Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,092
- 43,265
Katika nchi ya kidemokrasia uchaguzi unafanyika kwa sababu mbili kubwa.
Kwanza, ni kwa ajili ya wananchi kupima na kutoa hukumu juu ya yale yaliyofanywa katika kipindi kilichopita. Wale wanaomaliza muda wao waliingia na ahadi kadha wa kadha. Je, wametimiza ahadi hizo kwa kiasi gani? Je, wapewe muda mwingine wa kumalizia zile ambazo hazikutimizwa? Je, wanastahili Kuelewa nafasi nyingine?
Hivyo, wananchi wanapewa nafasi ya kufanya uamuzi juu ya uongozi na utawala wa maeneo yao. Endapo wananchi wanakubali na kuridhishwa na kilichofanywa basi watawarudisha viongozi waliopita. Na kama ni la, basi watawaingiza madarakani viongozi wengine.
Sababu ya pili ya kufanya uchaguzi katika nchi ya kidemokrasia inatokana na sababu ya kwanza. Nayo ni kutoa hukumu ya kisiasa juu ya chama tawala. Chama kilichopo madarakani kinaweza kudhania kuwa kinastahili kuwepo madarakani. Hata hivyo ni wananchi ndio wanatakiwa kutoa hukumu hiyo kila baada ya muda fulani, kwa Tanzania ni kila baada ya miaka mitano, kwa Marekani ni kila baada ya miaka minne kwa Urais, miaka miwili kwa wawakilishi na sita kwa maseneta.
Lengo la hili la pili ni kutoa nafasi kwa chama kingine kuja na mwelekeo tofauti na ule wa chama tawala na kuwapa wananchi viongozi wapya nje ya wale wanaomaliza muda wao kutoka chama tawala.
Katika kuhakikisha sababu hizi mbili zinafanikiwa, nchi zenye demokrasia iliyokomaa zimefanya mambo makubwa kadhaa:
1. Kutengeneza na kusimika mfumo wa uchaguzi unaoweka uwezekano wa aliyeko madarakani (incumbent) kushindwa. Mfumo, unahakikisha aliyeko madarakani anaweza kushinda au kushindwa bila dhulma, hadaa, au matumizi ya njia za mkato.
2. Walioko madarakani hawaogopi au kuhofia wapinzani wao walio nje. Kama wanaongoza vizuri na wanatimiza ilani yao, hawahitaji virungu au vurugu kujitangaza. Kazi zao zinajionesha na mafanikio yao yanajipigia panda yenyewe.
3. Ili kuhakikisha kila mtu yuko sawa, nauli zozote au maagizo yoyote yenye kuashiria kutokujiamini au yenye kutaka kuvuruga mfumo wa uchaguzi yatapingwa na kukataliwa. Ukimpa mtu nafasi ya kuchagua vitu vitatu halafu ukamwekea bastola kichwani na kumwambia achague cha kwanza basi kinachofanyika siyo uchaguzi bali uchafuzi wa kidemokrasia! Hakuna uchaguzi mbele ya shurti! Huwezi kuwa huru kuchagua kama familia, mtaa, jamii yako inashikiliwa mateka.
Ni kwa sababu hiyo naamini ukuu wa dhamira na ukweli (the supremacy of conscience and truth) unamtaka mtu kuamua kama anaitaka kushiriki katika uchaguzi au uchafuzi wa kidemokrasia. He, mtu ajiandikishe kupigika kura wakati chama chake hakiko huru kufanya shughuli same za kisiasa? Je, ashikiri huku akijua wasimamizi wamekatazwa kumtangaza mshindi kama akiwa wa chama chá upinzani? Je, ashiriki uchaguzi huku akijua muda yake haitahesabiwa?
Basi katika nchi ya kidemokrasia Ni muhimu sana kuhakikisha kuwa kinachofanyika ni uchaguzi na siyo uchafuzi, na mfumo ni wa demokrasia na siyo demoghasia na kuwa mwisho wa siku watawala hawageuki kuwa watuwala.