Hivi uchaguzi ukirudiwa Zanzibar CUF watafanyaje?

juvenile davis

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
4,752
4,463
Jamani mi kuna swali najiuliza na kuwaza ila jibu sipati.mwenye majibu labda anisaidie.
Najiuliza hivi ikitokea zanzibar ikifika mwisho wa siku uchaguzi unarudiwa hawa ndugu zangu wa ukawa wenzangu wa CUF watafanya nini?
Je watasusia silu ya uchaguzi? Kama ni hivo ccm basi watashinda kwa kishindo ngazi zote mana hawatakuwa na upinzani kwa kuwa vyama vingine ni vya kipuuzi tu
na je baada ya kususia uchaguzi ni nn kitafuata?
Mawazo yangu
Mi nadhani maalimu seif hamad sharifu na ismail jusa ladhu na viongozi wa CUF wangejikita kuelimisha wananchi wakapige kura kwa wingi ili ushindi uende CUF tena (kama wao walivosema walishinda).hatutaki kuja kusikia lawama baada ya uchaguzi kupita,unless otherwise watuambie je baada ya kususa ni hatua gani watazifuata? Au ni kususa tu bora kususa harafu cha maana hakuna? Kama hawana kitu ambacho watafanya baada ya ushindi wa ccm basi ni afadhari wakakubali yaishe tu warudie uchaguzi na wasisuse.maana kuna kila dalili zote ya kwamba uchaguzi utarudiwa tuuu.ccm wenzetu wapo busy kuelimisha wanachama wao wajiandae na uchaguzi,wao CUF wapo busy kuelimisha wanachama wao kwamba uchaguzi haurudiwi,sasa uchaguzi ukirudiwa harafu CCM wakawa ni washindi basi kelele hatutaki,mana mnasusa bila kuelewa nini kitafuata baada ya kususa,msije mkawa kama wale viongozi wa chadema waliosema hawamtambui kikwete harafu muda si mrefu tukawaona ikulu na kikwete yuleyule ambae hawakumtambua kama raisi wanakunywa nae chai
 
Kauli ya kwamba vyama vingine ni vya kipuuzi sijaipenda au pengine vikijiunga na UKAWA utabadili gia angani!
 
wewe unataka usaidie kujua au unataka cuf wakubali kurudia uchaguzi maana ueleweki uko kama msukule wa lumumba
 
Jamani mi kuna swali najiuliza na kuwaza ila jibu sipati.mwenye majibu labda anisaidie.
Najiuliza hivi ikitokea zanzibar ikifika mwisho wa siku uchaguzi unarudiwa hawa ndugu zangu wa ukawa wenzangu wa CUF watafanya nini?
Je watasusia silu ya uchaguzi? Kama ni hivo ccm basi watashinda kwa kishindo ngazi zote mana hawatakuwa na upinzani kwa kuwa vyama vingine ni vya kipuuzi tu
na je baada ya kususia uchaguzi ni nn kitafuata?
Mawazo yangu
Mi nadhani maalimu seif hamad sharifu na ismail jusa ladhu na viongozi wa CUF wangejikita kuelimisha wananchi wakapige kura kwa wingi ili ushindi uende CUF tena (kama wao walivosema walishinda).hatutaki kuja kusikia lawama baada ya uchaguzi kupita,unless otherwise watuambie je baada ya kususa ni hatua gani watazifuata? Au ni kususa tu bora kususa harafu cha maana hakuna? Kama hawana kitu ambacho watafanya baada ya ushindi wa ccm basi ni afadhari wakakubali yaishe tu warudie uchaguzi na wasisuse.maana kuna kila dalili zote ya kwamba uchaguzi utarudiwa tuuu.ccm wenzetu wapo busy kuelimisha wanachama wao wajiandae na uchaguzi,wao CUF wapo busy kuelimisha wanachama wao kwamba uchaguzi haurudiwi,sasa uchaguzi ukirudiwa harafu CCM wakawa ni washindi basi kelele hatutaki,mana mnasusa bila kuelewa nini kitafuata baada ya kususa,msije mkawa kama wale viongozi wa chadema waliosema hawamtambui kikwete harafu muda si mrefu tukawaona ikulu na kikwete yuleyule ambae hawakumtambua kama raisi wanakunywa nae chai
Sasa kama uchaguzi ulishafanyika urudiwe wa nini? Huoni kama kuna maluweluwe hapo. Umewahi kukaa kutafakarina kujiuliza kwanini uchaguzi unarudiwa? Na ulifutwa kwa sababu gani
 
