Tetesi: Uchaguzi wa marudio ni kupika matokeo ya Urais. CUF itarudishiwa majimbo yote ya uwakilishi

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,408
54,886
..huu ni mtego ambao CUF hawatakuwa na njia ya kuutegua.

..sasa hivi wanalalamika kuhusu matokeo ya majimbo ya uwakilishi ambayo walishapewa shahada za ushindi.

..ZEC-CCM watawarudishia majimbo yote waliyoshinda. Ila Uraisi atapewa Dr.Shein.

..kwa hiyo zile kesi ambazo wawakilishi walikuwa wanafikiria kufungua zitakuwa hazina maana tena kwani ZEC-CCM itawatangaza washindi.

..Hali hiyo itamtenga Maalim Seif na wawakilishi ambao watatangazwa washindi.

..CUF watakuwa hawana sababu ya kususia baraza la wawakilishi, na zaidi kuingia ktk serikali ya mseto.

..Jecha amelenga kwenye kutoa ushindi kwa wakilishi wa cuf. Wakati huohuo kumpa ushindi wa Raisi Dr.Shein.

..CCM wana MABAVU/MAJESHI na zaidi wana MAARIFA.
 
Hii mbinu ya kitoto ilishajulikana kitambo sana , na hasa baada ya mamluki jecha kukataa kuondoa majina ya wana cuf , lakini cuf ishaweka msimamo kwamba hawataenda kuapishwa hata kama maalim seif atatangazwa mshindi , lazima uelewe kwamba cuf haijishughulishi na uzushi huo 100% hata wakala wa cuf hatokuwepo kituo chochote .
 
Hitimisho la siasa za Zanzibar liko hapa;

Huu ni ukweli ambao ni mchungu kuukubali!

Hizi ndizo siasa za Zanzibar. Whatever you agree or not!

Kama hukubaliani nazo inabidi utumie unconventional method katika kufika Ikulu!
Huu sio ukweli bali ni ulevi wa madaraka. Lakini watu nao wanabadilika hivyo CCM isitarajie kutumia nguvu kuingia ikulu kila wakati? Nani alijua mtu kama rais mstaafu wa Zanzibar Karume atajageuka na ku-support ushindi wa CUF? Kumbuka kuna uchaguzi uliomweka yeye kwa nguvu huku ukiacha makumi wakiwa marehemu.
 
CCM wana mbinu 100 na mpaka sasa wametumia asilimia 20
CCM hawana mbinu 100 plus, ila CCM wanaendelea kukaa madarakani kwa kutumia vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi vinavyoendeshwa kwa kodi za wananchi, kuhakikisha kuwa CCM wanaendelea kukaa madarakani hata kwa zile mbinu 'haramu' hadi mwisho wa dunia!

Si mnakumbuka yale yaliyotokea pale kwenye kituo cha kujumlisha matokeo pale Bwawani Hotel ile siku ya tarehe 28/10/205 ambapo Makamu Mwenyekiti wa ZEC alikuwa 'arrested' na muda mfupi baada ya tukio hilo akaonekana Jecha kwenye ZBC akitangaza kuyafuta matokeo yote ya uchaguzi huo?

Hivi unaweza kuita hali hiyo kuwa ni mbinu za CCM za kutafuta ushindi au ni ubabe wa kupitiliza unaokiuka Katiba ya Zanzibar na sheria ya uchaguzi ya Zanzibar kwa kuvitumia vyombo vya dola kulazimisha ushindi?
 
Watauotoa na urais...wasipo fanya hivyo wakisafiri nje tu watakamatwa.....
Wasubiri vikwazo vya kusafiri
Wanaangaliwa tu na upuuzi wao
 
Back
Top Bottom