Zanzibar 2020 Uzinduzi wa kampeni za CCM Zanzibar: Mwinyi kuhakikisha Zanzibar inanufaika na bahari, kuleta Upendo na amani

the horse

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
605
500
Chama Cha Mapinduzi Zanzibar leo tarehe 12 Septemba 2020 kinafanya mkutano wa uzinduzi wa Kampeni zake katika Uwanja wa Demokrasia, Kibandamaiti. Mgombea wa Kiti cha Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dokta Hussein Ally Mwinyi ataeleza dhamira yake ya kuitumikia Zanzibar.

Mkutano huu utarushwa mubashara na vituo vya televisheni vya TBC, ZBC, Clouds TV, Channel 10 na ITV, pia matangazo yatarushwa live kupitia kurasa rasmi za Chama Cha Mapinduzi katika mitandao ya kijamii;

Twitter; @ccm_zanzibar @ccm_tanzania & @hpolepole

facebook; @zanzibarCCM na @tanzaniaCCM

Youtube CCM Zanzibar & CCM Tanzania

Instagram: @ccmtanzania

#YajayoNineemaTu
#TwendeNaMwinyi
#KuraKwaMwinyi2020

WhatsApp Image 2020-09-12 at 12.11.42.jpeg

Kikundi cha Zanzibar Big Star kikiwa jukwaani kutoa burudani kwa wanachama wa CCM na wananchi wa Zanzibar waliojitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa Kampeni za Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, Uwanja wa Demokrasia, Kibandamaiti.

231d9a24-c487-4a90-8f1e-c5ba2903fb3f.jpg

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Mpendae Zanzibar wakiwa njiani kuelekea katika Uwanja wa Demokrasia, Kibandamaiti kushuhudia uzinduzi wa Kampeni


=======

DOKTA ALLY SHEIN RAIS WA ZANZIBAR AMESEMA;

‘’Dkt. Mwinyi miaka 20 iliyopita alikuwa Mbunge wa jimbo la Mkuranga na mihula mitatu katika jimbo la Bohani, ni mwanasiasa aliyebobea anaijua siasa, ana taaluma kubwa ni daktari bingwa wa maradhi ya binadamu’’ - Dkt. Ally Shein.Rais wa Zanzibar

"Dkt. Mwinyi anasifa zote za kuwa kiongozi wa CCM kuiongoza zanzibar bila mushkeli, mimi ni Rais wa Zanzibar ninamfahamu na chama kikamchagua kwamba ana uwezo wa kuiongoza Zanzibar’’ - Dkt. Ally Shein

"Muungano wetu wa serikali mbili ya Tanzania, ndio uhai wetu na ndio roho yetu watu wa Zanzibar". Dkt .Ally Shein.

"Leo tunapozindua kampeni hii, nataka mzingatie maelezo yangu, msije mkafanya makosa ya kujaribu uongozi, kumpa mtu ambae hana uwezo, kumpa mtu ambae ana tamaa yake binafsi".Dkt.Shein.

"Tutatoa ajira laki tatu (3) kwenye sekta rasmi na zisizo rasmi, lakini haya yote yatawezekana mkitupatia ridhaa ya kuiongoza Zanzibari." Hussen Mwinyi mgombea wa urais Zanzibar kwa tiketi ya CCM awaahidi Wazanzibari hii leo katika uzinduzi wa kampeni viwanja vya Kibanda Maiti.

MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR HUSSEIN MWINYI AMESEMA;

"Tuache kufanya kazi kwa mazoea, katika hili niseme wazi kwenye serikali iwapo mtanichagua kuwa Rais wa awamu ya nane, naweka bayana kabisa nitawawajibisha wale wote wasiowajibika" - Dkt Hussein Mwinyi, Mgombea Urais Zanzibar kwa tiketi ya CCM

"Tutaweka mkazo mkubwa tuhakikishe kwamba amani na upendo vinatawala kwa sababu bila amani hakuna maendeleo, tutaendelea kudumisha amani siku zote’’ - Dkt. Hussein Mwinyi, Mgombea Urais Zanzibar

"Tutaendeleza kukuza uchumi wa nchi kwa kasi, ndugu zangu visiwa hivi vina kila sababu ya kunufaika na bahari tuliokuwa nayo na kipekee tutaongeza nguvu katika kukuza utalii katika nchi yetu’’ - Dkt. Hussein Mwinyi.

"Niwapeni vionjo tu vya mambo ambayo yanakuja, wenyewe mnajua yajayo yanafurahisha nawaombeni mjitokeze kwa wingi siku ya uchaguzi tukapige kura kwa wingi kwa wagombea wa CCM ili tuendelee kuleta maendeleo’’ - Dkt. Hussein Mwinyi

FUATILIA MATANGAZO MUBASHARA KUPITIA LINK HII;
IMG-20200912-WA0039.jpg
IMG-20200912-WA0031.jpg
IMG-20200912-WA0028.jpg
IMG-20200912-WA0030.jpg
IMG-20200912-WA0026.jpg
IMG-20200912-WA0045.jpg
IMG-20200912-WA0043.jpg
IMG-20200912-WA0044.jpg
IMG-20200912-WA0046.jpg
IMG-20200912-WA0036.jpg
IMG-20200912-WA0040.jpg
IMG-20200912-WA0023.jpg
IMG-20200912-WA0048.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom