Wawakilishi 1,257 Nchi nzima: Baada ya Uchaguzi Oktoba 28, tutarajie nini uwakilishi wa Wabunge?

Asha D Abinallah

Senior Member
Apr 5, 2015
140
904
Habari Wana JF,

Nimesukumwa Kuweka mawazo Yangu na kukusanya muongozo wa kumbukumbu ili iwe rahisi kupima ushindi haswa kwa watakaochaguliwa kutuwakilisha Bungeni. Bunge limekuwa likilaumiwa kuwa na mapungufu mengi ambayo mara nyingi huonyesha ni sabbat ya uwingi wa Watawala kwa wakabi hue CCM ukifananisha na wapinzani.

Tumebakisha siku mbili tu kuelekea siku ya Uchaguzi Mkuu, utakaofanyika Oktoba 28. Uchaguzi wa Mwaka huu 2020 utakuwa wa aina yake haswa kwenye suala la Wagombea urais ambao kuna mchakato mkali sana unaendelea kati ya Mgombea wa CCM ndugu John Pombe Magufuli na Mgombea wa tiketi ya CHADEMA ndugu Tundu Antipas Lissu. Kwa namna moja ama nyingine uchaguzi wa Mwaka huu unaturudisha na kutukumbusha mchakato wa Uchaguzi wa Mwisho (2015) kati ya Mgombea wa CCM na wa Ticket ya CHADEMA ndugu Edward Lowassa. Licha ya madai ya Mgombea wa CHADEMA kudai alishinda uchaguzi huo kwa 62%, Kwa mujibu wa taarifa rasmi za Baraza la Uchaguzi la Taifa (National Electoral Commission of Tanzania); uchaguzi huo rais John Magufuli alishinda kwa kura 8,882,935 sawa na asilimia 60% ya kura zote huku Ndugu Edward Lowassa akiwakilisha Ukawa alipata kura 6,072,848 sawa na asilimia 40%.

Kampeni za Urais zimekuwa tofauti ya matarajio ya wengi na vile ambavyo ilifikiriwa itakuwa. Nje ya sababu nyingi ambazo zipo kwa kuwepo na matarajio tofauti, inajumuisha pia kitendo cha vyama pinzani (CHADEMA, ACT, CUF, CHAUMMA, NCCR, UDPD & CCK) kutoshiriki kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 24, 2019 hivyo kuipatia CCM ushindi wa 98%

Wabombea Urais kwa Mwaka 2020

Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mkuu 2020 tuna vyama 15 tu ambavyo vipo katika orodha ya walioteuliwa kugombea kiti cha Urais. Wagombea katika idadi ya Wagomba hal 15 tuna wanawake wawili, na patika nafasi ya wagombea wa Kiti cha Makamu wa rais kuna Wanawake 5 kati ya 15. Hivyo kufanya kuwa na jumble ya wanawake 7 katika orodha ya Wagombea wakuu 30. Orodha ya vyama vilivyo na wawakilishi wa kugombea kiti cha urais na kama ifuatavyo.
  1. Chama cha Mapinduzi (CCM)
  2. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
  3. Chama cha Civic United Front (CUF)
  4. Alliance for Change and Transparency - (ACT Wazalendo)
  5. NCCR Mageuzi
  6. National Reconstruction Alliance (NRA)
  7. Sauti Ya Umma (SAU)
  8. Demokrasia Makini (MAKINI)
  9. Alliance for Democratic Change (ADC)
  10. Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA)
  11. Alliance for Tanzanian Farmers Party (AFFP)
  12. Union for Multiparty Democracy (UMD)
  13. United People's Democratic Party (UPDP)
  14. Democratic Party (DP)
  15. African Democratic Alliance and the Tanzania Democratic Alliance ( ADA TADEA)

Umuhimu wa Kura nyingi za Urais katika Uchaguzi Mkuu

Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ndiyo unaongoza kwa idadi kubwa ya wagombea wa Upinzani toka tulipoanza mfumo wa vyama vingi. Idadi nyingi ya kura alizopata Mgombea wa UKAWA pamoja na kuwa alishindwa katika Uchaguzi huo, ilikuwa neema kwa upinzani kwenye suala la nafasi za ziada ya Ubunge. Izingatiwe kuwa idadi ya viti maalum hutegemeana na idadi ya kura za Urais. Kuungana kwa UKAWA ulinufaisha upinzani kwa kiasi kikubwa kwenye suala la kuongeza idadi ya Wawakilishi wa Vyama. CHADEMA ilipanda idadi ya wawakilishi bungeni kutoka 48 hadi 72 na CUF ilipanda kutoka 36 kufikia 41. Idadi ilikuwa kwa vyama vyote kasoro NCCR-Mageuzi ambao walikuwa na wabunge 4 mwaka 2010 na kushuka hadi Mbunge mmoja.

