Uchaguzi 2020 Uchaguzi wa mwaka huu uwe fundisho la mwisho kwenu wapenda mabadiliko

Alwatan kamba

Member
Nov 16, 2020
70
236
Inasikitisha kwamba pamoja na chaguzi za mfumo wa vyama vingi zilizopita bado watu hamjalielewa somo badala yake mmekuwa mkirudia makosa yale yale kila baada ya miaka mitano.

inawezekana kweli somo ni gumu kuelewa lakini hata picha hamuoni?

unakuta mtu na akili zake timamu anaacha kufanya shughuli zake za kumuingizia kipato anaenda kupanga foleni kupiga kura ya kumchagua Rais.

hivi ni nani ana wadanganya kuwa hisani ya Rais hutokana na maamuzi ya karatasi "kura" zenu?

kila baada ya uchaguzi hasa wa vyama vya upinzani mmekuwa mkilalamika kuibiwa kura lakini ni nyie wenyewe mmekuwa vinara wa kuhamasishana kwenda kupiga kura kila kipindi cha uchaguzi. Matokeo yake mmebaki kuwa watu wa kulia lia na kulalamika kila siku mithiri ya vifaranga vilivyo achwa na mama yao lakini bado hamjifunzi...Inasikitisha sana.

ukweli ni kwamba, kura yako wewe haina nguvu wala maamuzi ya kuamua nani awe Rais labda kwa Wabunge.

Rais kama Rais ni taasisi na upatikanaji wake hutegemea na Rais aliyepo madarakani, marais wastaafu na vikao vya deep state. Kwa kifupi Rais hatokani na kura yako bali huandaliwa na watu wenye nguvu za ushawishi, maono na mamlaka.

Kwahiyo, Kuitisha uchaguzi ni kukamilisha tu taratibu za kidemokrasia kwamba tunafuata mfumo wa vyama vingi ili tusikose mikopo na misaada kutoka kwa nchi wahisani lakini kimsingi hauna nguvu yoyote katika kuamua nani awe Rais.

Nadhani mmeshuhudia kwenye uchaguzi uliopita na picha halisi ya demokrasia ya afrika mmeona jinsi ilivyo.

Uchaguzi huo uwe ni fundisho kwamba kipindi kingine cha uchaguzi usihangaike kupiga kura ya Rais, pigia ya mbunge kisha wahi kwenye mishe zako, habari za Rais achana nazo kabisa utapoteza muda wako bure.

Mwenye masikio asikie, asiye na masikio asome na aelewe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom