Uchambuzi - Sheikh Ponda Issa Ponda

Uchambuzi - Sheikh Ponda Issa Ponda

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
23,263
Reaction score
33,866
JUHUDI YA SHEIKH PONDA ISSA PONDA KUNUSURU MALI ZA WAKFU ZA WAISLAM WA TANZANIA

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD]
IMG-20151018-WA0090.jpg
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Sheikh Ponda akifunguliwa pingu mahakamani[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Historia ya Waislam wa Tanzania itakapokuja kuandikwa jina la Sheikh Ponda Issa Ponda litaunganishwa na jina la Mufti Sheikh Hassan bin Amir kwa kitu kimoja nacho ni ardhi ya Chang'ombe Dar es Salaam ambako Waislam chini ya uongozi wa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) walikusudia kujenga Chuo Kikuu mwaka wa 1968. Katika uwanja huu ndipo Rais wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere akishuhudiwa na Tewa Said Tewa na Mufti Sheikh Hassan bin Amir aliweka jiwe la msingi la chuo hicho. Chuo hakikujengwa na EAMWS ikapigwa marufuku na serikali. Mambo hayakuishia hapo. Sheikh Hassan bin Amir akakamatwa na kufukuzwa nchini akarudishwa ''kwao'' Zanzibar. Serikali ikaunda BAKWATA na Chuo Kikuu cha Waislam hakikujengwa. Nini kilisababisha nakma hii? Waliokuwa karibu na Sheikh Hassan bin Amir wanasema katika siku zake za mwisho kila alipotajiwa ule mradi wa chuo kikuu alikuwa akilia na kusema ilikuwa hamu yake kujenga chuo Kikuu kama Azhar ya Misri na akifika hapo alikuwa akibubujikwa na machozi. Wakati ule Sheikh Hassan bin alikuwa na miaka zaidi ya 90 na aliishi na simanzi hizi hadi alipokufa mwaka 1979.

Kwa takriban miaka 40 Waislam wakawa wanapata taarifa kuwa ule uwanja ambao ulikuwa wakfu ulikuwa ukimegwa na viongozi wa BAKWATA na kuuziwa wafanyabiashara wakubwa matajiri.Waislam hawakuwa na uwezo wa kuzuia dhulma hii ikawa wao ni kulalamika tu na kila miaka ilivyozidi kwenda ndivyo kiwanja kile cha wakfu kilivyozidi kumegwa, kukatwa na kuuzwa. Ghafla siku moja Waislam wakasikia kupitia vyombo vya habari kuwa Sheikh Ponda na baadhi ya vijana wa Kiislam wamekwenda kwenye kiwanja cha wakfu na kutangaza kuwa wamekirudisha kwa wenyewe Waislam na watajenga Msikiti utakaoitwa Masjid Hassan bin Amir ikiwa ni kumbukumbu kwa mwanazuoni huyu wa Kiislam, mwanasiasa na mmoja katika watu waliokuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Ujenzi wa Masjid Hassan bin Amir ulianza ukiwa ni msikiti wa muda ''temporary,'' na Waislam walianza kuswali hapo. Haukupita muda askari waliwavamia wale vijana usiku wakakamatwa pamoja na Sheikh Ponda na kufunguliwa mashtaka. Waislam wale walipigwa na askari waliingia hadi Markaz pale na kuvunja baahi ya computer kwa kile kilichoelezwa kuwasaka wahalifu.

Hivi sasa karibu mwaka mmoja Sheikh Ponda kanyimwa dhamana na yuko rumande akisubiri kesi yake. Leo hii mwandishi alihudhuria kesi ya Sheikh Ponda kwenye Mahakama ya Mkoa Morogoro. Bahati mbaya palitokea purukushani kati ya Waislam na polisi. Wakati Sheikh Ponda analetwa mahakamani akisindikizwa na ulinzi mkali, alipofika langoni mmoja kati ya Waislam kama ilivyo ada alipiga ''takbir'' kwa sauti kubwa, ''Takbir.'' Waislam waliitika kwa sauti kubwa ya kishindo, ''Allahu Akbar.'' Inaelekea hili halikuwafurahisha polisi na askari mmoja akaagizwa amkamate yule aliyepiga ''takbir,'' hapo ndipo Waislam kwa umoja wao wakamkabili yule askari na vurugu ikatokea. Hata hivyo viongozi wa polisi alizungumza na Amir wa Waislam na utulivu ukarejea ingawa yule askari aliumia halikadhalika yule Muislam aliyekuwa akamatwe. Wote walikwenda kupata huduma ya kwanza hospitali ya mkoa. Lakini iko siku wote watasimama mbele ya Allah Hakimu Muadilifu na wao wataulizwa ni nani aliyestahili kuwa rumande akifungwa pingu na kuteseka yeye na familia yake. Ni yule aliyedhulumu haki ya Allah au yule aliyetaka kuinusuru?