Kwa mujibu wa taarifa za Bunge nafasi ya Wabunge kikatiba ni 393. Hata hivyo mwaka 2015 bunge lilikuwa na wabunge 374. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilishinda viti 195, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) walishinda viti 35, Chama cha Civic United Front (CUF) kilishinda viti 31, Chama cha ACT Wazalendo kiti 1 na NCCR Mageuzi 1. Kwenye ubunge wa Viti maalum CCM ilikuwa na nafasi 66, Chadema nafasi 37 na CUF nafasi 10.

Awamu hii ya bunge (2015 - 2020) ilikuwa na wawakilishi 388. Uwiano wa viti vilivyo chini ya Serikali tawala CCM ni 273 na Upinzani (CHADEMA, CUF, ACT & NCCR) 115 ikiwa sawa na uwiano wa asilimia 70.36% dhidi ya 29.64% . Hata hivyo itambulike kuwa tokana na idadi Kikatiba kuwa 393, kulikuwa na nafasi za wabunge 5 zilikuwa wazi moja ikiwa ni ya jimbo moja (Longido) kuwa na chagamoto. Ilikuja kujazwa baadae kwenye uchaguzi mdogo na ndugu Lekule Laizer baada kumshinda Dk Stephen Kiruswa baada ya Mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2015. Kesi hiyo ilikuwa kati ya Mgombea wa CCM Dk Stephen Kiruswa na Onesmo Nangole (CHADEMA).

Idadi za Wabunge kwa Chama 2015 - 2020

MPs list.png
*Idadi ya viti maalum hupatikana tokana na idadi ya kura za mgombea rais Uchaguzi Mkuu


Tutarajie nini katika wawakilishi wa Ubunge kwa Mwaka 2020?

Tanzania tuna majimbo 264, bara tukiwa na majimbo 214 huku visiwani kukiwa na majimbo 50. Mwaka huu vyama vilivyoweza kushiriki kwa kusimamisha wawakilishi waliopitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mkuu 2020 ni 1,257 idadi hiyo ikijumuisha wawakilishi wa vyama 19. Katika idadi yote ya wagombea 963 (77%) ni wanaume na wanawake wakiwa 294 (23%). Izingatiwe kuwa endapo kila chama kingekuwa na uwezo wa kusimamisha kila jimbo kwa vyama vyote 19, yapaswa tungekuwa na wagombea 5,015. Hivyo idadi ya waliojitokeza bado ni ndogo kuweza kupata uwakilishi mzuri zaidi Ki demokrasia. Kwa muktadha huo ina maana tuna asilimia uwakilishi wa 25% wa idadi stahili ambayo ilipaswa tuwe nayo ya wagombea ubunge kwa Tanzania bara na visiwani.

A. Ubunge CCM (Ya kwanza kwa uwingi) 2020
CCM ndiyo chama pekee ambacho kimeweza kuwa na wawakilishi katika kila jimbo hivyo kuifanya hadi sasa tayari kujishindia viti 28 bila kupingwa. CCM kina wagombema 264 kikiwa na wagombema wanaume 239 na wanawake 25 tu (9%). Mtwara ikiwa imeongoza kuliko majimbo yote kuwa na Wanawake wengi zaidi wagombea wa CCM kwa idadi ya 3. Katika utaratibu wa CCM wa wagombea kupigiwa kura na wajumbe wa chama ili kupata mwakilishi wa jimbo; kati ya majimbo yote 264, Chama kilitengea na kupitisha majina ya wagombea mbadala katika majimbo 20 yote yakiwa bara.​

B. Ubunge CHADEMA (ya pili kwa uwingi) 2020
CHADEMA kina wagombea 211 na ndiyo chama cha pili kuwa na wawakilishi wengi wa wagombea nchi nzima baada ya CCM. Wagombea wanaume 151 na wanawake 60 (29%). Arusha ndiyo inaongoza kuwa na wanawake wengi kwa idadi ya 5. Kwa mujibu wa CHADEMA katika majimbo hayo 264, ilikuwa tayari na nguvu ya kuwa na uwakilishi wa Wagombea wa Ubunge kwa bara na visiwani 235. Katika orodha hiyo majimbo yapatayo 50 wamekosa wawakilishi kutokana na sababu mbali mbali, huku upande wa bara majina yapatayo 36 yamewekewa ama pingamizi au kutopitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mkuu 2020.​

