Wadau,
Nipo Dom hapa nazugazuga tu katika kujaribu kuangalia hizi chaguzi za CCM. Huyu mama kaaibika sana kwakweli...
Story ilianza hivi;
Alisimama ili aulize swali ila akawa kama anahutubia vile, watu wakaanza kelele na kuanza gumzo, akawa anamwambia Mwenyekiti wa uchaguzi amlinde kwani watu wanamzomea, Mwenyekiti akambeza "We uliza swali hatutaki hotuba", ila haikuwa vile akawa anaongea tu huku Mwenyekiti anamtuliza hataki, watu nao wakaja juu, akaanza kutoka nje ya mada na kudai wote hapa hamfai hamuwezi kuchagua kiongozi.
Akawa anakashifu taratibu na ndivyo wakawajibika kumtoa ila akawa bado anaongea kama kalewa, watu wanamzomea, wanamtoa nje na huku anatukana, watu wanatamani kumpiga, chaguzi za magamba, ni aibu aisee