Uchaguzi wa mwaka huu, walimu tusirudie makosa

MR. MORRIS T. J.

JF-Expert Member
Apr 18, 2013
1,167
402
Madai Ya Kujengewa Nyumba,mishahara Kuboreshewa,malimbikizo Ya Mishahara,kuboreshewa Mafao Yetu, Masurufu Ya Kazi Yupo Mtu Mmoja Tu Mwenye Kuweza Kuyakabili Hayo.

Mtu Huyo Alishaianza Kazi Hiyo.Alianza Kwa Kujenga Shule Za Kata Zaidi Ya 2000 Ndani Ya Miezi. Je, Angekaa Miaka Mitano Hali Ingekuwaje?

Tangu Ameondoka Hadi Leo Hakuna Shule Ya Kata Hata Moja Iliyojengwa Na Hata Zile Zilizopo Hadi Sasa Hazina Waalimu!

Mtu Huyo Anaitwa TUMAINI LETU WANYONGE EDWARD NGOYAI LOWASA.Na Kama CCM Wasipompitisha Msihofu Tunae Mkombozi Mwingine Ni Dr Wilbroad Peter Slaa.

KUHUSU WABUNGE CHAGUENI WOTE KUTOKA UKAWA na CCM MUMBAKISHE OLE SENDEKA.

Mkifanya Hivyo Madai Yenu Yatabaki Historia.
 
Umepatia kasoro mwanzo tu, Lowasa hafai hata kuongoza shule ya kata. Huko kwingine uko sawa, walimu ni mtaji mzuri wa ccm, sasa badilikeni
 
We lazima utakua mmasai tu......wamasai wamekua wakimpigia lowasa kampeni sijui hata kwa nn....ni wabinafsi sana...mbona kikwete aliagiza maabara zijengwe kwenye shule zote za kata husemi...
 
Walimu ni wafanyakazi waoga sana, wakipewa viposho kidogo tu hasa wakati wa uchaguzi wanaharibu mipango ya kuwaondoa viongozi wabovu.
 
We lazima utakua mmasai tu......wamasai wamekua wakimpigia lowasa kampeni sijui hata kwa nn....ni wabinafsi sana...mbona kikwete aliagiza maabara zijengwe kwenye shule zote za kata husemi...

J.K. Ni Kweli Kaagiza Zijengwe, Lakini Waalimu Wamekatwa Kwa Lazima Kwenye Mishahara Yao Kati Ya Sh. 25000 Na 60000 Ndo Maana Niliwahi Kuhoji Hapa Kasimu Majaliwa Anakatwa Ngapi Kuchangia Maabara? Je Watumishi Wa Kada Zingine Nao Wanakatwa Ngapi?Mathlani Madaktari,n.K, Sasa Unataka Nimpongeze Jk Kwa Hilo La Kulazimisha Michango Ya Waalimu Huku Mishahara Yao Ikiwa Midogo?
 
Walimu ni wafanyakazi waoga sana, wakipewa viposho kidogo tu hasa wakati wa uchaguzi wanaharibu mipango ya kuwaondoa viongozi wabovu.

Waalim sasa hivi wamebadilika sana na CCM tayari tumewastukia ,wanadai JK alisema haitaji kura za wafanyakazi kwa hiyo wana kisasi na CCM.
 
Hakuna nafasi ya ukoo wa panya kwa sasa,dr Slaa anatutosha sisi walimu wa nchi hii tuliopuuzwa kwa miaka 54
 
@MR Morris, unaweza kunitajia shule mbili(2) tu alizojenga Edward Lowassa?

Hulu kwetu shule za Kata tumejenga kwa kuchangishwa michango kila mtu mwenye kufanya kazi. Majina waliandika mabalozi wa CCM na kupeleka kwa Mtendaji wa Mtaa.
 
Last edited by a moderator:
Walimu ni wafanyakazi waoga sana, wakipewa viposho kidogo tu hasa wakati wa uchaguzi wanaharibu mipango ya kuwaondoa viongozi wabovu.
Hata chama cha walimu, CWT hakitoi msimamo!
Kimekuwa kimya sana.nchi zingine vyama vya wafanyakazi vimeleta mabadiliko!
 
Umetoa mada nzuri ya kujadili ulipomuingiza Lowassa tu umechemka mbaya,labda kama ulikuwa unaiwasilisha mada yako kwa walimu MBULULA UKO SAHIHI kwa sababu wapo ingawa idadi yao imepungua sana kwa sasa.

PIGIA KURA YA HAPANA KATIBA YA CCM INAYOPENDEKEZWA.
 
Back
Top Bottom