C. Ubunge ACT Wazalendo (ya tatu kwa uwingi)
ACT Wazalendo kina wagombea 156 wa Ubunge Tanzania bara na visiwani na ndiyo chama cha tatu kwa uwingi wa wawakilishi baada ya CCM na CHADEMA.. Kati ya idadi hiyo wanaume ni 135 huku wanawake wakiwa 21 (13%). Tanga ndiyo inaongoza kuwa na wanawake wengi kwa idadi ya 4 (4 kati ya wagombea wote 6). Kwa mujibu wa ACT chama kilikuwa na nguvu ya kura na wawakilishi 196 kwa bara na visiwani. Washiriki 40 wamekosa wawakilishi kutokana na sababu mbali mbali, huku upande wa bara majina yapatayo 22 yamewekewa ama pingamizi au kutopitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mkuu 2020.​

D. Ubunge CUF (ya nne kwa uwingi)
CUF kina wagombea wa bungee 154 Tanzania bara na visiwani na ndiyo chama cha nne kwa uwingi wa wawakilishi baada ya CCM, CHADEMA na ACT. Kati ya idadi hiyo wanaume ni 117 na wanawake ni 37 (13%). Dar es Salaam, na Mjini Magharibi ndiyo zinaongoza kuwa na wanawake wengi zaidi zote zikiwa na wanawake wawakilishi 5 kwa 5. Kwa mujibu wa CUF chama kilikuwa na nguvu ya kusimamisha wagombe​

E. Ubunge NCCR Mageuzi (ya tano kwa uwingi
NCCR kina wagombea 85 Tanzania bara na visiwani na ndiyo chama cha tano kwa uwingi wa wawakilishi baada ya CCM, CHADEMA, ACT na CUF. Kati ya idadi hiyo wawakilishi wanaume ni 66 na wanawake wakiwa 19 (22%). Mjini Magharibi ndiyo inaongoza kwa kuwa na wanawake wengi kwa idadi ya 3 kwa majimbo yote. Jimbo hilo lina jumla ya wagombea 5.​
Number of Candidate.png
Ubunge vyama vilivyobakia
Vyama vingine 14 vilivyobakia vina jumla ya wagombea 387 ikijumuisha wanaume 255 na wanawake 132. Namba hii ya uwakilishi wa vyama unaonyesha vyama vidogo vimetoa nafasi kubwa na kujenga mazingira hamasishi ya Wanawake kujitolea kugombea nafasi ya Ubunge kwa nafasi ya asilimia 65% kwa 35%. Na hali kwa Vyama tano bora vina wagombea jumela 870 ikijumuisha wanaume 708 na wanawake 162 ikiwa ni 82% kwa 18%.​
Idadi hiyo ya 387 inajumuisha wagombea 48 (ADC), wagombea 44 (MAKINI), wagombea 37 (TADEA), wagombea 34 (NRA), wagombea 33 (UDP), wagombea 28 (CHAUMMA), wagombea 28 (AAFP), wagombea 27 (TLP), wagombea 23 (DP), wagombea 22 (UPDP), wagombea 19 (SAU), wagombea 18 (CCK), wagombea 17 (UMD) na wagombea 9 (NLD).​


Baadhi ya Yatokanayo na Uchaguzi Mkuu 2020

Ubunge wa Viti maalum kama Mtaji

Pamoja na CCM kuwa na wawakilishi wachache sana wanawake, baada ya uchaguzi kuna idadi kubwa ya uhakika wa viti maalum, ingawa ni vigumu kujua idadi hadi uchaguzi mkuu kuisha. Hili linaibua ulazima wa kujadili hoja ya Viti Maalum bungeni kuandaliwa vigezo vipya. Tokana na namna ya Upatikanaji wa Viti hivi inaonyesha wazi kwamba sasa kuna umuhimu wa Kutathmini Viti Maalum tokana na Idadi kubwa ya nafasi hizo ambazo zina tija ya Maslahi kwa jamii. Mabadiliko hayo yanapaswa kutoangalia tu jinsia ya Mwanamke, ila kuna haja ya kuongeza vigezo hivyo kusukwa kwa mtindo kuwa hata Wanaume, makundi maalum na vijana wanaweza teuliwa katika nafasi hizo kwa vigezo ambazo vitahakikisha vinajenga misingi ya Uwajibikaji na zaidi kwa kuhakikisha watu hawarudi tena miaka mingine mitano kwa kuteuliwa.