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD]
20140430_151443.jpg
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Kwenye Uwanja wa Changombe Mwaka 1968 Mufti Sheikh Hassan bin Amir
Akimkaribisha Mwalimu Julius Nyerere Kuweka Jiwe la Msingi la
Chuo Kikuu Cha Waislam Kati yao ni Tewa Said Tewa[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD]
DSCN0626.JPG
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Sheikh Ponda Akizungumza na Mawakili Wake Kulia ni Advocate Nassor[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
u2Fnjp7znCj4HfhWHd0miJ8j37CXArHu80uVB8WAeN3A=w756-h567-no

DSCN0637.JPG

DSCN0652.JPG

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD]
DSCN0648.JPG
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Kushoto ni Mzee Bilali Rehani Waikela Muasisi wa TANU Tabora 1955,
Katibu wa EAMWS Jimbo la Magharibi na Inaaminika ni Yeye Peke Yake
Aliyehai Aneijua Historia Yote ya Kiwanja Cha Chang'ombe na Ujenzi wa Chuo
Kikuu Cha Waislam.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
DSCN0654.JPG

DSCN0659.JPG

DSCN0658.JPG

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD]
mbili.JPG
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Sheikh Ponda Akipelekwa Mahabusi Mwanzo wa Kesi Dar es Salaam[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD]
DSCN0656.JPG
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Waislam Wakiondoka Mahakamani kwa Maandamano

DSC03979.JPG

Picha ya Mwaka 2012 ya Sheikh Ponda Akisimama Kuomba Dua Mbele ya
Kibla Cha Msikiti wa Kichangani, Magomeni Dar es Salaam Kabla ya
Kuongoza Maandamano ya Waislam Kupinga Dhulma Dhidi ya Wanafunzi
Waislam Katika Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)

DSC04006.JPG
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

JEhT7Ttcu54H81zRVehBzP4pOguJUOrmGiPsAztuZVqBJpXtjSowOFMQF15q5Cb95AkPQbS9edGrvdCE9snVzOdIvD4KYjp__PlGSYSJIMZt9TIXXds5QIQEm7OaEFebvwh5dXUZDUhOqa1o=w506-h335

ponda+pingu.jpg

DSCN0880.JPG

Wajina, nazipenda sana bandiko zako! Una mawazo mapana na uwakilishi mzuri wa Maada.... Ila unaacha ? Ktk vichwa vya Wasomaji wako, je? Nn kifanyike kuondoa dhulma?
 
Mwenyezimungu atamlipa Sheikh Ponda kwa Juhudi zake za Kutetea Mali za Waislamu.
Huyu Sheikh ni mfano mkubwa sana wa Kuigwa na Kizazi hiki.
Na Serikali itambue kuwa Kila Wakifanyacho juu ya Huyu Sheikh kitakuja warudia wao kwa wao.
Haki ya mtu haipotei bure. Iko siku watayaona haya madhila wanayompa huyu muungwana.

Mungu yuko pamoja nae hata km MAKAFIRI watachukia.

Shukran sana Mzee Mohamed kwa Taarifa hii
 
Aalim endelea kutoa bayana.
Nimekuza maandishi ili yasomeke kwa wepesi.
 
Hii makala ya zamani kama inasema Sheikh Ponda amefungwa mwaka mmoja. Nakumbuka miaka miwili iliyopita Butiama nilikuwa naongea na waandishi wa habari naiomba Serikali imuachie huru Sheikh Ponda.Niliongea kuhusu mambo mawili siku ile:Magufuli na Sheikh Ponda. Kuhusu Magufuli watu walikuwa wameanzisha vugu vugu la kumfukuza kazi wanasema Magufuli hana rafiki,kazi yake kubwa ni kusema,hii nyumba imejengwa karibu na barabara,nataka ibomolewe. Nikaongea kumtetea Magufuli. Kuhusu kuwafunga Waislamu hii siyo mara ya kwanza.Wakati katika kampeni ya Mkapa walikuwepo Waislamu waliofungwa kwa akili ya maandamano. Na mimi nilisema wakati ile CCM sasa hivi haina tatizo kubwa kuliko wale Waislamu waliofungwa. Na ni nasema wale Waislamu wataachiwa huru kabla ya siku ya kupiga kura. Na kweli ndiyo ilivyokuwa wale Waislamu waliachiwa kabla ya Uchaguzi..
 
Wajina, nazipenda sana bandiko zako! Una mawazo mapana na uwakilishi mzuri wa Maada.... Ila unaacha ? Ktk vichwa vya Wasomaji wako, je? Nn kifanyike kuondoa dhulma?
Somo yangu Mudy panya hafunzwi kula sufi. Wewe ni lilulalbab. Mja mwenye akili.
 
Wewe mzee hapa ndipo unaponichosha. Wakati huu wa uchaguzi tuna nafasi kubwa ya kuwang'oa CCM na kukaribisha chama kipya tunachoweza kukidhibiti (kwa njia ya kura maana hakitakuwa na mizizi mirefu kama CCM). CCM ndiyo inayolea hii dhuluma, ungana na watanzania wengine na kuwahamasisha CCM itoke. Lakini wapi bwana, umekaa kimya sana kuhusiana na uchaguzi huu adhimu. Utakuja kuibuka baada ya mwaka mmoja kwa kasi kubwa kupinga mfumo kristo wakati chama dhulumati mnakiacha kishinde hata kwa bao la mkono.
 
Ungewakumbusha wamchague Raisi mwenye hofu ya Mungu aliyewasaidia waislamu hata kabla ya kugombea Lowassa
 
Wajina, nazipenda sana bandiko zako! Una mawazo mapana na uwakilishi mzuri wa Maada.... Ila unaacha ? Ktk vichwa vya Wasomaji wako, je? Nn kifanyike kuondoa dhulma?
....hilo wala auhitaji kumuuliza muft kaka.....sbb dhulma ya kwanza ni ile tunayojifanyia wenyewe kwa kukosa umoja na mshikamano...! Labda swali ni kujua mawazo ya mwandishi juu ya kiini cha kukosa umoja na mshikamano miongoni mwa waumini...
 
Wewe mzee hapa ndipo unaponichosha. Wakati huu wa uchaguzi tuna nafasi kubwa ya kuwang'oa CCM na kukaribisha chama kipya tunachoweza kukidhibiti (kwa njia ya kura maana hakitakuwa na mizizi mirefu kama CCM). CCM ndiyo inayolea hii dhuluma, ungana na watanzania wengine na kuwahamasisha CCM itoke. Lakini wapi bwana, umekaa kimya sana kuhusiana na uchaguzi huu adhimu. Utakuja kuibuka baada ya mwaka mmoja kwa kasi kubwa kupinga mfumo kristo wakati chama dhulumati mnakiacha kishinde hata kwa bao la mkono.

Sooth,
Ukianza na ''Wewe Mzee...'' ni kuwa umeghadhibika na umetokwa na staha.
Ukishaniita, ''Mzee,'' basi tambua nastahili heshima.

Bila ya heshima hatutaweza mimi na wewe kufanya mjadala wa maana.
Labda ukisoma hapa chini tutaelewana kuhusu uchaguzi:

http://www.mohammedsaid.com/2015/10/mbunge-mtarajiwa-wa-newala-jaffar-mneke.html

http://www.mohammedsaid.com/2015/09/is-terrorism-pawn-for-general-election.html

http://www.mohammedsaid.com/2015/08/kutoka-jf-waislam-na-uchaguzi-mkuu-2015.html
 
Wewe mzee hapa ndipo unaponichosha. Wakati huu wa uchaguzi tuna nafasi kubwa ya kuwang'oa CCM na kukaribisha chama kipya tunachoweza kukidhibiti (kwa njia ya kura maana hakitakuwa na mizizi mirefu kama CCM). CCM ndiyo inayolea hii dhuluma, ungana na watanzania wengine na kuwahamasisha CCM itoke. Lakini wapi bwana, umekaa kimya sana kuhusiana na uchaguzi huu adhimu. Utakuja kuibuka baada ya mwaka mmoja kwa kasi kubwa kupinga mfumo kristo wakati chama dhulumati mnakiacha kishinde hata kwa bao la mkono.