Ukirudiwa na CCM wakashindwa kwa kishindo je,watarudia tena???Au CUF walishindwa na walitaka Uchaguzi urudiwe CCM it akubali???Ni kitendawiki ambacho hakuna anayeweza kujibu sababu ya Madaraka
 
Wewe mtoa mada .elewa hivi .hata cuf wakirudia uchaguzi mara mia .hawatotangazwa kama wameshinda .kwa sababu zanzibar hawajali wala hawataki demokrasiabya kura .
Ww uko wapi mbona huelewi? .jecha ndio atasimamia uchaguzi tena akiona cuf inaelekea kushinda anafuta tena sasa wewe mbona hujui hilo .? Unaakili gani weewe?.hawa wanataka cuf waingie ili wafanye ujanja wa kumtangaza mtubwao kwa nguvu sio kwa kura .bado hujaelewa ninibkinatafutwa? Kinachotafutwa ni ushindi wa kulazimisha
 
Sasa kama uchaguzi ulishafanyika urudiwe wa nini? Huoni kama kuna maluweluwe hapo. Umewahi kukaa kutafakarina kujiuliza kwanini uchaguzi unarudiwa? Na ulifutwa kwa sababu gani

Na kama sababu ni kujitangaza na sio CCM kushindwa basi namwomba Maalim Seif akubali tu kurudia halafua ajitangaze tena ili ufutwe tena.
Na ukirudiwa ajitangaze tena ili ufutwe na ukirudiwa iwe hivyo hivyo kama kweli adhabu ya kujitangaza ni kufutwa kwa uchaguzi nchi nzima je,wawakilishi ambao hawakujitangaza haki yao iko wapi?
Jecha amefanya jambo baya sana kwa wazanzibari ili tu kufurahisha watu wachache.
Historia itamuhukumu milele.
Jambo alilofanya halifai kabisa kuigwa na au kufanyika kwenye nchi yoyote yenye binadamu wenye utu na hekima.
Tumuombe tu Mungu aepushe nchi yetu isije ikatokea tena mwanamke atakayezaa mtu wa aina hii mana ni dalili mbaya na janga kwa taifa.
Mola tuepushe na watu wa aina ya Jecha kwani ndio wanaoleta machafiko duniani kwa kukosa busara.
Tulikubali Shein agombee kiti cha urais na Maalim Seifu tukiamini kuwa wote ni Wazanzibar tena waislam kwa kujua kua atakayeshinda atawaongoza wazanzibari leo hii Jecha anatuambia kuwa matoleo na kura zimeharibika kwa wajumbe kupigana na Maalim seifu Kujitangaza jambo ambalo halina uhusiano. Hivi Huyo Jecha hajui kuwa kupigana ni kosa la jinai na sio kosa la kisiasa?Kwa nini kupigana wa watu tena nje ya kituo cha kupiga kura kuathiri uchaguzi?
Je ni kituo kipi cha kupigia kura ambacho wapigakura wameshindwa kujitokeza au kupiga kura kwa sababu ya wajumbe wa ZEC kupigana?
Kwama watanzania wote tutakaa kimya na kukubaliana na maamuzi ya hatari ya Jecha basi tutakua tumefanya dhambi kubwa sana.
Leo hii Zanzibar ingekua imemtangaza Maalim Seif kwa ushindi wake halali na wananchi wa vyama vyote kuunganishwa na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kama ilivyokuwa kwa Muda uliopita baada ya Dr.Shein kushinda na CUF wakakaa pamoja na CCM basi Zanzibar wangezidi kuwa na umoja na amani na utulivu zaidi huku kila moja akiona jinsi demokrasia ilivyokua na ubaguzi na lugha za kibaguzi zisingekuwepo kama inavyozidi kutokea.
Pia nchi yetu ingezidi kupokea pesa MCC na kuimarisha bajeti yake.

Sijui itakuaje endapo CUF itasusia uchaguzi!
Tutakua tumerudishwa nyuma na maamuzi ya ajabu ya mtu mmoja.
Ni lazima watu kama Jecha wapigwe vita kwa nguvu zote ni hatari mno kwa ustawi wa nchi na demokrasia.
Roho inaniuma sana ninapoona kuwa mtu mmoja ameamua kuvuruga ule umoja wa kitaifa uliokwepo na wananchi waliofikia mahali wansherehekea kwa pamoja kati ya CUF na CCM kwenye maadhimisho mbalimbali.

