utapata la maisha.Unaweza ukafutwa kazi kwenye kampuni A ikawa ni njia yaw ewe kupata kazi nzuri zaidi kwenye kampuni B.Kuna nyakati unaweza ukaugua ukaenda hospital kumbe ni nia ya kumpata mwenza/mwenzi wa maisha yako!
5. You can choose what your problem will do to you.
Muda nyakati ngumu huja bila taarifa,lakini ni jukumu lako kushinda hizo nyakati ngumu na kuzibadili kuwa fursa kubwa kwako.Hakikisha hauwi mtumwa wa tatizo,hakuna changamoto yako au huna hakimiliki ya changamoto fulani wala nyakati fulani ngumu.Tambua nyakati na shinda nyakati
6. There is a negative and a positive reaction to every problem.
Watu wenye mafanikio na ambao wameshinda nyakati ngumu…hufanikiwa kutokana na namna wanavotazama nyakati na changamoto zake.Mtazamo hasi au chanya huamua namna ya ushindi! Swala namba moja kuelekea ushindi ni mtazamo chanya,ukweli ni kuwa sio jambo rahisi kama ilivokuandika,ni jambo gumu kuwa na mtazamo chanya kwenye nyakati ngumu na changamoto lukuki,ila lazima kufanya pamoja na ugumu wake!
Mwandishi anatoa mfano wa mtazamo hasi kuwa ni pale ambako umefutwa kazi,unaenda baa kulewa au kuvuta bangi kama sehemu ya suluhisho la changamoto yako!kimsingi hapa unaongeza ukubwa wa tatizo badala ya utatuzi!au wengine huamua kuiba ili kupata ada au matibabu,,utaishia jela kwa kosa la wizi.Mtazamo chanya ni mgumu ila muhimu,unaweza kuwa unadaiwa njia chanya ni kumfuata mdeni wako na kumweleza ukweli,kisha umwombe akupe muda wa kulipa kile unachodaiwa badala ya kukimbia kimbia na kuzima simu au kutopokea simu!
Mwandishi anasema kuna changamoto nyingine unaweza kushindwa kuzitatua ,pale ambako utatuzi umeshindikana angalau hakikisha kuwa una control tatizo..yaani wewe ndio unakuwa juu ya tatizo.Kuna kanuni kumi na mbili za kukabiliana na changamoto/nyakati ngumu
1. Don’t underestimate.
Usidharau wala kupuuzia tatizo,au chagamoto ya maisha,maana huanza kidogokidogo,hatimae huwa kubwa.Changamoto nyingi zimekuwa kubwa baada ya mwanzo kupuuziwa au kutofanyiwa kazi kwa usahihi,unawezakuta mzazi anasema mtoto wangu hafanyi vizuri darasani,lakini atajua tu mbeleni…au naumwa kichwa ila ni kawaida tu kwa kuwa sijanywa maji leo na jana……navuta sigara moja tu hivo siwezi kupata madhara kama wengine…………..matatizo hukua taratibu kama ujauzito…….
2. Don’t exaggerate.
Usikuze changamoto yako na kuifanya ya pekee Duniani.Au usifanye kuwa changamoto yako ndio imeleta balaa zote,na hivo kupata kitu cha kujifichia.Kuna watu huwa wakifiwa tu basi ndio sababu ya kila kitu……akifukuzwa kazi anafanya ndio wa kwanza kufutwa kazi…The one battle most people lose is the batter over the fear of failure… try… start… begin… and you’ll be assured you won the first round.
