Kaka Ahsante na wewe. Inabidi nilale maana saa hizi, ni kulala kwa dakika chache si saa chache. Hayo ni matokeo ya saa 7.15 (01.15hrs) ambako CCM walikua wakiongoza kwa tofauti ya kura takriban 2000, lakini kasi ya Chadema ilikua kubwa kwani saa 6.06(00.06) CCM walikua wakiongoza kwa tofauti ya kura 4,000 ambazo baada ya saa moja za Chadema ziliongezeka. Lakini wakati huo sehemu kubwa walikua wamekwisha kuhesabu. Kuna UKIUKWAJI mkubwa wa taratibu katika uchaguzi huo na kwa hali ilivyo KAMA CCM watashinda itakua ni ushindi wa AIBU. Kwa idadi kubwa ya wabunge walionao hawakua na sababu ya kufanya yaliyotokea Kiteto, pamoja na kuwa ni MKAKATI WA kuzuia UPEPO wa MABADILIKO.
CCM wanaelekea kushinda japo kwa tofauti ndogo kama hakutakua na muujiza wowote katika maeneo machache yaliyosalia. Nadhani huu ni wakati ambao Chadema wamefanya mazoezi ya kulichukua hilo jimbo 2010 kwani CCM wakati huo kila mtu atakua anatetea jimbo lake na si wote kuhamia Kiteto. TATIZO KUBWA (SIJUI KWANINI) zaidi ya nusu ya wapiga kura hawajajitokeza kupiga kura na zaidi katika maeneo ambayo mgombea wa CHADEMA ana wafuasi wengi. Inawezekana ilikua ni mkakati maalumu wa CCM na hapo ndipo wapinzani wanapopata fundisho la kujiandaa kwa mikakati na si mambo ya "mbwembwe". CCM wanaangalia wapi ulipopasahau na hapo ndio watapita, hawana njia moja ya kupata ushindi. Wakikosa katika kampeni za kawaida watakumaliza kampeni za kimkakati, wana timu na wataalamu wa kila fani wakiwamo wanaolipwa fedha za walipa kodi (watumishi wa serikali). Tuna safari ndefu ya kutokea mabadiliko katika nchi hii.
Mtazamo safi sana halisi.
Ijapokua CCM wamesambaratika na kashfa zinazokumba nchi ni wazi kuwa upinzani wana-homework ya kufanya.This will always take time maana democracy has to mature.Pia hilo swala la watu kujitokeza kupiga kura hua lipo in most places maana ari ya kujitokeza huonekana sana wakati wa uchaguzi mkuu.
Civil Education has to be promoted through NGO's.The government itself and other organs of State.Hapo nd'o tutaweza kusema vizingiti vya demokrasia vimeanza kukita.It will take time lakini tutafika.Asanteni
Kwa muda wenu tetembeleeni: http://www.eastafricayote.com/index.php
mpya zilizopo kuwa chadema wameangukia pua.
tunatanguliza pole zetu kwa ndugu zetu na wamejitahidi sana ila ndio hivyo bado ni wachanga mno.
wache wajipange zaidi huenda baada ya miaka 20 wanaweza kuaminila alau kupata baadhi ya majimbo.
sasa uchaguzi umeisha tushirikiane ktk kuijenga kiteto na tanzania
Mimi nitakuwa Thomaso hadi pale nitakapoona matokeo rasmi walau kura 40,000 zikiwa zimehesabiwa na walau sisiem inaongoza kwa zaidi ya kura 10,000 ndio niweze kusema ni kweli wameshinda vinginevyo hakuna mshindi hadi sasa. Tusubiri matokeo in term of numbers sio maneno.
no haya si maneno tu hizi ni habari za ndani/. la kama huamini subiri magazeti hapa jf ss hupokea habari in first hand.
ila nnachosubiri ndugu zangu kuja na sababu za kushindwa. huenda wakaja kutwambia alipewa sumu, komba kaimba kwenye mkutano wao, polisi walipendelea, ccm imetumia dola, na mengi ya uzushi.
nitawaona mashujaa kama chadema kukubali matokeo bila ya manung'uniko na kukubali asiekubali kushindwa si mshindani.
upinzani unahitaji kujipanga zaidi, wasikate tamaa jitahidini sana.
na usione simba karoa ukadhani kesha.
Mtu wa pwani naomba nitofautiane na kauli yako hapo juu!!!!!!! Kumbuka kwamba uchaguzi una taratibu zake na ukiukwaji wa makusudi wa taratibu hizo basi huufanya uchaguzi huo kutokuwa huru na haki!!!!!!!!!
Chadema wanaweza kutumia mapungufu yeyote ya msingi yaliyojitokeza kupinga matokeo na hiyo ni sehemu halali demokrasia. Hivyo basi kuanza kubeza mapema kabisa namna hii wakati hata matokeo hayajajulikana ni dalili za ushabiki usiokuwa na tija na inaweza pia kuashiria kuwa aidha una chuki na chadema au wanachadema au mashabiki wa chadema.
someni matokeo kutoka kushoto kwenda kulia inaanza na CHADEMA,CCM ,PPT NA SAU.
Imegoma kuattach excel ndio maaana imekuwa hivyo wakuu samahanini.
Ni kwasababu wameshindwa... otherwise kungekuwa na zaidi ya mabandiko kumi kuhusu kitetoMbona hujazimwaga data hizo kama BREAKING NEWS?
Unanichekesha, yaani unataka kujiunga katika chama kwa lengo moja tu, la kugombea ubunge? Bora ubaki hivyo hivyo, bila ya chama, uendelee kuwakebehi wapinzani.
Ni kwasababu wameshindwa... otherwise kungekuwa na zaidi ya mabandiko kumi kuhusu kiteto
1. Chadema kuna nini? Hata hiki kiti kimoja tu mnashindwa? Au ni kusindwa tu kawaida? Kuna matatizo ndani ya Chama? Au bado ni mbinu chafu za CCM? Je Chadema hakukuwa na mbinu chafu nao? Well kwa mwelekeo huu basi Upinzani una mda mrefu kupata fursa kuongoza dola Tz- as CCM wataendelea kutawala kwa miaka mingi ijayo! Poleni, it is a challenge CHADEMA, mmejifunza, tusonge mbele!
2. Naomba ushauri- Sasa mimi kwa sasa sina Chama na ni mzalendo kweli (Halisi)..nauliza kama nataka kugombea nijiunge na Chadema au CCM?