Ushauri wangu ni kuwa Endapo Zanzibar uchaguzi utarudiwa basi tume ya uchaguzi isiongozwe na Jecha na ikiwezekana watoke wasimamizi kutoka nchi za nje kama vile Botswana ,South Afrika na Ghana lakini sio tume iliyoundwa na Dr. Shein ambayo imeshindwa.
 
Ukirudiwa na CCM wakashindwa kwa kishindo je,watarudia tena???Au CUF walishindwa na walitaka Uchaguzi urudiwe CCM it akubali???Ni kitendawiki ambacho hakuna anayeweza kujibu sababu ya Madaraka

Je,Maalim Seif atajitangaza tena na wajumbe wakapigana uchaguzi utarudiwa tena?
Na wakiendelea kufanya hivyo hivyo tena na tena utarudiwa tena na tena au na usanii tu wa Jecha?

Na kama hautarudiwa tena na tena na tena ni kwa nini adhabu ya kujitangaza imewaathiri wawakilishi ambao hawakujitangaza?
 
Watasusia na ikiwezekana patatokea vurugu zisizo mfano na kama itakuwa hivyo
huo ndio utakuwa mwisho wa kitu kiitwacho muungano na kama serikali
haitachukua hatua sasa juhudi kubwa iliyofanywa na wasisi wetu itakuwa ni bure na
pengine kunaweza kupelekea kuyumba kwa uchumi wetu.
Binafsi naona suala hili kama ni mtego kwa mpendwa wetu Mh.Rais. ,lakini sidhani kama
suala hili litamshinda.

Cha kufanya
1.Kuzuia kurudiwa kwa uchaguzi na kama utafanyika lakini isiwe sasa.

2.Kuitisha bunge la katibu na kuwashirikisha wajumbe wote wa baraza la
wawakilishi katika bunge hilo ili kama ikiwezekana kufanya review ya katiba
ili kama kuna mapungufu au maboresho yaweze kufanyika kwa haraka.

3. Kura ya maoni ifanyike kwa Wazanzibar wote kuulizwa kama wanataka
ama " Uchaguzi urudiwe, Makamu wa Rais wa JMT awe ndiye Rais wa Zanzibar au
Kutangazwa matokeo yaliyofutwa".Kama itafaa waulizwe pia kama bado wanauhitaji
muungano.

4.Kuondoa ile dhana ya lazima chama chetu kishinde na badala yake kuweka
dhana ya lazima Wazanzibar wote washinde katika hili kwani ni wao pekee
wenye dhamana ya maisha yao na si kuwa watumwa wa wanasiasa.

5.Pasipo kuwa na woga wowote chama tawala kikubali ushauri uliotolewa
na baba wa Taifa Mwl.J.K Nyerere alioutoa kwa wenzetu nchini Burundi ili
utumike .

6.Kuitisha mjadala wa wazi wa wanazuoni ili kujadili kwa kina nini kifanyike
kwa maana ya suluhisho la kudumu au la mpito.
 
Aliyoyafanya Jecha hayana tofauti na aliyoyafanya Kivuitu mwaka 2007 kule Kenya alipomtangaza Kibaki kuwa ndiye mshindi wa kiti cha Urais wakati akijua kuwa mshindi wa uchaguzi ule alikuwa Raila Odinga.

Kutokana na madudu hayo ya Kivuitu yalisababisha vifo vya wakenya wasiopungua elfu moja.

Ni vyema waTZ wakatambua kuwa kitendo alichofanya Jecha cha kukataa matakwa yaliyofanywa na wazanzibari yanaweza kuitumbukiza nchi yetu kwenye machafuko makubwa.

Japo watawala wetu wanatulazimisha wananchi wote tujifanye 'vipofu' na tusiione hatari inayolinyemelea Taifa letu.
 
Wana cuf wanaogopa nn kurudia uchaguz ?kama walishinda ni wakati mwafaka wa wao kwenda kupiga kura na kushinda kwa kishindo zaid ili wanalumbumba kama waliiba ijulikane tu wazi hamna kuuana wala nn...ukweli ujulikane.
 