3. Don’t wait.
Ni kosa kubwa kukaa na kusubiri mambo yatokee…mambo hufanywa kutokea,hayatokei kwa bahati mbaya bali kwa mipango.Kama umefutwa kazi usije ukarudi nyumbani ukakaa kimya bila kuchukua hatua,Mwombe Mwenyenzi Mungu ,kisha chukua hatua….usije ukaketi kusubiria kuitwa kazini tu.Kusubiria muujiza bila kuchukua hatua stahiki kunaweza kupelekea tatizo kuzidi kukua na kuzaliana(Mwenyenzi Mungu ametupa akili ya kufikiri sawasawa na kuchukua hatua)
4. Don’t aggravate.
Usianze kurusha lawama kwa wengine,jamii,kampuni..ukaanza kusema kwa nini meneja amenifuta kazi mimi,huyu meneja yuko hivi ama vile…ukifanya hivo utakuwa unaongeza tatizo! Weka mtazamo chanya tu………
5. Illuminate.
Jiulize maswali kadhaa,je kuna mtu aliwahi kupata tatizo kama langu akalishinda?kuna mtu amewahi kupita kwenye nyakati ngumu kama hizi zangu akashinda?Je nimefukuzwa kazi au nimestaafishwa mapema?Je tatizo lako ni fedha kweli au ni matumizi mabaya ya fedha ulizo nazo hadi unafikiri hazitoshi?pengine unapaswa tu kubadili matumizi yako kisha utapata akiba,
6. Motivate.
Mtazamo chanya hupelekea suluhisho chanya,mfano kuna watu ambao ni walevi wa kupindukia,ulevi wake husababishwa na marafiki zake.Ukitaka kuacha ulevi sharti uachane na hao marafiki zako walevi……….ni swala la uamuzi sahihi kwa matokeo sahihi
Kuna wakati kwenye maisha unahitaji tu kufanya uamuzi sahihi ambao unatibu matatizo yako yote!
7. Bait.
Mwandishi anasema wakati mwingine unapswa kuwa kwenye sehemu sahihi kupata majibu sahihi,na matokeo tarajiwa,kuna watu kwenye maisha yao wapo sawa na mtu anayesubiria ndege itue baharini.Tambua sehemu sahihi ya kupata majawabu ya changamoto yako! Mfano unapenda kuvua sharti uende kwenye maji,mtoni,ziwani,baharini…huko ndio uvuvi hufanyika,pili unataka kuvua nini samaki gani,uende anakopatikana
8.Date.
Kama huna ajira na unahitaji kuajiriwa nenda katafute ajira kama mtu atafutavyo mchumba.Usijiwekee limit kuwa siku hizi hakuna ajira na zilizopo hadi uwe na fodfather wa kukushika mkono….Jiamini wewe ni godfather wa maisha yako,wewe ni shujaa wa maisha yako mwenyewe…usijikatishe tamaa ukitarajia kuna mtu atakuja kukutia moyo.Lazima utambue kuwa kila siku kuna mtu anastaafu au kuacha kazi hivo usikate tamaa
9. Sublimate.
Mlango mmoja ukifunga mingine inafunguka………..ifanye changamoto yako kuwa ngazi ya kupandia utukufu hadi utukufu
10. Now dedicate.
Watu wengi hushindwa sio kwa kukosa fursa,au kukosa akili au kipaji bali hushindwa kwa kuwa huwa hawashughuliki na tatizo husika bali dalili za tatizo.Ni lazima ushughulike na kiini…lazima uangalie mahali umejikwaa sio mahali umeangukia
Ukijitoa kwenye maisha ni ufunguo muhimu wa kufungua milango yako mingine…ukifanya kazi kokote fanya kwa bidi,na weledi utashangaa vile utafanya watu bora zaidi…unaweza kuwa muhudumu kwa mama ntilie ukamhudumia mteja kwa bidi na weledi kumbe huyu mteja ni mmiliki wa hotel ya nyota tano ukajikuta umepata ajira bila kuandika barua,bidi na weledi na kujitoa kwa moyo wote ni ufunguo tosha!
11. Communicate.
Usijimwambafai! Jifunze lugha bora ya mawasilano yenye mtazamo chanya.Mawasiliano ya kijamii ni moja ya njia bora za kutatua tatizo kwenye jamii.Kuwa mnyenyekevu wakati wote
12. Insulate.
Usijitenge wala kujificha ukiwa kwenye changamoto! Usianze kuwa kwenye mwonekano wa ovyo kwa kuwa tu una changamoto