Uchaguzi wa serikali za mtaa: Wakurugenzi watano wafukuzwa kazi

Pia ghasia anatakiwa kuondoka mara moja kwenye uwaziri, kwenye uchaguzi huu kila wilaya imelipa tofauti waliosimamia uchaguzi ule, wengine wamelipwa 50000 toka uandikishaji mpaka usimamizi wa kura, wengine wamelipwa 100000 toka uandikishaji na upigaji kura. Pinda na mawaziri wanaohusika waondoke mara moja.
 
Hawa wamehatarisha kitumbua cha chama lazima watimuliwe Mara Moja, ila waliopitisha mapingamizi na kuwaengua wapinzani wanasubiri kupewa ukuu wa mikoa.

dhaifu gvment
 
Hakika huu ni uonezi kwasababu uzembe umeanzia ngazi za juu...nilikua Kwimba na nimeona hali halisi.
Huu ni utaratibu wa serikali yetu kuwaacha SAMAKI na kuvua dagaa!!! Shame on you!!
 
Kwa hiyo ni wilaya 17 zimejisahau katika uchakuaji nyingine walifanikiwa. hongera escrow. kizazi cha panya
 
kiongozi akifanya kazi yake mnamlaumu..asipofanya mnamlaumu...mnahitaji nini nyie....uchaguzi si tukio la ghafla DED anashindwaje kujipanga usambazaji wa vifaa kwa wakati...hongera mama ghasia if its true..good move...
 
habari wakurugenzi watano wasimamishwa kazi!

serikali imetengua uteuzi wa wakurugenzi sita wa halmashauri, na kuwasimamisha kazi wengine watano kupisha uchunguzi, kutokana
na kubainika kuchangia kuvurugika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa, uliofanyika tarehe 14, mwezi huu.

Akitangaza hatua hiyo kufuatia ripoti iliyoibua madudu yaliyofanyika katika uchaguzi huo waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu, tawala za mikoa na serikali za mitaa (tamisemi) mhe. Hawa ghasia amesema uamuzi huo pia umeridhiwa na rais jakaya kikwete.

Mhe. Ghasia amewataja halmashauri ambazo wakurugenzi hao waliotenguliwa uteuzi wao kuwa ni za mkuranga, kaliuwa, kasulu,
serengeti, sengerema na bunda, waliosimamishwa kazi ni wakurugenzi wa hanang', mbulu, ulanga, kwimba pamoja na wa manispaa ya sumbawanga.

Waziri ghasia amesema kuwa wakurugenzi wengine watatu wapewa onyo kali, ambao ni wa rombo, busege na muheza na wengine
watatu wakipewa onyo la kawaida, wakurugenzi hao ni wa manispaa ilala, hai na mvomero.

my take
mwaka huu kila mtu atakuwa mamluki nabadooooo


acha watimuane ...lakini kuna wakurugenzi esp wa dar ...wamepewa onyo kinafiki kwa kuwa walikuwa wamepewa firm instruction kuvuruga uchaguzi baadhi ya maeneo ambayo ccm walikuwa na hali mbaya .....mfano matumbi,vingunguti ..etc ...tabata kwenye magarage ....mgombea wa chadema ..jina moja limepatikana anaitwa mbegga ...alishinda lakini ...mtendaji alishinikizwa kumtangaza mgombea wa ccm [Akisimamiwa na makongoro mahanga na polisi ]...na wajumbe wake ...hali mtaani ni ya malalamiko sana ..hata huko tanga ambako mkurugenzi aliyevuruga uchaguzi jina lake halipo ......

Naona hapa huyu bibie anajikosha ili kupooza hasira na kufunika kombe...kubwa ni waliofukuzwa pengine ni wale waliopoteza viti
 
Back
Top Bottom