Huo uchaguzi ulishafanyika na ccm walishashinda kwa nini Cuf wapoteze muda kwa mchezo wa kuigiza wanataka wajione nao Pemba wanakubalika kumbuka kura ya maruhani hii imejirudia tu walishindwa kufuta pemba peke yake kwa maana yao
 
Kurejea uchaguzi ni sawa tu nakuhalalisha haramu iliyotukuka, uchaguzi tulishafanya zamani tangu trh 25 na ulimaliza tarehe hiyo cc wapemba hatuingii uwanjani tena na haswa ukizingatia ccm hawajawahi kupata hata kiti kimoja hata kile kisichokua na mamlaka makubwa kwa huku cha udiwani since 1995! Tumewakataa kwa mikono na midomo yetu, HATUHITAJI TENA UCHAGUZI PBA tunataka matokeo yaendelee kumaliziwa kutangazwa!
 
ukweli utatuweka huru. aliyeshinda atangazwe. dhuluma sio nzuri siku zote na hutengeneza manung'uniko na masononeko mioyoni mwa watu.
Jamani mi kuna swali najiuliza na kuwaza ila jibu sipati.mwenye majibu labda anisaidie.
Najiuliza hivi ikitokea zanzibar ikifika mwisho wa siku uchaguzi unarudiwa hawa ndugu zangu wa ukawa wenzangu wa CUF watafanya nini?
Je watasusia silu ya uchaguzi? Kama ni hivo ccm basi watashinda kwa kishindo ngazi zote mana hawatakuwa na upinzani kwa kuwa vyama vingine ni vya kipuuzi tu
na je baada ya kususia uchaguzi ni nn kitafuata?
Mawazo yangu
Mi nadhani maalimu seif hamad sharifu na ismail jusa ladhu na viongozi wa CUF wangejikita kuelimisha wananchi wakapige kura kwa wingi ili ushindi uende CUF tena (kama wao walivosema walishinda).hatutaki kuja kusikia lawama baada ya uchaguzi kupita,unless otherwise watuambie je baada ya kususa ni hatua gani watazifuata? Au ni kususa tu bora kususa harafu cha maana hakuna? Kama hawana kitu ambacho watafanya baada ya ushindi wa ccm basi ni afadhari wakakubali yaishe tu warudie uchaguzi na wasisuse.maana kuna kila dalili zote ya kwamba uchaguzi utarudiwa tuuu.ccm wenzetu wapo busy kuelimisha wanachama wao wajiandae na uchaguzi,wao CUF wapo busy kuelimisha wanachama wao kwamba uchaguzi haurudiwi,sasa uchaguzi ukirudiwa harafu CCM wakawa ni washindi basi kelele hatutaki,mana mnasusa bila kuelewa nini kitafuata baada ya kususa,msije mkawa kama wale viongozi wa chadema waliosema hawamtambui kikwete harafu muda si mrefu tukawaona ikulu na kikwete yuleyule ambae hawakumtambua kama raisi wanakunywa nae chai
 
Jamani mi kuna swali najiuliza na kuwaza ila jibu sipati.mwenye majibu labda anisaidie.
Najiuliza hivi ikitokea zanzibar ikifika mwisho wa siku uchaguzi unarudiwa hawa ndugu zangu wa ukawa wenzangu wa CUF watafanya nini?
Je watasusia silu ya uchaguzi? Kama ni hivo ccm basi watashinda kwa kishindo ngazi zote mana hawatakuwa na upinzani kwa kuwa vyama vingine ni vya kipuuzi tu
na je baada ya kususia uchaguzi ni nn kitafuata?
Mawazo yangu
Mi nadhani maalimu seif hamad sharifu na ismail jusa ladhu na viongozi wa CUF wangejikita kuelimisha wananchi wakapige kura kwa wingi ili ushindi uende CUF tena (kama wao walivosema walishinda).hatutaki kuja kusikia lawama baada ya uchaguzi kupita,unless otherwise watuambie je baada ya kususa ni hatua gani watazifuata? Au ni kususa tu bora kususa harafu cha maana hakuna? Kama hawana kitu ambacho watafanya baada ya ushindi wa ccm basi ni afadhari wakakubali yaishe tu warudie uchaguzi na wasisuse.maana kuna kila dalili zote ya kwamba uchaguzi utarudiwa tuuu.ccm wenzetu wapo busy kuelimisha wanachama wao wajiandae na uchaguzi,wao CUF wapo busy kuelimisha wanachama wao kwamba uchaguzi haurudiwi,sasa uchaguzi ukirudiwa harafu CCM wakawa ni washindi basi kelele hatutaki,mana mnasusa bila kuelewa nini kitafuata baada ya kususa,msije mkawa kama wale viongozi wa chadema waliosema hawamtambui kikwete harafu muda si mrefu tukawaona ikulu na kikwete yuleyule ambae hawakumtambua kama raisi wanakunywa nae chai
Msikilize Lubuva anasemaje kuhusu Kura zilizopigwa Zanzibar?

