Uchaguzi Zambia

Jul 8, 2013
47
65
Kampeni za mwisho mwisho za Uchaguzi mkuu wa Zambia unaotarajiwa kufanyika Agosti 11 zimeshika kasi. Kampeni hizi hazijacheza mbali na mmoja wa wanasoka bora kuwahi kutokea barani Afrika, KALUSHA BWALYA. Yu katika timu maalumu ya kampeni ya mgombea urais wa Chama Tawala PF (Patriotic Front) Edgar Lungu ambaye anachuana vikali na Hikainde Hichilema wa UPND (United Party for National Development). Tangu ipate uhuru mnamo mwaka 1964 kutoka kwa Uingereza vyama vitatu vimetawala Zambia hadi sasa.

UNIP 1964-1991 Keneth Kaunda(Rafiki wa dhati wa Mwl. Nyerere )baada ya shinikizo kubwa la kuanzishwa kwa vyama vingi aliridhia na kuitisha uchaguzi ambao ulihitimisha miaka 27 ya Chama chake.

MMD 1991-2011 Chama hiki kiliasisiwa na Frederick Chiluba rais wa pili wa Zambia. Baada ya miaka 20 ya utawala wake wananchi wa Zambia wakakiweka benchi na kuingiza mchezaji mpya.

PF 2011- SASA Baada ya kuhangaika UNIP, MMD na kushindwa kupewa fursa ya kugombea urais Michael Satta alianzisha chama chake na kukiita Patriotic Front (PF) NA baada ya kujaribu mara tatu, mwaka 2011 Wananchi wa Zambia (Taifa jirani na Tanzania )walifanya 'sub' kwa kukipumzisha MMD na hivyo kuhitimisha miaka 20 ya utawala wa Chama hicho.

KAMPENI
Kampeni ni kali hasa kati ya Lungu na Hichilema. Agenda kuu zikiwa rushwa, ukosefu wa ajira, umaskini uliotopea n.k
 

Attachments

  • 13754475_1022493991201959_2566801193780281504_n.jpg
    13754475_1022493991201959_2566801193780281504_n.jpg
    61.6 KB · Views: 37
wanasema ktk afrika hiyo nchi nayo inajitahidi sana kwenye maswala ya demokrasia ijapo kuwa umaskini bado uko pale pale. lakini waakomae labda ipo siku watatoka.
 
Back
Top Bottom