Uchaguzi serikali za mitaa Babati Mjini, CHADEMA yaidondosha CCM. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi serikali za mitaa Babati Mjini, CHADEMA yaidondosha CCM.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dullo, Mar 28, 2011.

 1. Dullo

  Dullo JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 24, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uchaguzi wa wenyeviti wa mitaa na vitongoji katika jimbo la babati
  mjini umemalizika huku chama cha demokrasia na maendeleo (chadema)
  kikiibuka mshindi kwa kuongoza mtaa mmoja na vitongozi viwili na
  chama cha mapinduzi ccm kikiongoza vitogoji viwili.

  Chama cha chadema kimeshinda mtaa wa ngarenaro, na vitongoji vya
  mutuka na soraa huku ccm kikiambulia vitongoji vya nakwa na maisaa
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  FALSAFA NZURI YA CHAMA CHA SIASA NI SHARTI IAKISI JAMII HUSIKA NA
  UHALISIA WA MATUMAINI / NDOTO ZAO, MAZINGIRA WANAMOISHI,
  URAHISI KUKUMBUKIKA / KUELEWEKA KWA FALSAFA YENYEWE NA YENYE KUENDANA VILIVYO NA KIPINDI KATIKA MAISHA WANAMOISHI

  Nitangulie kuwapa hongera sana sana tena sana CHADEMA kwa kuweza kuibuka na falsafa ambayo kiujumla ni sura halisi ya matakwa ya Wa-Tanzania na safari yetu ndefu kama jamii moja katika maisha haya.

  Hakika kwa ufahamu wangu falsafa ya CDM imekidhi misingi yote muhimu kiasi cha kutosha kututambulishia kwamba CHADEMA ni watu gani katika jamii yetu, wanaamini katika lipi na siku zote tuwafanyie tathmini katika uendeshaji wa shughuli za kila siku katika taifa hili huku wananchi tukizingatia misingi gani hasa zinazotambulika rasmi.

  Ndio, Falsafa ya Chama Cha Siasa si sawa na mtu kufanya ziara binafsi kwenye mbuga za wanyama kokote duniani. Wala Jambo hili halipigiwi KOFULI MLANGONI kwamba haukua nalo jana leo hii ukitangaza kuwa nalo basi ni kosa la jinai - laa hasha!! Hivyo mtu kusema kwamba labda kwa kuwa Mwenyekiti Mstaafu, Mhe Edwin Mtei, katika mahojiano yake na vyombo vya habari pengine miaka 5 iliyopita hakulitaja falsafa ya Chama; hiyo peke yake hakizuii chama kuweza kupiga hatua zaidi kwa KUJIPA SURA HALISIA kisiasa nchini.

  Kiukweli, kupokezana kule kete la majukumu ndani ya Chama na hiyo ndio maana tunasema CHADEMA ni cha Wa-Tanzania wote na wala si mali ya mtu binafsi kama vilivyo vyama vingine vya mifukoni hapa nchini hivyo kama Mzee Mtei aliweza kutekeleza hatua fulani muhimu kwa uhai wa chama hiki basi nasisi Vijana Wa-Tanzania wenye mali yao tunaendelea kukamilisha mengine na mengi zaidi mazuri bado yako njiani yanakuja - kaeni mkao wa ushindi kote nchini!!

  Nielewavyo mimi, falsafa ya Chama Cha Siasa kwa maelezo miepesi ni UJUMLA WA MAWAZO NA FIKRA yanayotafuta kumtambulisha mtu na au Chama na kile anachokiamini, kupenda kuliona likitendeka kwa jamii yake na kwamba yuko tayari kuwekeza muda na rasilmali nyinginezo muhimu kuendeleza fikra na mawazo hayo kwa faida na maendeleo ya jamii katika ujumla wake.

  le majibu ya maswali ya msingi kama vile; (1) nyinyi kama Chama cha siasa wananchi tuwatambueni kuwa muu akina nani hasa?? (2) mnaamini katika mambo yepi hasa ambayo lasimamia ambayo ndiyo itakayokua ni chimbuko na muongozo wa shughuli zenu zote kiutendaji kama chama.

  Na kwa mantiki hii ndipo nako tunapotangaza kwamba ni mwisho wa SIASA ZA MKUMBO huku tukifungua ukurasa mpya wa siasa za kisasa zenye kuegemea misingi ya wazi na iliotukuka mioyoni mwa Wa-Tanzania tuliowengi.

  Hadi hapo nawashauri vijana wenzangu kote nchini na wananchi kwa ujumla kwamba maadam sote tumeshajionea madhara makubwa yalioletwa na falsafa mpya ya Chama fulani nchini; falsafa ya 'Kasi Mpya, Nguvu Mpya na Ari Mpya' pasipo kuelewa hasa dira zima ya wapi tunakopelekwa kama taifa, na hatimaye kutokea ajali ya mwaka kisiasa ambapo chama hicho hivi sasa kimeparaganyika vipande 200 kidogo, ni muda muafaka sote tukajiunga CHADEMA leo hii na wala si kesho.

  Hakika CHADEMA pekee ndiyo nyumba salama kisiasa kwa watu wa rika zote, dini zote, rangi zote, jinsia zote na daraja zote za uelewa sawa na vile ambayo hata Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliiona na kutuambia kwa kinywa kipana sote nchini.
   
 3. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kazi nzuri, CDM SASA WAJIPANGE KWA CHAGUZI ZIJAZO!
   
 4. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  kilichofanyika babati kizuri sana. people are starting to emancipate themselves from mentally slavery. nawashauri cdm waendelee vjijin humo wa kitangaza sera na kuwafungua wananchi kutoka minyororo ya ccm. wale vjana wa songea waliowasha taa mchana maendeleo yao vp? mwenye latest updates anijuze tafadhali
   
 5. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Imekuwaje tena CCM kupata viwili. Bado kidogo hawatapata kabisa:drum:
   
 6. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,509
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Sijakuelewa. Kwa hiyo matokeo ya mwisho bado??
   
 7. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  nafikiri taa iliwashwa songea ingetuika na kukanadaliwa utaratibu ikazunguka nchi nzima mithili ya mwenge wa uhuru lakini kwa malengo ya kuwamulikia watanzania ukweli wa nchi yao na kuwaunganisha vijana katika vijiji vyote. Ni nema viongozi wa kitaifa wakaratibu mwenendo wake na viongozi wa kila mkoa/wilaya kujipanga vema kuhakikisha taa hiyo inazunguka vijijini "at lwast" kila kata.
   
 8. m

  mzambia JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Hongereni sana chadema ila msibweteke
   
 9. m

  mzambia JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Msibweteke chadema
   
 10. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,207
  Trophy Points: 280
  Kitu gani hakieleweki Mr. Zero.
   
Loading...