Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam

koryo

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
639
278
Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu,msemo anaoutumia mara nyingi kwenye hotuba zake Mhe Magufuli. Kimahesabu UKAWA wanawazidi wenzao wa CCM kwa wingi wa Madiwani.Mimi sioni sababu ya CCM kwenda Mahakamani kuzuia uchaguzi wakati wakijua kuwa UKAWA watashinda hata iweje. Mbona Mhe. Magufuli alimshinda Lowassa mbona UKAWA walikubali?. Tufike mahali tusilete fujo kwa mambo yasiyo na tija. Kwa vyovyote kama haki itatendeka UKAWA NDIYO MSHINDI. Sisi wananchi tunataka maendeleo na siyo fujo.
 
Wabunge Wa kuteuliwa na Wa muungano from znz pia wana haki...sheria za uchaguzi Tamisemi zipitiwe upya zina mapungufu ..anyway ukawa pia wana haki
 
Na mbaya zaidi kuendelea kutesa wabunge na madiwani wa Ukawa kwa kutumia polisi.... saa nyingine najiuliza huko makanisani na misikitini hawa viongozi wetu wanaenda kufanya nini...maana kule wanahubiri haki na wajibu na wao wakiwa viti vya mbele ila wakitoka kule haki sio issue kwao.... Muogopeni Mungu enyi kizazi cha NYOKA......
 
Serikali ya CCM inatakiwa kusoma alama za nyakati na kuacha kuishi ama kuenenda kimazoea.....wananchi wa Dar es salaam hawakuikataa CCM kwa bahati mbaya bali ni baada ya kuchoshwa na ukiritimba uliokuwa ukifanyika kwenye manispaa mbali mbali hapa Dar.....na kwa utashi wao wakaipigia kura ya hapana wakiwa na matumaini ya kuona manispaa ikiwa chini ya uongozi mpya na hatimaye kupata mabadiliko.......kitendo cha CCM kulazimisha kumpata meya kutoka kwao kinaonyesha ni jinsi gani kilivyo chama cha kishenzi kisichoheshimu matakwa na maoni ya wananchi ambao wamewakataa kwenye boksi la kura....na hii ikikomaa itaelekea kwenye udikteta na hatimaye machafuko.....

Haya mambo hayapaswi kutokea katika nchi inayojiita kuwa ni kisiwa cha amani...

Hali hii haipaswi kutokea chini ya raisi anayejinadi kutawala kwa misingi ya sheria na kanuni zilizowekwa.....hii inadhihirisha ni jinsi gani tulivyo na viongozi wanafiki wasiotenda yale wanayoyanena na wanaojali maslahi yao binafsi na vyama vyao na sio amani ya nchi...na hii ni sifa mbaya kwa kiongozi wa umma.......

CCM WAKUMBUKE KUWA MUSTAKABALI WA NCHI NI BORA KULIKO MASLAHI YA CHAMA CHAO....kwani iliumbwa ardhi na baadae chama....

HAKUNA MAREFU YASIYO NA MWISHO....
 
Utashangaa majitu yamajipanga kwenda kupata communion! Ushenzi mtupu! Hivi rais naye haoni unyama wanaofanyiwa RAIA wema? Hii nchi sijui nani katuloga aisee!!
 
waulizeni wenzenuvwa uganda.burundi.rwanda.mtajua kua ccm wakoje
 
Utashangaa majitu yamajipanga kwenda kupata communion! Ushenzi mtupu! Hivi rais naye haoni unyama wanaofanyiwa RAIA wema? Hii nchi sijui nani katuloga aisee!!

Aliyeturoga na kuwatoa wananchi wengi akili ni hiyo hiyo CCM . Wamehakikisha watu wanapata elimu ndogo sana na isiyoweza kumsaidia mwananchi kuamua hui ya yanayomkabili
 
Kwa hili la uhuni unaofanywa na viongozi wa CCM kwenye suala la uchaguzi wa Umeya jijini Dar na Rais Magufuli kutokemea uhuni huo unaofanywa na wanaccm wenzake, kunamfanya naye awe katika kundi la 'wanafiki' wa CCM, ikiwa ni kinyume kabisa na matamshi aliyoyatoa yeye mwenyewe kuwa anawachukia sana wanafiki!
 
Hmheshimiwa JPM ana taarifa juu ya haya yote yanayo endelea Kilombelo na Dar .kukaa kwake Kimya juu ya hili kuna ondoa Imani kubwa aliyo Anza kuienga Kwa wananchi wote bila kujari itikadi ya vyama vyao Kwa kifupi hii Ni aibu
 
Hivi, waziri mwenye dhamana yupo au katoka? Kama yupo ni kwanini hatoi tamko la kuzuia upuuzi huu unaohatarisha amani? Kama hayupo basi waziri mkuu aondoe figisu hii.
 
hivi hawa wanawexaje kusimama majukwaan wakjifanya eti tuwasaidie kuomba mungu watumbue majipu?!
ni mungu yupi wanamuabudu
yaani waanatuona wajinga au?!
 
Kwa hili la uhuni unaofanywa na viongozi wa CCM kwenye suala la uchaguzi wa Umeya jijini Dar na Rais Magufuli kutokemea uhuni huo unaofanywa na wanaccm wenzake, kunamfanya naye awe katika kundi la 'wanafiki' wa CCM, ikiwa ni kinyume kabisa na matamshi aliyoyatoa yeye mwenyewe kuwa anawachukia sana wanafiki!
Na yeye pia ashakua jipu sijui atamtumbua Nani?
 
Jamani huyo ni raisi wa ccm sio wa vyama vyote angalikuwa wa vyama vyote lazima angetoa tamko

fanyeni duniani kesho mbinguni kuna moto. ccm haitendi haki kabisa inaniuma sana

jipu hili la ccm sijui Nani ataliweza kulitumbua. haya bana lakini MUNGU yupo.
 
Back
Top Bottom