Kijana we huna wazazi?
Laanakum.

Babako huwa unamuita "we mzee"

Upuuzi wako wa siasa peleka Huko hapa tunamuongelea Muaddham Al Sheikh Ponda .

Ukizidi kukosa adabu Sasa hivi utashangaa umepigiwa hodi na Askari kanzu.
Bata mzinga.
 
Wewe mzee hapa ndipo unaponichosha. Wakati huu wa uchaguzi tuna nafasi kubwa ya kuwang'oa CCM na kukaribisha chama kipya tunachoweza kukidhibiti (kwa njia ya kura maana hakitakuwa na mizizi mirefu kama CCM). CCM ndiyo inayolea hii dhuluma, ungana na watanzania wengine na kuwahamasisha CCM itoke. Lakini wapi bwana, umekaa kimya sana kuhusiana na uchaguzi huu adhimu. Utakuja kuibuka baada ya mwaka mmoja kwa kasi kubwa kupinga mfumo kristo wakati chama dhulumati mnakiacha kishinde hata kwa bao la mkono.

CCM NA CHADEMA wote hawana nia nzuri juu ya waislam na uislam wao.ndio maana GWAJIMA anataka kubadili misikiti tunayoabudia kuwa shule yeye na maswahiba zake.huu uonevu tutautoa sisi wenyewe waislamu tutapoipiga BAKWATA chini
 
Ungewakumbusha wamchague Raisi mwenye hofu ya Mungu aliyewasaidia waislamu hata kabla ya kugombea Lowassa

acheni kutuletea siasa zenu hapa hakuna raisi mwenye khofu na mungu hapa tanzania.LOWASSA alikuwa hawasaidii bali alikuwa anahonga ili aje atughiribu akili zetu na rushwa yake. LOWASSA NA GWAJIMA NA CHADEMA YENU NA CCM YENU PELEKENI HUKO. hapa ni uislam wenye msimamo thabiti na amiri wetu PONDA
 
