Mtanganyika
JF-Expert Member
- Jul 18, 2007
- 1,601
- 964
MOD: Nawaombeni hii muiche yenyewe kwa siku chache ijadiliwe na baadaye muinganishe pamoja na thread zingine ambazo zimeshajadili uchaguzi wa Kiteto.
Watu kadhaa mmeuliza maoni yangu kuhusu uchaguzi wa Kiteto, kabla sijaanza kujadili mtizamo wangu- someni kwanza hapa msimamo wa kina wa CHADEMA kuhusu yaliyojiri katika Uchaguzi wa Kiteto: http://www.chadema.net/tamko/2008/kiteto.php
Kwa wale mnaofahamu 'the science and art of rigging elections' mtajua kwamba uwizi katika uchaguzi haufanywi kwa njia moja, ni mkusanyiko wa njia mbalimbali ambapo kila moja inatumika kuathiri matokeo kwa maana ya kuongeza au kupunguza idadi fulani ya kura. Jumla ya mbinu zote ndizo huzaa matokeo fulani ambayo yanakuwa yamepangwa.
Nawaomba tusome kwa makini ukurasa hata ukurasa katika tamko hili la kurasa tano. Nitarejea kutoa maoni yangu
JJ
Tamko hili tulikujibu siku za nyuma.unganisha na ile thread.
kama kweli katika TAMKO RASMI aka OFFICIAL RESPONSE ya chadema inasema kwamba ccm ilitumia bilioni moja katika uchaguzi mdogo wa kiteto, nipo radhi kufuatilia hayo madai hadi nijue ukweli, na kama la basi jua nitakuandama kwa uongo wako (wenu) huo hadi ukiri kwamba umeongopa !
mambo ya dirty politics hapa hakuna, au lete transcripts (wewe mnyika) zinazoonyesha madai yako, JE NA NYINYI CHADEMA mlitumia kiasi gani ?
Mr. John Mnyika
Ahsante sana kwa taarifa lakini naomba kuuuliza haya
a) Hivi ni kweli asilimia 77 ya wananchi wa kiteto hawajui kusoma na kuandika?....idadi hii mbona inaonekana kuwa kubwa sana.
b) Kama mnalalamika kwamba mambo mengi yamepindishwa mbona nasikia mlikubali kushindwa?
c) Kama tuhuma zinazoelezwa umo ni za kweli (baiskeli, kugawa cement, wakuu wa mikoa 2 kutembelea Kiteto kufanya kampeni na mwingine kutembelea miradi ya mandeleo...) sasa kwa nini msipeleke kesi mahakamani kudai uchaguzi ubatilishwe?
d) Hivi madai ya kwamba CCM imetumia takribani bilioni 1 ni ya kweli na kuna jinsi ya kuweza kuthibitisha? Kama hii ni kweli basi inabidi JF na wengine wote wanaoitakia nchi yetu mema kufanya uchunguzi wa kina na hasa kwenye chaguzi zijazo maana hii imenitisha sana kwa kweli.
e) Na mwisho Mr. Mnyika na wenzako wa CHADEMA mna mikakti ipi ya 2010 na kuendelea? Maana mambo ya kukurupuka wakati wa uchaguzi hayana maana yoyote...je unaweza kutupatia mpango mkakati wenu wa miaka 3, 5 hadi 10 ijayo? au mnavamia mambo tu...mkishapigwa chini na CCM mnaanza kutafuta visingizio kibao? Tafadhali tuelezeni tujue....
Kazi njema na naomba ujumbe wangu mfikishie mwenyekiti, Katibu Mkuu na wakurugenzi pamoja na wanachama wenu wote....
Mkiwa na mikakati kamili na njia mbadala ya kupambana na CCM mtaweza kushinda....
Mungu Ibariki Tanzania......
Sasa tukasome nini na wewe ushatuambia "mmeibiwa" kwa njia mbalimbali.
Since when u conceaded defeat? u will always have excuses to justify u failure...
John Mnyika.
Good point, lakini nataka kwanza kabisa you need to declare that CHADEMA lost in Kiteto. I understand their were problems in campaign and election day, however CHADEMA had weakness in running campaign.
Vile vile, nilizungumza kwenye mjadala mmoja ya Rev. Kishoka kwamba tatizo sio wananchi, tatizo ni policy za CHADEMA zisizojulikana na wananchi. Ni imani yangu kwamba 2010 haiko mbali sana, kama kweli CHADEMA wanataka kuongeza viti bungeni then this few things need to be do
CHADEMA needs to create realistic strategy. Yaani lazima chadema wa set number ya wabunge wanayotaka kufikia bungeni, then inabidi waangalie miji gani CCM wana weakness, then waananchi wapewe option ya kuchagua strong candidates within CHADEMA ambae atashindana na CCM in 2010
CHADEMA needs to change the whole organization leadership chart.
Sasa hayo ni machache, maana kuna mengi yanayotakiwa kufanyika ili chadema iwape wananchi imani kwamba CHADEMA wako tayari.
Mpango Mkakati wa Pili kwa 2006 -2010
Kutambua, kulea na kuandaa viongozi wa baadaye wa serikali na chama kwa kuwajengea uwezo wa kiuongozi na kitaaluma.
Katika kipindi cha miaka mitano mafunzo yatapewa kipaumbele katika maeneo mbalimbali.
Kutambua,kujenga mawasiliano na kuwaandaa wagombea watarajiwa mapema na Kuhakikisha chama kinashinda katika chaguzi ndogo zitakazojitokeza hususani katika ngazi ya ubunge.
Kuhamasisha vijana kujiunga na CHADEMA, wengine kugombea uongozi na mkazo utawekwa katika kuwapa vijana mbinu na mafunzo ya kisiasa hususani katika ngazi za chini.
Mkazo uwekwe kuhakikisha wanawake wengi wanajiunga na CHADEMA na kuandaliwa kupenya katika uongozi na kuwa mhimili muhimu wa chama wakati wa chaguzi mbalimbali.
KadaMpinzani good to see you back.
John, moja ya weakness za upinzani ni kulalama kwamba wanaonewa na kukataa kushindwa. I know CCM ni wezi, i know that from experience of other elections. Lakini swala sio CCM tuu, i want you to tell us what is the problem with in CHADEMA?
I know wamerun campaign ya billion of shilling, but the point is does your candidate likeble enough in that region? Ni procidure gani mlitumia kumpata mgombea? What is his credentials in that region?
If you wanna beat CCM then you have to fight as a winner and not a looser. How Zitto won Kigoma sit? How about Ndesamburo? I heard you runed an amazing campaign back in 2005. Why you, Ndesamburo, Slaa and Zitto survived CCM pressure? Sababu you guys has credentials needed to have a sit bungeni.
John, inabidi kwanza muwaambie wale wazee kwamba CHADEMA needs to change its strategy. Mnaitaji kina dada zaidi kama Hon. M.Rhuwanya, kinana kaka wengi zaidi mfano wako na Zitto, then mnaset long time goals.
Soma:
CHADEMA tumesema wazi tumetumia bei gani, na tumesema pia kwa nini tunasema CCM imetumia kiasi hicho na tumewataka nao waweke wazi matumizi yao kwenye kampeni. Na hii ni mara ya pili, tuliweka wazi Mei 2006 matumizi yetu ya kampeni 2005; tukawataka CCM nao waweke wazi. Mpaka leo hawajafanya hivyo, wanaficha kwa nini?
JJ
Mtanganyika
Nakubaliana na wewe jambo moja- mpinzani wako akiweza kutoa rushwa, kukutisha, kukuhujumu na hata kukuibia katika uchaguzi basi wewe una weakness fulani. Tarime, Pemba nk- hizo weakness zinaelekea kutokuwepo? Jibu ni kwamba, katika maeneo hayo, wananchi wameamua kuasi- hivyo, wameacha kufanya siasa za kistaraabu, ndio maana wanaweza kupambana na hujuma za aina hii. Lakini siasa za uasi, in a long run sio nzuri kwa utangamano wa taifa. CCM itatupeleka mahali ambapo tutalazimika kuchochea wananchi kuasi kila mahali tunapokwenda kufanya kampeni za uchaguzi. Tukifika huko, amani yetu itakuwa mashakani. Unafanyaje katika uchaguzi ambao makomandoo wa CCM wanashirikiana na polisi kuwapiga viongozi waandamizi wa kampeni? Unamwagaje sera katika mahali ambapo Komba baada ya kukosa watu katika mikutano yao anavamia mkutano wa CHADEMA kumwaga sera zake na bado polisi wanamuangalia? Unafanyaje katika siasa ambazo Waziri Nagu, yupo pamoja na wenzake wakituhumiwa kunununua kadi za wapiga kura- huku TAKUKURU wakiwa wamekaa tu toothless?
Katika mazingira kama hayo, unaweza kusema CHADEMA haina sera- wala CHADEMA haina mikakati?
Tuma mtu Kiteto leo, mgombea wa CCM anapita kwa tabu makao makuu ya wilaya huko Kibaya, wanachi wanazomea. Nenda kata za wananchi waliowengi wenyewe ulewa kama Matui. Leo hii Kiteto haina tu vyombo vya habari, lakini ukweli ni kuwa uchaguzi umeacha majeraha kule- watu wakipita na nguo za CCM nyakati za jioni wananchi wanawapiga.
Ukweli ni kuwa umma umemkubali Kimesera na sera za CHADEMA; lakini kuna sehemu ya umma pia- hususani maeneo ya wafugaji, huko ambapo kampeni zilifanywa kwa kilugha, na vituo kikahamishwa hamishwa na mambo mengine kama ambavyo Mzee Kasisiko Mwenyekiti wetu wa Kigoma ameeleza, huko ndipo kumefanya mambo yakawa yalivyo.
Unapotumia milioni chini ya 50, mwenzio akatumia milioni zaidi ya 500, kwa watanzania imeacha mfumo unaoendeleza umasikini wa kipato, huku wengine wakiwa hawajui kusoma na kuandika; unaweza kabisa kujua nini kitafuata!
Mnakumbuka hapa- kwa uchaguzi wa Tunduru, nilikiri hapa kwamba kweli palikuwa na udhaifu kwa upande wa mgombea wa CHADEMA; lakini kwa Kiteto- ni tofauti kabisa. Badala ya kutumia muda mrefu kuilaumu CHADEMA kuhusu Kiteto, tutumie muda huu kwa yoyote mpenda demokrasia- kuuchambua mwenendo wetu wa uchaguzi na uwanja wetu wa kisiasa- kwa hapa ndipo tatizo la msingi lilipo.
Lakini tusipochukulia hili kwa uzito wake, ipo siku watakuja wapinzani ambao uvumilivu utawashinda, wataendeleza siasa za kuchochea uasi, ili pasiwepo vitisho, rushwa, hujuma na uwizi- kwa kuwa vyombo vya dola, vinashindwa kusimamia sheria zetu kuweka uwanja sawa wa ushindani katika siasa! Madhara ya siasa za uasi ni chuki kuendelea hata baada ya uchaguzi, majeraha yake huchukua muda kuponyeka.
Naamini watanzania tumeona madhara ya siasa za uasi kwa jirani zetu Kenya- tusijaribu kabisa, kutafuta power sharing baada ya uasi kutokea. Tuitafute power sharing mapema, kwa kuruhusu chaguo la wananchi waliowengi kukubalika, kwa kuruhusu ushindani wa kisiasa uwe huru na haki.
JJ
Naona kuwa njia moja kubwa ya kutafuta ushindi kwa upande wa CHADEMA ilikuwa ni helikopta. Yaani waTanzania wamekuwa mbumbumbu kiasi cha kuweza kudanganywa na helikopta? Laiti chadema wangeelekeza nguvu zao kwingine zaidi ya kutegemea helikopta labda matokeo yangekuwa kwingine. Nikimaanisha kuwa, CHADEMA ingewekeza katika kuonyesha maendeleo yepi na kwa mifano si kwa maneno na kabla ya kukurupuka na helikopta dakika za mwisho wakitegemea kuwa, kwa kuwa wanazunguka na helikopta basi ndio chombo cha kuwaletea ushindi. Inashangaza sana, kwani sidhani kama waliona kuwa wanaojazana kwenda kuilaki helikopta ni watoto na wengi si wapiga kura. Na isitoshe hata yaongewayo na huyo aliekuja na helikopta hawayasikilizi, wao huwa wako na issue ya helikopta. Si "washamba" wa helikopta?
Na hili la rigging tumelisikia miaka nenda miaka rudi, linakuwa kama nyimbo. Mimi nauliza hivi, hivi nyumbani kwako kila siku unaibiwa na kudhulumiwa na wewe unapiga kelele tu baada ya kudhulumiwa na kuibiwa miaka yote, huchukuwi preventive security measures? au unategemea "ngoja wamalize kuiba nipate ushahidi"? nashindwa kuelewa.
Kama mambo yenyewe ndio hayo, kitaeleweka tu.
Me, I have a big feeling kuwa most ya viongozi wa CHADEMA si CHADEMA kweli na bado ni wale wale system. Wanadanganya wananchi tu.
Mtanganyika
http://www.chadema.net/mikakati/msingi.php
Long term goals za wagombea vijana tunazitengeneza: http://www.chadema.net/mikakati/msingi.php na naomba utuunge mkono.
