Uchaguzi wa Marekani sio wa Kidemokrasia

fullcup

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
806
2,182
Habari wanabodi,

Ifike wakati tusipelekeshwe kama mbweha, wao kila siku Tanzania hivi mara Tanzania vile ilimradi taflani. Mimi nasema uchaguzi wa Marekani sio wa kidemokrasia kabisaaa. Yaani eti kesho 3rd Nov 2020 wanapiga kura wavuja jasho woote na siku nyingine wanapiga mabwanyenye sijui maseneta.

Sasa upuuzi wao upo hapo kwenye hizo kura mbili, yaani unaweza kushinda kwa majority kama Clinton halafu kwa maseneta ukifeli ndo umefeli Urais! Sisi kama Tanzania nchi ya kidemokrasia na nchi kuu katika ukanda huu tupinge dhuruma hii inayofanywa na hawa mabeberu.
 
Wamarekani wameanza kupiga kura muda kidogo, na kama sikosei tangu wiki mbili zilizopita. Kuna utaratibu wa kupiga kura ambao unatumiwa karatasi ya kupigia kura kwa barua (posta), unajaza na kuipeleka wewe binafsi sio kwa njia ya posta, kwenye kituo cha kupitia kura kilicho karibu nawe, na mpaka sasa wapiga kura wapatao milioni 80 wameshaitumia njia hiyo. Ila hiyo tarehe Novemba 3, ndio siku ya mwisho kwa wote ambao hawakupiga kura.

Kwenye matokeo sasa ndio kuna hiyo tofauti unayoiongelea. Kuna matokeo ya kura ya wote (popular votes), hiyo ni raia wote walipiga kura jumla yake huwa ni mamia ya milioni, halafu kuna baadhi ya watu, nao wanapiga kura kama wengineo, sio kama ulivyosema wana siku yao, na pia sio maseneta, ila niwaite wateuliwa na kwa ujumla wao wanaitwa (electoral college), ndio mshindi bila ya kujali wingi wa kura za wengi, atatangazwa kutegemea na wingi hizi kura za electoral college.
Nimenakili maelezo kwa urahisi yanayoeleza maana ya hiyo electoral college.

In the Electoral College system, each state gets a certain number of electors based on its total number of representatives in Congress. Each elector casts one electoral vote following the general election; there are a total of 538 electoral votes. The candidate that gets more than half (270) wins the election.

Ni kweli taswira inayopatikana ni kuwa, kuna uwezekano wa wengi kutopewa au kutopata chaguo la mtu waliyempenda, ni mpaka pale tu wingi wa kura za wengi utakapoendana na wingi wa kura za hili kundi kumuelekea mgombea mmoja, ndio hapo itaonekana kuna demokrasia tunayojua na kutegemea, ila kura zikiwaelekea wagombea tofauti, atakayeshinda ni aliyepata kura nyingi za hili kundi dogo la uwakilishi.

Kinachotokea Marekani, kwa mtazamo wangu ni kama kinachotokea Tanzania. Wenzetu wanafanya bila ya kificho licha ya malalamiko na maandamano, mfano baada ya kuchaguliwa Trump, ila kwa Tanzania tunachoshuhudia, haijalishi mgombea wa chama gani anapendwa, atakayeshinda ni wa ccm, hiyo ni kwa urais, na kwa ubunge, kwa mtazamo wangu na hasa kwa uchaguzi huu uliopita, anayeshinda awe wa ccm au wa upinzani, ccm ndio walioamua na sio wapiga kura.
 
Hapa kwetu maneno mengiii hakuna lolote wangekamata kura fake wangeitisha mpaka BBC kuonesha hizo kura lakini walichoma box wakadai ni kura.
Daah ndiyo akili za mbogamboga, wenzao wanakomaa wasitoke madarakani ili watetee ulaji, wewe unakufa njaa tuu
 
Wamarekani wameanza kupiga kura muda kidogo, na kama sikosei tangu wiki mbili zilizopita. Kuna utaratibu wa kupiga kura ambao unatumiwa karatasi ya kupigia kura kwa barua (posta), unajaza na kuipeleka wewe binafsi sio kwa njia ya posta, kwenye kituo cha kupitia kura kilicho karibu nawe, na mpaka sasa wapiga kura wapatao milioni 80 wameshaitumia njia hiyo. Ila hiyo tarehe Novemba 3, ndio siku ya mwisho kwa wote ambao hawakupiga kura.

Kwenye matokeo sasa ndio kuna hiyo tofauti unayoiongelea. Kuna matokeo ya kura ya wote (popular votes), hiyo ni raia wote walipiga kura jumla yake huwa ni mamia ya milioni, halafu kuna baadhi ya watu, nao wanapiga kura kama wengineo, sio kama ulivyosema wana siku yao, na pia sio maseneta, ila niwaite wateuliwa na kwa ujumla wao wanaitwa (electoral college), ndio mshindi bila ya kujali wingi wa kura za wengi, atatangazwa kutegemea na wingi hizi kura za electoral college.
Nimenakili maelezo kwa urahisi yanayoeleza maana ya hiyo electoral college.

In the Electoral College system, each state gets a certain number of electors based on its total number of representatives in Congress. Each elector casts one electoral vote following the general election; there are a total of 538 electoral votes. The candidate that gets more than half (270) wins the election.

Ni kweli taswira inayopatikana ni kuwa, kuna uwezekano wa wengi kutopewa au kutopata chaguo la mtu waliyempenda, ni mpaka pale tu wingi wa kura za wengi utakapoendana na wingi wa kura za hili kundi kumuelekea mgombea mmoja, ndio hapo itaonekana kuna demokrasia tunayojua na kutegemea, ila kura zikiwaelekea wagombea tofauti, atakayeshinda ni aliyepata kura nyingi za hili kundi dogo la uwakilishi.

Kinachotokea Marekani, kwa mtazamo wangu ni kama kinachotokea Tanzania. Wenzetu wanafanya bila ya kificho licha ya malalamiko na maandamano, mfano baada ya kuchaguliwa Trump, ila kwa Tanzania tunachoshuhudia, haijalishi mgombea wa chama gani anapendwa, atakayeshinda ni wa ccm, hiyo ni kwa urais, na kwa ubunge, kwa mtazamo wangu na hasa kwa uchaguzi huu uliopita, anayeshinda awe wa ccm au wa upinzani, ccm ndio walioamua na sio wapiga kura.
20201104065642_526288105_5563928455355822206_320_320_75_webp.jpg
 
Back
Top Bottom