Ni Kweli Kabisaa Hilo Ndilo Chimbuko La Sheikh Ponda Issa Ponda Kuandamwa Na Vyombo Vya Dora!! Lkn SWALI, Hivi Kama Hili Suala Halina Mkono Wa BAKWATA, Ambao Ndio Walitoa Maagizo Ya Kumdhibiti Sheikh Ponda, Kutokana Na Kusimamia Kwake Kwa Dhati Mali Za Waislam, Ili Ziweze KULETA Maendeleo Kwa Jumuiya Nzima Ya Waislam Na Dini Yao!! Badala Ya Kutumiwa Na BAADHI Ya Viongozi Wa BAKWATA Kwa Maslahi Yao BINAFSI!! Najiuliza Hivi DPP ANAWEZA Vipi KUZUIA DHAMANA Ya Sheikh Ponda!! Kwa Zaidi Ya Mwaka Mzima, Huku BAKWATA WAMEKAA Kimyaa!!! Kama Lenyewe Ndilo Baraza Kuu La Waislam Wa Tanzania!!! Iweje Sheikh Ambaye ANAYESEMA UKWELI Na Kuwatia Hamasa Waislam Wenziwe Kudai Mali Zao Zilizoporwa, Anakamatwa Na Waumini Wenziwe Na Kufunguliwa Mashitaka Ya Wizi, Wa Nondo, Kokoto, Matofali, Mchanga, Mbao, Mabati Na Misumari!! Na Kunyimwa DHAMANA Pale Mahakama Ya Kisutu!! Hadi Hukumu Ilipotoka Sheikh Ponda Akafungwa Kifungo Cha Nje Mwaka 1 Na Waumini Wengine Cha GEREZANI!! Wkt. Sheikh Ponda AKIENDELEA Na Kifungo CHAKE!! Ndio Yakazuka Hayo Ya Moro!! Eti Anashitakiwa Kwa Kukiuka Masharti Ya Hukumu Ya Mahakama Ya Kisutu!! Na KUFANYA Mkutano Usio Na Kibali, Kusema Maneno Ya UCHOCHEZI Na Yenye Kuudhi Watu Wengine!! Tukashuhudia Sheikh Ponda Akisafirishwa Kwa CHOPA Toka SEGEREA Mahabusu, Kwenda MAHAKAMANI Moro, Mara IKAWA Kwa Msafara Wa Magari!! Hatimaye Mahakama Ya Kisutu Akalitupa Shitaka La Kukiuka Masharti Ya Hukumu Ya Kifungo Cha Nje, Iliyotolewa Nayo!! Imebakia Hayo Ya Moro!! Ndio Akahamishiwa Mahabusu Ya Moro HADI Leo, Ambapo Ndio Tarehe Ya Hukumu Yake!!! Kama BAKWATA Haina Mkono Ktk. Kadhia Hii, Mbona Wako Kimyaa!!!?? Je, TAASISI Hiyo Sio Ya Waislam Na Mali Zao!!!??? Je, BAKWATA Iko Kwa Maslahi Ya Waislam Wa Aina GANI TANZANIA!!!?? Nini Kifanyike, Kwanza Waislam Wa TANZANIA Tudai Baraza La Waislam Wa TANZANIA Lenye MFUMO Ambao Linashirikisha Waislam WOOTE, Taasisi Zoooote, Jumuiya Zoooote Na Madhehebu Yooote!! Pili Kuundwa Kwa Baraza Lenye Sura, Malengo, Fikra, Mtazamo Na UMOJA! Kwa Kuwashirikisha Waislam WOOTE NCHINI, Ktk. Mchakato Wa Undwaji Wake Na Kupatikana Viongozi Wake!! SIO KAMA ILIVYO Sasa, WATU WACHACHE Ndio Wanaamua Na Kusimamia Mambo Ya Waislam WOOTE NCHINI!! Tatu Waislam Tuache UNAFIKI, Huu Ndio Unaotutafuna Jmn! HIVI Madhira YOTE Haya, Tokea Miaka Ya 90 Pale Wahadhiri Wa Kiislam Walipofungwa Miaka 3 GEREZANI Kwa Mashitaka Ya Kuvunjwa Mabucha Ya Nyama Ya Nguruwe!! Ambao Wakikamatwa Pale Msikiti Wa Mwembechai, Akiwepo Na Sheikh Mazinge Shaban! Baadae Wakaachiwa Kwa Msamaha Wa Rais MWINYI!! Lkn Likifika Suala La Uchaguzi Wa Viongozi, Tunaonekana Kuyumbishwa Na Maslahi YETU BINAFSI Badala Ya WOOTE!!! Kama TUTAENDELEA Kuwa WANAFIKI Tu, Basi Tukubali Tu Kudhurumiwa Na Kunyanyasika MILELE!!!!!
 
Hawa jamaa pamoja na kuonewa kote na ccm ila walikuwa kimya sana , naona wameamka tena .duh!
 
Hii makala ya zamani kama inasema Sheikh Ponda amefungwa mwaka mmoja. Nakumbuka miaka miwili iliyopita Butiama nilikuwa naongea na waandishi wa habari naiomba Serikali imuachie huru Sheikh Ponda.Niliongea kuhusu mambo mawili siku ile:Magufuli na Sheikh Ponda. Kuhusu Magufuli watu walikuwa wameanzisha vugu vugu la kumfukuza kazi wanasema Magufuli hana rafiki,kazi yake kubwa ni kusema,hii nyumba imejengwa karibu na barabara,nataka ibomolewe. Nikaongea kumtetea Magufuli. Kuhusu kuwafunga Waislamu hii siyo mara ya kwanza.Wakati katika kampeni ya Mkapa walikuwepo Waislamu waliofungwa kwa akili ya maandamano. Na mimi nilisema wakati ile CCM sasa hivi haina tatizo kubwa kuliko wale Waislamu waliofungwa. Na ni nasema wale Waislamu wataachiwa huru kabla ya siku ya kupiga kura. Na kweli ndiyo ilivyokuwa wale Waislamu waliachiwa kabla ya Uchaguzi..

Andrew,
Hii makala niliiweka tarehe 5 Januari 2015 kwenye blog yangu:
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...uzi-sheikh-ponda-issa-ponda.html#post14384143
 
Back
Top Bottom