Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,534
- 24,083
Mwaka jana nlisema kuwa Ukawa watashinda uchaguzi ila Rais atatangazwa wa CCM wengi walinibishia na kunitukana. Nimekuwa na access ya kufaham mambo mengi yanayoendelea hapa nchini. Na wengi kwa kuwa wananiona mimi ni chizi hawajali maneno yao wanapoongea nami ninapoongea.Zanzibar nlisema kama CCM wamesema uchaguzi utafanyika basi utafanyika. Na hili limeandaliwa kwa ustadi mkubwa ikiwa ni pamoja na kuwaandaa watu kisaikolojia kupitia wasomi walionunuliwa ,viongozi wa dini na wanasiasa wakongwe.Hawa watatumika kutoa matamko ya kuunga mkono uchaguzi kurudiwa na nadhani wengine mmewasikia na wengine watasikika tena na tena. Kuna ambao wametishiwa kutokana na kesi walizo nazo na wengine kutokana na ufisadi waliowah kuufanya hivyo wamelazimishwa kuukubal uchaguzi urudiwe. Wengine ni pesa na ahadi ndizo zinazotumika. Tegemeeni meng sana.uchaguzi zanz unarudiwa .CCM WATASHINDA na zanzibar itabaki na amani kusubiria miaka 5 mingne ijayo suala la kuvunjika aman halipo. Watu wamejipanga sana kutimiza haja za mioyo yao na Zitatimizwa