In Kiteto, we fought like winners- not losers, soma maelezo yangu hapo juu utaelewa kwa nini nasema hivyo. Katika vijana wa CHADEMA ninao wafahamu, hakuna ambaye alikuwa na crediantials kama za Mzee Kimesera pale Kiteto. He was the candidate the party could foot. Najua hata Mzee Nangoro wa CCM aliyetangazwa mshindi, naye anajua kwamba kwa upande wa crediantials, Mzee Kimesera anaheshima zaidi Kiteto zaidi yake. Lakini uchaguzi, unapokuwa uchafuzi, mambo huwa mengine kabisa.
Inabidi pia wakati wa kujadili, tutofautishe katika ya by election, na uchaguzi mkuu- tabia moja wapo ya by election ni kuwa nguvu yote huwa inamwagwa hapo. Sasa katika siasa zetu zinazoendeshwa kwa kanuni za mwitu, unajua maana yake.
Ya Kiteto ni funzo kwa demokrasia yetu changa, tutazame mbele. Lakini rai yangu ni moja tu- kama tutaendelea kuilaumu CHADEMA, na kuendelea kuacha hali ikawa kama ilivyo katika uwanja wa kisiasa. Tunatangwa maji kwenye kinu. Nyinyi mlio huo ughaibuni, ukisoma hilo tamko ukurasa kwa ukurasa, ukilinganisha na siasa za hapa nyumbani- mnajifunza kitu gani?
Naweza nikawa nazungumza with a lot of emotions- ni kwa sababu uchaguzi wa Kiteto umenikumbusha mambo kadhaa kuhusu Ubungo; kwamba unaweza kuendesha kampeni safi za sera ukakubalika, lakini mwishowe ukashindwa- kwa sababu za tofauti kabisa. Ndio chaguzi zetu hizo! Lakini natazama mbele kwa matumaini makubwa, kwamba mabadiliko yanakaribia.....
JJ
Mtaalamu mwingine wa propaganda na kuhamisha mijadala. We unajua kuwa CHADEMA imetumia helikopta siku mbili za mwisho za Kampeni; siku zingine zote 19 fedha zilielekezwa kwenye mikakati mingine ya kampeni chini kwa chini. Helikopta ambayo iliwapa kiwewe CCM mpaka nao wakakimbilia kukodi helikopta, lakini kwa bahati mbaya CCM walikuwa wakizomewa na helikopta yao
JJ
Mtanganyika
http://www.chadema.net/mikakati/msingi.php
Long term goals za wagombea vijana tunazitengeneza: http://www.chadema.net/mikakati/msingi.php na naomba utuunge mkono.
In Kiteto, we fought like winners- not losers, soma maelezo yangu hapo juu utaelewa kwa nini nasema hivyo. Katika vijana wa CHADEMA ninao wafahamu, hakuna ambaye alikuwa na crediantials kama za Mzee Kimesera pale Kiteto. He was the candidate the party could foot. Najua hata Mzee Nangoro wa CCM aliyetangazwa mshindi, naye anajua kwamba kwa upande wa crediantials, Mzee Kimesera anaheshima zaidi Kiteto zaidi yake. Lakini uchaguzi, unapokuwa uchafuzi, mambo huwa mengine kabisa.
Inabidi pia wakati wa kujadili, tutofautishe katika ya by election, na uchaguzi mkuu- tabia moja wapo ya by election ni kuwa nguvu yote huwa inamwagwa hapo. Sasa katika siasa zetu zinazoendeshwa kwa kanuni za mwitu, unajua maana yake.
Ya Kiteto ni funzo kwa demokrasia yetu changa, tutazame mbele. Lakini rai yangu ni moja tu- kama tutaendelea kuilaumu CHADEMA, na kuendelea kuacha hali ikawa kama ilivyo katika uwanja wa kisiasa. Tunatangwa maji kwenye kinu. Nyinyi mlio huo ughaibuni, ukisoma hilo tamko ukurasa kwa ukurasa, ukilinganisha na siasa za hapa nyumbani- mnajifunza kitu gani?
Naweza nikawa nazungumza with a lot of emotions- ni kwa sababu uchaguzi wa Kiteto umenikumbusha mambo kadhaa kuhusu Ubungo; kwamba unaweza kuendesha kampeni safi za sera ukakubalika, lakini mwishowe ukashindwa- kwa sababu za tofauti kabisa. Ndio chaguzi zetu hizo! Lakini natazama mbele kwa matumaini makubwa, kwamba mabadiliko yanakaribia.....
JJ