Uchambuzi: Bomba la mafuta ya wizi Ungindoni, Kigamboni

Mkuu unaota ,unakula ,unalala wewe ni awamu ya tano tu,sema ulichokosewa au ulichokikosa, sidhani kama itakusaidia sana kila siku kujadili na kulaumu awamu ya tano,wewe si ulikuwepo ulifanya nini baada ya kuona hayo mapungufu na mchango wako ni upi, kila siku unabwata tu awamu ya tano eh awamu ya tano.
Bado tu unamtetea yule dictator?
 
Kwa kweli inatisha sana, Binafsi nilishtuka sana. Huu ni wizi wa kimkakati sana.

Nilishawahi kusoma wizi wa dizaini hii. Lakini ile wanasema wezi walichimba ardhini kwa kuchoronga hadi wakaibukia benki... Wakachota fedha za kutosha.

Nadhani ni Brazil, mji wa Fortaleza. Hiki kisa sijui nilikisoma humu?
Hii ya kutoboa mabomba ya mafuta na kuiba sio ngeni watoto wa Mexico mafia wa narcotics wanafanya Sana hii kitu huko hata Niger Delta Kule Nigeria hizi ishu za kawaida kabisa Tu ,ni jinsi Tu ya kujua Kula na kipofu
 
Umeandika maelezo meeengi sana lakini point muhimu iko moja tu, ''ukijua hivi wenzako wanajua vile na kinyume chake''

Mheshimiwa Rais alikuwa na nia nzuri sana kwa nchi yetu amejitahidi sana kudhibiti lakini kama alivyosema mwenyewe vita ya uchumi ni ngumu sana lazima ujitoe si kimataifa tu hata ndani ya nchi kulikuwa na vita ya kiuchumi yaani wapigaji walikuwa hawampendi na walijitahidi kutafuta viongozi ambao si waaminifu kutekeleza hujuma dhidi ya rais na juhudi zake sasa yeye kama yeye asingeweza kuzibiti kilaeneo wakati kuna wanaompinga katika vitahii wanataka waendelee kupiga.
Hakuwa na lolote alikuwa mpigaji tu kama alitaka kupambana na ufisidi asingezuia vyombo vya habari vyenye akili nakuua mihimili minginr
 
Tatizo uzalendo wetu wa kitanzania hauwezi kuufananisha na Uzalendo wa Mmarekani.
kwanini kuna tofauti?
wezetu uzalendo kwa nchi yao unapandikizwa/kufundishwa kwa watoto kuanzia chekechea, tena unafundishwa na wazalendo walio iva.
sisi huku tunaanza kumfundisha Uzalendo mtu aliye kubuhu kwenye wizi!!, ubadhirifu!!!
uozo! uozo kila mahali.
unaweza kuta mpaka ikafikia kufahamika uhalifu huo wa wizi wa mafuta kuna mtu miongoni mwa wakubwa karukwa au kanyimwa mgao ndipo kaamua kuchomoa betri!!!
Uzalendo kwa Taifa letu uanze kufundishwa kwa bidii kuanzia chini kabisa sambamba na elimu ya Maadili hapo ndipo kizazi chetu kitafurahia matunda ya rasilimali za Taifa letu.
hata hivyo wapo viongozi wachache ambao kweli ni wazalendo wa kweli, na hao ukichunguza sana maadili yao yanatokana na historia ya elimu aliyo ipata/shule alizo soma n.k, japo na wao hufika wakati wanazidiwa nguvu na mfumo corrupts na hivyo huachia goli.
watu wachafu na waovu ni wengi zaidi kuliko watu wema na waadilifu. hii ni hatati sana.
Uzalendo haufindishwi uzalendo inatakiwa kuanzia kwa watawala huwezi kuniambia niwe mzalendo ikiwa mtawala anaua watu wake eti kwa vile wanampinga anakwiba rasilimali anajenga kwao ikiwa Kuna mtu hajui mwanae atarudije Shule kwa kukosa ADA
 
Kwa kweli inatisha sana, Binafsi nilishtuka sana. Huu ni wizi wa kimkakati sana.

Nilishawahi kusoma wizi wa dizaini hii. Lakini ile wanasema wezi walichimba ardhini kwa kuchoronga hadi wakaibukia benki... Wakachota fedha za kutosha.

Nadhani ni Brazil, mji wa Fortaleza. Hiki kisa sijui nilikisoma humu?
Ipo documentary yake, lakini na wao walikopi ilishatokea kitambo nadhani uingereza
 
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya muunganiko! MATAGA pia natumai hamjambo!

Rejea mada hii: BLINDSPOT: Uchochoro wa kupiga popote

Kukamatwa kwa bomba hili kwa bahati nasibu tuu ni mwendelezo wa ufunuo wa udhaifu wa serikali ya awamu ya tano iliyojinasibu kudhibiti wizi, rushwa, upigaji na ubadhilifu...! Ukijua hivi wenzako wanajua vile na kinyume chake.

Leo nitaandika mada ndefu kidogo kuhusiana na hili kwakuwa kwa namna moja au nyingine linagusa usalama wa nchi na ya kwamba kwenye hili hatupaswi kuaminiana ama kumuamini yoyote hata awe na pesa na ukwasi kiasi gani.

Tukumbuke ya kwamba waliofanikisha kujenga lile bomba la wizi wa mafuta toka bomba la serikali si watu wa kawaida bali ni mtandao wa watu wenye akili kubwa,hela, vitendea kazi vya kisasa, wataalam wa kuchimba, wasoma ramani nknk

Hebu tupitie dondoo hizi:

1. Eneo la upigaji ni nyumba ya kupanga/kupangishwa
Ni eneo la kimkakati kutokana na ujenzi wake! Eneo kubwa lililozungushiwa ukuta mrefu kotekote! Ndani kukiwa na nyumba moja tuu.. Je kuna uhusiano gani kati ya mmiliki na mpangaji? Je hawezi kuwa mtu mmoja mwenye sura mbili!? Cha kushangaza zaidi eneo linatazamana na serikali ya mtaa Ungindoni, kinachowatenganisha ni barabara tu!