Wabunge wapya kama Mtaji kwa ACT

Ni wazi kuwa mwaka huu, ACT Wazalendo wana nafasi kubwa ya kukua kutoka kuwa na Mbunge mmoja mwaka 2015 na kuongeza idadi ya Wabunge. Ndani ya miaka mitano kutoka uchaguzi wa mwaka 2015 hadi kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu 2020, nje ya jitihaza za kujenga chama, ACT imecheza karata nyingi za kuwajenga na kuwanyanya zaidi. Kubwa kuliko zote ilikuwa kumpata Maalim Seif Sharif Hamad akiwa na kile wanachoita mtaji wa Siasa “Political Power) akiwa na wafuasi walioongeza nguvu ACT. Maalim Seif alihamia ACT Machi 18, 2019. Karata ya sasa hivi wa Viongozi wa chama kumuunga mkono Mheshimiwa Tundu Lissu mgombea wa Tiketi ya CHADEMA itachagiza idadi ya kura za wabunge katika majimbo mbali mbali.

Kulikuwepo na hoja nyingi kipindi Maalim Seif anahamia ACT likiwepo kundi baadhi la wafuasi wake kuona kama ameua Ndoto Yao kwa kuitufaisha ACT na kudhoofisha nafasi yake ya kushinda Urais Zanzibar wakiamini ilipaswa ahamie CHADEMA. Kwa matukio yanayoendelea sasa katika Kampeni naamini wafuasi hao sasa wana matumaini mafya.

Wawakilishi Ubunge CUF

Uchaguzi huu wa mwaka 2020 unatoa hamu ya kutaka kufahamu uwepo au kutokuwepo kwa pengo kwa kundoka kwa Maalim Seif mapema mwaka jana. Kulikuwepo na mpasuko ndani ya CUF kwa muda mrefu na hivyo kupelekea kugawanyika kwa chama na kuwa na makundi mawili ya CUF ya Profesa Ibrahim Lipumba na CUF ya Maalim Seif Sharif Hamadi, hadi maalim alipoamua kuondoka. Hata hivyo kikiwa chama ya nne kwa uwingi wa wagombea huku ACT ikiwa imewashinda kwa kuwa ya tatu, CUF wamejitahidi kuwa na idadi kubwa kiasi kwa kuwa na wagombea 154. CUF ina wawakilishi katika majimbo 44 visiwani hivyo kuwafanya tayari kuwa wamepoteza majimbo 6.


Kuna mengi tumeeona, tunaendelea kuona na yale ambayo tunatarajia kuona. Shauku ni kubwa na more than ever tuna hoja mbali mbali ambas kwa kiasi kikubwa zinawezeshwa na uwepo wa Mitandao ya Kijamii na kutupa nafasi watumiaji ya kuchagua ni namna ipi utashiriki patika hoja mbali mbali iwe kwa kushiriki au kutoshiriki moja kwa moja.

Mwenyezi Mungu atusimamie zoezi liende vizuri tuone Historia ikijengwa, kwani Mwaka huu kati ya wagombea wote wawili wakubwa wakishinda. Itakuwa ni Historia ya aina yake.

Mungu Ibariki Tanzania.

Nawasilisha,

Asha D. Abinallah
 
Ikumbukwe kuwa katika uchaguzi wa mwaka 2015, kura za madiwani pamoja na kura za Wabunge na Rais baada ya kujumlishwa na kuandikwa katika fomu za matokeo, wasimamizi walizipeleka katani ili ziunganishwe na kupata matokeo ya jumla kwa kata husika. Baada ya hapo, nakala halisi za matokeo hayo zilipelekwa jimboni ili kuunganishwa na kupata jumla kwa jimbo huku nakala zingine wakipewa mawakala.

Ikumbukwe hapa ilikuwa ni rahisi kudhibiti ikiwa kutatokea nyongeza ya VITUO HEWA vya kupigia kura.

LAKINI MWAKA 2020;

Baada ya kura kuhesabiwa na kupata matokeo ya kituo husika,ni matokeo ya MADIWANI tu yatakayounganishwa katani lakini matokeo ya WABUNGE NA RAISI kwa kila kituo, HAYATAUNGANISHWA KATANI badala yake yatapelekwa jimboni kuunganishwa.

IMG_20201026_193517.jpg


TATIZO LINAWEZA KUTOKEA:

Tatizo hili linaweza kuwa kuongeza vituo hewa endapo mawakala hawatakuwa na orodha ya vituo vyote vya jimbo na ikiwa hawatakuwa makini wakati wa kujumlisha kura.

VYAMA VYOTE VYA SIASA, CHUKUA TAHADHARI.
 
Back
Top Bottom