masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,173
- 13,776
Sintofahamu ya chama kikuu cha CUF huko Zanzibar kutoshiriki uchaguzi wa jana tarehe 20/3/216 kunaweza kuibaua mabadiiko makubwa katika siasa za visiwani humo.
Sasa hivi kiongozi anayejulikana sana medaniza kisiasa na anayeonekana mbadala wa Maalim Seif ni Hamad Rashid, na alikuwa hasimu wa Maalim ndani ya CUF hadi alipoondolewa na kuondoka kuunda chama chake, ADC(Alliance for Democratic Change).
Itabidi waangalizi wa kisiasa waendelee kusubiri. lakini Hamad Rashid kwa hali inavyokwenda anaweza kuwa Makamu wa Rais, na kuchukua nafasi au ombwe la Maalim Seif Sherrif Hamad.
Wadau, maoni yenu