Uchaguzi wa Magogoni Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi wa Magogoni Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kibunango, May 22, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Naona macho na masikio ya JF yapo huko Busanda tu, kwa taarifa kesho katika Jimbo la Magogoni kuna uchaguzi wa Mbunge vile vile..

  Kampeni za Jimbo la Magogoni Z'bar kuhitimishwa Ijumaa

  FAINALI ya kampeni za kunadi wagombea wa nafasi ya uwakilishi wa jimbo la Magogoni kisiwani Unguja itakuwa leo wakati vyama pinzani vya CUF na CCM vitakapofanya mikutano yao ya hadhara kwenye viwanja tofauti kurusha karata zao za mwisho kabla ya upigaji kura utakaofanyika kesho.

  CCM, ambao wanatetea kiti hicho, watahitimisha kampeni zao kwa kufanya mkutano kwenye viwanja vya Daraja Bovu, ambako mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama hicho, Dk Ali Mohamed Shein atakuwa mgeni rasmi, wakati CUF itakuwa kwenye viwanja vya Kwa Mabata, ambako makamu mwenyekiti wa chama hicho, Machano Hamisi Machano atakuwa mgeni rasmi.

  SAU, chama kingine kilichosimamisha mgombea kwenye uchaguzi huo, kitahitimisha kampeni zake kwenye uwanja wa Diwani.

  Asha Mohamed Hilal atakuwa akijaribu kukirejesha kiti hicho CCM baada ya mwakilishi wa jimbo hilo, Daud Hassan Daud kufariki dunia mwaka jana, wakati CUF imemsimamisha Hamad Ali Hamad na SAU imemsimamisha Khamis Msele Omar.

  Kampeni hizo za uchaguzi zilizoanza tangu Mei 9 zimekuwa zikitawaliwa na malalamiko na vijembe na jana Umoja wa Vijana wa CCM (UV-CCM) ulitangaza kuwa vijana watakaowapigia kura wapinzani watakuwa wanasaliti mapinduzi ya mwaka 1964 na uhuru wa Tanganyika wa mwaka 1961.

  Naibu katibu mkuu wa UVCCM-Zanzibar, Mohamed Hassan Moyo alitoa kauli hiyo jana wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni za kumnadi mgombea wake, Asha Mohamed Hilal.

  Moyo alisema kuwa mapinduzi ya 1964 na juhudi za kuleta uhuru wa 1961 mikakati yake ziliandaliwa na kutekelezwa na kundi la vijana, hivyo ni lazima heshima ya vijana wa ASP na TANU zilindwe na kuthaminiwa na wote.

  Alisema itakuwa ni aibu na usaliti dhidi ya juhudi za wanamapinduzi na wapigania uhuru ikiwa kada ya vijana nchini walioelimishwa na kujengeka katika afya bora chini ya Serikali za Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakivipigia kura vyama vya upinzani.

  “Vijana wa TANU na ASP hawakuwa na hofu, woga wala usaliti hivyo vijana walio chini ya UV-CCM nao pia wanapita katika nyayo hizo kwa vitendo na ujasiri,” alisema Moyo ambaye ni mtoto wa mwanamapinduzi, Hassan Nassor Moyo.

  Naibu katibu mkuu huyo alisema vyama vya upinzani havistahili kupewa ridhaa ya kuongoza kwa sababu ni vyama vya kihuni vinavyohubiri shari na uvunjaji wa amani badala kujijenga kisiasa hadi vijijini.

  Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi limewatahadharisha wapiga kura kuhakikisha amani na utulivu wakati watakapokuwa wakipiga kura kesho kumchagua mwakilishi wa jimbo la Magogoni.

  Kamanda wa mkoa wa Mjini Magharib, Bakari Khatib Shaaban alitoa tahadhari hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Zanzibar.

  Nayo Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imewataka wananchi wa jimbo hilo waliothibitishwa kuwa ni wapiga kura halali kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi huo.

  Taarifa ya tume hiyo ambayo ilisambazwa kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa, tume itahakikisha kila aliyekuwa na haki anapewa nafasi ya kupiga kura katika uchaguzi huo. Taarifa hiyo inaeleza kuwa vituo vitafunguliwa kuanzia saa 12:00 asubuhi na vitafungwa saa 12:00 jioni.

  Source: Mwananchi
   
  Last edited by a moderator: May 23, 2009
 2. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu umeweka jina la CHADEMA kuuza thread nini? mbona sioni kokte iliko ongelewa chadema na uhoi wake? Nijuvye mkuu sijakupata kabisa!
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  May 22, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Chadema wamemsimamisha mgombea gani huko?
   
 4. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2009
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mkuu hiyo signature yako ingekuwa inatumika kwenye kampeni za huko Magogoni nadhani chama chako (ambacho hakiko hoi) kingekuwa hoi !!
   
 5. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2009
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mzee Spinning Doctors ni wanamazingaombwe!!
   
 6. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Chadema hawana ubavu huko visiwani, Umaarufu wa Chadema visiwani ulikuwa mkubwa miaka ya tisini, hata hivyo wameshindwa kuuendeleza kiasi cha kushindwa kuweka mgombea katika Jimbo la Magogoni ambalo kwa namna moja ama nyingine lina ufahamu mkubwa katika kutathimini sera za vyama na sio mapenzi ya watu na itikadi zao kwa vyama, hali ambayo ipo kwenye majimbo mengi visiwani humo.

  Hii inamaanisha kuwa Chadema pamoja na kuvuma sana huko Bara, ipo hoi bin taabani huko visiwani, tofauti na vyama kama CCM na CUF ambavyo vinatamba Tanzania nzima.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  May 22, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  chama kinaweza vipi kuwa hoi mahali ambapo hakishindani? CUF ndiyo inaweza kuwa hoi au CCM huko visiwani! ama?
   
 8. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kwikwi.. CUF mnao wabunge wangapi bara wa kuchaguliwa vile...nnnnhh?
   
 9. Mchizi

  Mchizi JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2009
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 680
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 180
  Chadema haina haja ya kuwa na nguvu sehemu ambayo wakazi wake wote hata hawafikii nusu ya wakazi wa Mwanza.Chadema ikijiimarisha bara inatosha sana
   
 10. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #10
  May 22, 2009
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  wamemsimamisha GT!
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  May 22, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hapa nimecheka
   
 12. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #12
  May 22, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,841
  Likes Received: 1,102
  Trophy Points: 280
  Hii heading mbona haihusiani na maudhui thread? au???
   
 13. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #13
  May 22, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Nadhani huu ushabiki haufai, Chadema wanakuwaje hoi hapo? Hizi ni chuki ambazo hazina msingi.
   
 14. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #14
  May 22, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kibs, punguza tende
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  May 22, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Duh!... GT mbunge wa Chadema Magogoni?..ama kweli mnamtafuta kwa mengi.
   
 16. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #16
  May 22, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Swali kaulizwa GT wewe unajibu!!! Ndio maana michango yako inafananafananana, ama kweli kazi kwelikweli.
   
 17. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #17
  May 23, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmmhh siku hizi comparison ya maende unaweza kuifanya kwa mchele ( irrelevant comparison) sijui kama utapata unachokusudia; anauza jina la chadema tu huyo hana lolote
   
 18. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #18
  May 23, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Bahati mbaya jina la Chadema haliuziki huko Zenj...!
   
 19. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #19
  May 23, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  siyo issue kubwa sana, kuna wapiga kura milionin ngapi huko?
   
 20. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #20
  May 23, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Tatizo sio idadi ya wapiga kura, tatizo ni sura ambayo Chadema wanayoijenga kwa taifa hili la Muungano.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...