Sio kama wanavyosema,wana ushahidi wa fomu za matokeo yaliyobandikwa majimboni na CCM pia wanazo fomu hizo za matokeo. Waombe CCM ambao unawapigia debe wakuoneshe kama hujaziona.
CCM wameshindwa na CUF kwa wingi wa kura lakini wametengeneza "mkwamo".

ZEC wamalizie kutoa matokeo na sio kufanya ubadhirifu wa fedha za umma kwa kurudia uchaguzi ili "kuishindisha" CCM au "kutoshelezesha kura za CCM".

Hakuna sababu za msingi za kurudia uchaguzi. CCM wajifunze kukubali kushindwa. Sio siri tena kuwa CCM wamepora ushindi wa CUF tokea uchaguzi wa 1995 na mara hizo zote CCM wamekataa kuachia madaraka. CCM ndio itaingiza nchi hii katika uvunjifu wa amani.

Kama CCM wanalazimisha kurudia uchaguzi, ni bora hizo fedha watumie kujenga miundo mbinu na sio kubadhiri fedha za umma. CCM waendelee kama wanavyoendelea sasa, kung'ang'ania madaraka. Waendelee mpaka 2020 kama bado nchi itakuwa haijafata mfano wa Burundi, wabadilishe Katiba na wapige marufuku vyama vingi ili CCM iendelee kuwaletea "maisha bora" wanaowatawala. Hivi wanavyowadhalilisha wapiga kura wao inatosha,wawaache wauguze maumivu yao badala ya kuwaletea mengine kwa kuitisha uchaguzi ambao tayari wameshapanga matokeo yake.
 
Jamani mi kuna swali najiuliza na kuwaza ila jibu sipati.mwenye majibu labda anisaidie.
Najiuliza hivi ikitokea zanzibar ikifika mwisho wa siku uchaguzi unarudiwa hawa ndugu zangu wa ukawa wenzangu wa CUF watafanya nini?
Je watasusia silu ya uchaguzi? Kama ni hivo ccm basi watashinda kwa kishindo ngazi zote mana hawatakuwa na upinzani kwa kuwa vyama vingine ni vya kipuuzi tu
na je baada ya kususia uchaguzi ni nn kitafuata?
Mawazo yangu
Mi nadhani maalimu seif hamad sharifu na ismail jusa ladhu na viongozi wa CUF wangejikita kuelimisha wananchi wakapige kura kwa wingi ili ushindi uende CUF tena (kama wao walivosema walishinda).hatutaki kuja kusikia lawama baada ya uchaguzi kupita,unless otherwise watuambie je baada ya kususa ni hatua gani watazifuata? Au ni kususa tu bora kususa harafu cha maana hakuna? Kama hawana kitu ambacho watafanya baada ya ushindi wa ccm basi ni afadhari wakakubali yaishe tu warudie uchaguzi na wasisuse.maana kuna kila dalili zote ya kwamba uchaguzi utarudiwa tuuu.ccm wenzetu wapo busy kuelimisha wanachama wao wajiandae na uchaguzi,wao CUF wapo busy kuelimisha wanachama wao kwamba uchaguzi haurudiwi,sasa uchaguzi ukirudiwa harafu CCM wakawa ni washindi basi kelele hatutaki,mana mnasusa bila kuelewa nini kitafuata baada ya kususa,msije mkawa kama wale viongozi wa chadema waliosema hawamtambui kikwete harafu muda si mrefu tukawaona ikulu na kikwete yuleyule ambae hawakumtambua kama raisi wanakunywa nae chai
SIJUI UNAFIKILIA WAPI? KWANZA NI TUME IPI ITASIMAMIA UCHAGUZI KAMA SI KULAZIMISHA MAMBO. HII YA JECHA KIKATIBA HAIPO, NA WAJUMBE WAKE WAPO WA CUF AMBAO BILA WAO FORUM HAITIMII. NYIE MNADHANI TUMME NI YEYE JECHA TU. BY ANY MEANS UCHAGUZI AMBAO NI HALALI HAIWEZEKANI
 
Back
Top Bottom