Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 12,151
- 44,071
Kituko kipya cha karne katika siasa za Tanzania kimeibuka leo, baada ya Ikulu ya Tanzania kuitangazia dunia kuwa, Rais wa nchi amelipa kiasi cha shilingi milioni 38 ili kumlipia faini Mchungaji Peter Msigwa ambaye ni mfungwa wa kisiasa aliyetiwa hatiani kwa makosa ya jinai.
Sina uhakika kama Ikulu ilikuwa inajua kuwa kitendo ilichokifanya leo kilikuwa ni cha kitoto, kijinga na kituko mbele ya macho ya dunia na watanzania wengi.
Sababu za msingi kabisa ni hizi hapa.
1/Mchungaji Msigwa alishtakiwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inaongozwa na Rais wa Tanzania.
(Kwa maneno rahisi kimantiki ni kuwa Rais wa Tanzania alikuwa anamshtaki raia anayeishi Tanzania).
Sasa nini mantiki ya Jamhuri (Raisi) kumshtaki raia ili afungwe na kisha hapo hapo kuja kumlipia faini ili aachiwe huru?
Kwanini Jamhuri ipoteze muda, nguvu kazi ya mawakili wake, mshtakiwa na mahakama katika kuiendesha kesi hiyo kwa zaidi ya miaka 2 mfululizo wakati ikijua fika ilikuwa haina nia ya kumfunga Msigwa gerezani?
2/Rais wa Tanzania kikatiba anayo mamlaka ya kumwachia huru wakati wowote, mfungwa yoyote kutoka kifungoni.
Kwanini Rais akimbilie kumlipia pesa Msigwa badala ya kuamuru aachiliwe huru tu?
3/Mchungaji Msigwa alikuwa akitetewa na mawakili wake kutoka CHADEMA wakati wote wa kesi, na mara baada ya kutiwa hatiani, mawakili hao hao ndio waliweka utaratibu wa namna ya kukusanya pesa kupitia CHADEMA ili mchungaji Msigwa aweze kuachiliwa huru.
Kipi kimewafanya watendaji wa Ikulu kuibuka sasa kumpigania Msigwa baada ya kufungwa gerezani na sio wakati wote wa kuendeshwa kesi dhidi yake?
Nini kimeifanya Ikulu kuukwepa huo utaratibu wa Mawakili wake katika kulipa faini?
Nani kawatuma Ikulu kwenda kujipendekeza kwa Msigwa nje ya utaratibu wa wanasheria wa Msigwa?
Nini kitatokea ikiwa Msigwa atakuja hadharani kuwakana Ikulu?
4/Watanzania wengi wanajua na kuamini kuwa kesi yote hii iliyomtia hatiani Msigwa na wenzake ina mkono wa serikali, vyombo vya dola na CCM.
Sasa hii janja janja ya Ikulu kumlipia faini Msigwa ina lengo gani?
Kulikuwa na ulazima gani kwa Ikulu kuja kujikocha hadharani kwa mtindo wa namna hiyo?
5/Katika mazingira ambayo CHADEMA inarindima katika miamala ya fedha ya kona zote za nchi ili kuchangishana pesa za kuwatoa viongozi wao wote (pamoja na Mashinji ambaye amehama CHADEMA).
Nini mantiki ya Ikulu na CCM ghafla kuibuka na kudai na wao wamechanga pesa ili kuwatoa kifungoni baadhi ya viongozi hao?
Je, Ikulu imeamua kuiga utaratibu wa CHADEMA?
Je, Ikulu ina hofu au wivu kwa huo utaratibu wa CHADEMA?