Uchaguzi tumeuona, CCM tumewasikia, CHADEMA tumewasikia. Watanzania wanasemaje?

Hii ni aibu yetu sote! Mawaziri, ccm kama chama, bunge, viongozi wa dini, wananchi wote, wazee, mahakama, kwamba tumeshindwa kumdhibiti rais wetu na slowslow wafuate katiba na sheria za nchi? :) :) :)!
Tanzania iliyokuwa mfano katika Africa, tulikuwa tunakaribia Ghana kwa kufuata misingi ya democrasia!
Sasa hivi Ghana imetuacha kwa mbali kwa democrasia na haki za binadamu na pia kwa uchumi kwani wWekezaji wengi wanakimbilia Ghana na Kenya kwa sasa.
Tofauti na zamani taifa letu limesogelea South Sudan na Somalia!
Ninauliza ccm wanapata faida gani kwa hili! Ccm wanadhani anayepata aibu ni upinzani ama wao wenyewe?
Kwa chaguzi hizi hata mtoto wa miaka mitatu anatambua kuwa ni uozo!
Kama watu 500 wamejiandikisha kwenye kituo, wakapiga kura 50 tu wewe hata kama hujasoma au ni mjinga unapata picha gani???????? :) :) :) :)
Kweli unaweza kusema kuwa watu wako wanakupenda???
Tujitafakari kama serikali. Soon tutakuwa isolated from the world!
Tutashindwa kuaminika!
Tutadharaulika!
Tutaaibika au tayari tumekwisha kuaibika!
Tutarudi miaka 50 nyuma afadhali ya ukoloni!
SA Malema tu anatosha ; Uganda Bob Wine ameanza kutosha; yote kwa sababu mahakama, speaker na wananchi wakonyuma yao!
Tafakari! Tafakari! Tafakari sana!! :) :) :) :) :)
 
Ukiangalia mtiririko wa matukio katika uwanja wa Siasa za Tanzania, utaona kwa upande mmoja yuko Rais Magufuli, ambaye ana CCM, Serikali (Wizara, wakuu wa mikoa na wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, Ofisi ya Taifa ya Takwimu,COSTECH, nk) Majeshi ya ulinzi na Usalama, Bunge, sehemu ya Mahakama (Mahakama ni mhilimili unaojitegemea kwa hakika, lakini inaonekana kuna baadhi ya mahakimu wanaonesha kuwa tayari kutumika), Tume ya uchaguzi, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, RITA (wanaosajili bodi za wadhamini wa vyama vya siasa), baadhi ya vyama vya "upinzani" kama TLP, UDP, nk, pamoja na wapambe na wadau kadhaa wengine.

Ukiangalia upande wa pili kuna vyama vya Upinzani, vyenye upinzani kwa CCM, vyama hivyo ni CHADEMA, CUF-Maalim, ACT, NCCR-Mageuzi, UKAWA, Pia kuna taasisi kadhaa ambazo zinaonesha kuwa na msuli wa kuikosoa serikali ya JPM, kama Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC),kuna wengine huko nyuma walisikika, siku hizi siwasikii sana, mfano Haki Elimu, Mtandao wa Jinsia, JUKATA.

Tokea Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, imejionesha kuwa na mtindo wa pekee wa utendaji ukilinganisha na awamu zingine zilizotangulia, japo zote ziko chini ya chama kile kile cha CCM. Wakati upinzani wakianza awam hii, walikua wakitafakari jinsi walivyoongeza uwepo wao bungeni na kwenye Halmashauri, kwamba kama waliweza kufanya yale waliyofanya kipindi cha 2010 - 2015, sembuse sasa hivi wako wengi hivi? Lakini hawakuwa hata na wazo kwamba watajikuta katika hali ngumu namna hii.

Awamu hii ilianza kwa kupiga marufuku mikutano na maandamano, yaani shughuli zote za kisiasa za vyama vya upinzani. mwanzoni mikutano ya ndani iliachwa iendelee, maana sababu iliyotolewa ni kwamba "Uchaguzi umekwisha, tuache siasa tuwatumikie wananchi" kwa hiyo mikutano ya ndani haikuingilia utendaji wa serikali kuwahudumia wananchi. Lakini inaonekana lengo lilikuwa tofauti kabisa. maana baadaye hata mikutano ya ndani imezuliliwa, hivi hata mkusanyiko wa wapinzani katika msiba, unasambaratishwa kwa nguvu kubwa. Hapa lengo ni KUUWA UPINZANI.

Sambamba na hilo la kupiga marufuku shughuli za vyama vya siasa, na hasa kwa lengo la kuua upinzani, ilichukuliwa hatua nyingine kubwa ya kupiga marufuku BUNGE LIVE. Ilionekana kwamba hilo lilikuwa eneo kubwa la wapinzani kujidai na kujipatia umaarufu. pia ilionekana ule utaratibu wa kuwapatia wapinzani zile kamati za kuisimamia serikali, unawapa wapinzani mwanya wa kufurukuta, nako walibanwa. huko bungeni hatua zilizidi kupamba moto baada ya kuja mkakati wa kuratibu hotuba za kambi rasmi ya upinzani bungeni.

Baada ya hapo likaja suala la chaguzi za marudio, ambazo zimegeuka kuwa kiini macho. kila wapinzani wanapojipanga, serikali kwa kutumia vyombo vyote ilivyonavyo, bila aibu, bila kuficha, mchana kweupe, inafanya kila linalowezekana ili kuhakikisha CCM inashinda kwa gharama zozote. Tokea alyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, alipoomba radhi kwa JPM pale ilipotokea upinzani walipata ushindi katika kata moja, hakuna mkurugenzi, mkuu wa Wilaya, wala mkuu wa Mkoa, ambaye yuko tayari kuruhusu wapinzani washinde hata kata moja. sasa hivi ushindi ni asilimia 100 kwa CCM.

Tumemsikia Mbowe akitoa tathmini ya uchaguzi mdogo wa hivi karibuni. Tumewasikia CCM wakitoa kauli yao. wapo wanaokuabliana na Mbowe, na wapo wanaompinga. Lakini ukiangalia jinsi mazungumzo yanavyokwenda, inaonekana huu ni mtanange kati ya JPM na CCM yake na Serikali yake, kwa upande mmoja, na Vyama vya upinzani kwa upande mwingine. na inaonekana kwamba kukwama kwa vyama vya upinzani ni hasara kwao wenyewe. watu wanatoa maneno ya kejeli mfano "kususa ni tabia za kike", (Tusisahau wanawake ni mama zetu, ndio wanaotuzaa). Lakini je, ni kweli kwamba hili ni tatizo kwa wapinzani tu?

Mimi nadhani tatizo ni kwa Tanzania kama taifa. wapo walioonesha kusikitishwa na kudorora kwa upinzani kama mfumo katika Taifa letu. Hili ni tatizo kubwa ambalo ukubwa wake utakuja kujulikana hapo baadaye. Ni jukumu la watanzania wote, siyo Mbowe na wenzake peke yao, kulinda mfumo huu wa vyama vingi, wa kuwa na mawazo mbadala katika mfumo wetu wa utendaji. Tunawahitaji sana watu ambao wana jukumu la kuangalia kila mipango yetu, katika mtazamo tofauti na kutoa hoja zitakazo tusaidia. kama hawafanyi hivyo, siyo kosa lao peke yao, bali ni kosa la jamii nzima.

Hivi badala ya kutafuta namna ya kuwakosoa, kwamba kila mara tuwaulize mnafanyaje hapa, jamii ya watanzania ijione kwamba inahusika na mustakabali huu, tuoneshe kuwaunga mkono, hata kwa maneno tu. lakini pia kila mahali tulipo, watanzania waanze kuongea kuhusu mustakabali wao, na kujiuliza maswali magumu na kutafuta majibu yake katika sehemu walipo. kwamba hapa kwetu tufanye nini kudhibiti hali hii?
Kila nisomapo maoni ya mashabiki wa ccm na viongozi wao huwa nashindwa kuelewa kama wana akili timamu.
Hivi hawajifunzi kwa nchi jirani yanayojili/yaliyojili kama Burundi/Rwanda,Uganda au DRC-Congo?
Watawala ni mbegu iliyolaaniwa sana.
 
Waendesha vyama vya siasa,Vya upinzani wameishiwa maarifa, ispokua hawataki kuachia wengine gurudumu, kisa urafi Wa ruzuku, acha upinzani upwaye tu
Hoja hapa ni kwamba kama tutafika mahali hatuna vyama vya upinzani vyenye meno, nchi yetu itakuwa ya aina gani? kuanzia 2000, CHADEMA wamekuwa wakiongeza wingi wao katika madiwani na wabunge. na hata utendaji wa Magufuli ni matokeo ya kampeni kali zilizopigwa na vyama vya upinzani huko nyuma. ilifikia mahali Magufuli akaita M4C kuwa ni MAGUFULI FOR CHANGE wakati wa kampeni yake. kwa hiyo hatuwezi kuwapuuza moja kwa moja wapinzani.
 
Chukueni lenu uhko! tallest wewe siku zote ni ccm leo kwenye kushauri Mbowe aondoke ndiyo huna chama! Acha kutudanganya hapa. Mbowe! Mbowe! Mbowe! Mlitaka awe kama propesa? Haondoki Ngo! Wajinga wanaliia ruzuku wakidhani 200m/mwezi ni nyingi sana kendesha chama! Maskini wenzangu ambao hawajawahi kuona m na wala hawajawahi kuendesha hata kijiji kimoja siyo watu 6m.sasa mufunge midoo yenu!
 
Kama Unategemea Mnazi Mmoja Ndiyo Uwaze Kupanga Uzazi Na Wavivu Hata Wakati Mwingine Kuzaa Ni Shida
Zaeni


Maendeleo Hayana Chama
 
Back
Top Bottom