2. Usalama wa nchi na raia
Kigamboni ni eneo la kimkakati kwenye usalama wa nchi na raia pia na serikali imewekeza sana kule, kuna kambi ya jeshi na ofisi za vitengo vya usalama.. Lilipaswa kuwa eneo la kuogopwa na wapigaji wakubwa! Sasa ninini kilitokea hapa mpaka watu wanatoboa ardhi mpaka kulifikia bomba na kunyonya mafuta kwa miaka miwili kasoro bila kustukiwa na organ za usalama?

3. Mfadhili na mmiliki wa huu mradi si mtu mdogo asilani
Na pengine ni mojawapo wa matajiri wenye kumiliki kadi ya kijani na mfadhili wa chama na viongozi wake. Pengine ni mmojawapo wa matajiri anayeheshimiwa na pengine kuogopwa na viongozi wetu na pengine ana miliki cheti cha mlipakodi mkubwa mzuri kupitia miradi mingine aliyoanzisha kwa kutumia pesa za kutakatisha za wizi wa mafuta.

4. Kikosi kazi kilichotekeleza ule mtobozano ni kikosi toka nje ya nchi kwa vyovyote kilichokuwa na kila nyenzo ya kisasa zikisaidiwa na mashine za kutoboa visima virefu In fact kazi ilifanywa na watu wachache na mitambo ya kisasa kwa kutumia computer tu. Yaani vitu vinasetiwa toka umbali wa bomba lilipo, uchorongaji nknk. Watu wako kwenye AC na vikombe vya NIDO kama wanaangalia movie.

Hakuna jambo linalokosa asili. Ilianza kule Tegeta nadhani kuna watu walikamatwa kwenye nyumba nao wakiwa wamejiunganishia bomba lao toka bomba kuu na wakawa wanakula maisha kwa kwenda mbele. Hawa walikuwa level one au shule ya msingi.

Akaja kukamatwa tajiri aliyeibuka ghafla, Princess Muro akiwa na mabasi ya kusafirisha abiria mengi tu na vituo vya mafuta vilivyokuwa vinachipua kama uyoga. Kumbe huyu naye alikuwa kajiunganishia bomba lake la mafuta toka bomba kuu la serikali. Alikamatwa na kufilisiwa nadhani. Huyu ni level two au shule ya sekondari.

Huyu aliyekamatiwa vitu vyake Kigamboni yeye tunamuweka level 3 au chuo kikuu alisoma makosa ya waliotangulia akafanya marekebisho mengi akafanya yake!

Je, kutakuwa na level 4? Muda utasema!

Uzalendo ni kitu kikubwa sana. Uzalendo ni zaidi ya kuvaa scalf na nguo zenye rangi ya taifa, uzalendo ni zaidi ya kusimama majukwaani na kuhubiri. Ule wizi wa Kigamboni una mkono wa Watanzania wengi tu mle ndani na wengine pengine wakiwa na dhamana ya ulinzi na usalama wa nchi lakini wote wakapiga kimya!

Aakari waliokamata ile gari iliyopelekea kubumbuluka kwa wizi huu mkubwa sijui watapewa zawadi gani. Lakini hata hivyo pamoja na serikali kuishia kutaifisha ile nyumba na magari na ile mitambo sidhani kama wamiliki halali wa ule wizi watakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria, sana sana watakamatwa vijana wetu wasiojua mengi.

Kama hujui jamaa kapiga bei gani kwenye huu wizi angalia hizi hesabu. Na kama zikija kupatikana hesabu halisi huu unaweza kuja kuwa upigaji mkubwa kuja kutokea Tanzania.

Nakupa hesabu kwa uchache tuu na bei ya chini kabisa:

Kama kwa siku alivuna tanker kumi tu za lita elfu 10 kila moja na akaenda kuuza kila lita moja kwa sh. 1000 tu,
  • Kwa siku moja alikuwa anaingiza kwa uchache milioni 100 kumi za Kitanzania
  • Kwa wiki milioni 700
  • Kwa mwezi bilion 2.8
Piga kwa mwaka au miezi 20 aliyofanya kazi

Sitaki kuongelea ya Mkuu wa Wilaya ambaye alikuwa hajui jina hata moja ya vile vifaa vilivyotumika pale. Hivi kwanini hawakumuandaa? Walimkurupusha tu au alikurupuka? Hivi kweli DC anashindwa kusema hata welding machine?

Eneo lote lilikuwa na camera na ulinzi mkali 24/7, hivyo miliiki alikuwa anaona kila kitu. Mpaka DC na timu yake yote alionekana bila chenga. Hii ni big mistake! Walimpa nafasi bora sana ya kujipanga ama kukimbia.

Anyway, upigani ni jadi hasa kwa Taifa kama Tanzania na pengine hili nalo litapita kama mengine yote.
Iliwezekanaje Kujulikana kuwa Shughuli hiyo Ina miaka miwili toka imeanza!!??
 
Hii habari inaweza kuishia humu humu jf
Imeshaisha mkuu!

Na kuna makubwa zaidi yanakuja!

Enzi za kikwete itakuwa cha mtoto!

Watu wenyewe tupo busy kumsagia diamond sumu ila kwenye ishu nyeti kama hizi hamna kitu
 
Back
Top Bottom