Uchaguzi wa ajabu chuo cha ardhi

didy muhenga

Member
Nov 8, 2022
12
10
Leo mnamo tarehe 3/5/2024 ni siku amabayo uchaguzi wa chuo kikuu ardhi ulipaswa kufanyika kulingana na almanac ya chuo na taarifa hio wamafunzi wote walikua nayo na wagombea walijipanga kwa ajili ya sku hio.

Jambo la ajabu na kusikitisha ni kwamba eti leo asubuhi ilitoka taarifa kua uchaguzi umepelekwa mbele hadi mchana, ilipofika mchana ikatoka taarifa kua uchaguzi umeghairishwa mpaka jumatatu kwa sababu ya kwamba ety majina ya wanafunzi hayaonekani kweny daftari la tume ya uchaguzi.

Hii ni aibu kubwa sana kwa chuo chetu na nchi kiujumla ety uchaguzi unaighairishwa kisa majina hayajaprintiwa.Na tuna tume kabsa ya uchaguzi ina watu kabisa yaan ni jambo la ajabu kuwahi kutokea ni mfifisho wa demokrasia na uwepo wa dalili ya kuwepo kwa upangaji wa matokeo.

Kwanza moja ya sifa mtu kugombea urais lazima mtu awe of good conduct Lakini kuna mgombea mmoja alimtukana mwanafunz mwenzake matusi ya nguoni kabsa na ushahid ukapelekwa na kesi ikaenda hadi polisi lakini bado jamaa akapitishwa bila sababu kwa maan tu mwenyekiti wa tume yupo upande wake yaan spika, Spika ambaye aliulizwa nini maan ya good conduct alikua hajui na bado akaulizwa characteristics of good leadership akashindwa kutaja na ety ndo kiongozi wa baade, it's a great shame.

Mwisho kabsa naomba ardhi university walisemee hili maana wapo vizuri kujibu kama ilivyotokea ile issue ya wale malachi waliofanyiana mtihan.
 
Madogo siku hizi mnazingua sana, ardhi ni Moja ya chuo makini sana hapa nchini ila naangalia uandishi wako nabaki kusikitika tu, mnaaibisha vyuo vyenu

Mtoto wa kiume haipendezi kutumia maneno kama ety,maan andika maneno kwa usahihi kijana acha unyoronyoro
 
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ni Spika wa Bunge la chuo. Hahaha na wote hapo chuoni mkakubali kabisa?. Anyway utashangaa hata wapigakura wasifike nusu ya wanafunzi wote.

Vitu vidogo vinaanzia mbali sana ili vikue vikubwa.
 
Huo uandishi sio kipimo sahihi cha uwezo wangu kikubwa ujumbe umeupata mkuu.
 
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ni Spika wa Bunge la chuo. Hahaha na wote hapo chuoni mkakubali kabisa?. Anyway utashangaa hata wapigakura wasifike nusu ya wanafunzi wote.

Vitu vidogo vinaanzia mbali sana ili vikue vikubwa.
Ndo tupo kweny mageuzi ya katiba Mgeni wa jiji Lakini ni ngumu sana kuipata impartiality ambayo tunaipigania
 
Eti, ety, ety zimekuwa nyingi, mtoa mada ni jinsia gani kwanza?

Wewe hapo chuo umefuata uchaguzi au masomo?

Stress zingine ni kujitafutia tu.
 
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ni Spika wa Bunge la chuo. Hahaha na wote hapo chuoni mkakubali kabisa?. Anyway utashangaa hata wapigakura wasifike nusu ya wanafunzi wote.

Vitu vidogo vinaanzia mbali sana ili vikue vikubwa.
Nimeshangaa spika ndo mwenyekiti wa Time,
Hii nchii kumbe inaanziaga chini kabisa, Lol
 
mmh naona hamna test
inabidi mpewe test 10 kwa wiki moja uhuru mliopewa umepitiliza
 
Back
Top Bottom