Uchaguzi ndani ya CHADEMA lini?

Uchaguzi ndani ya CHADEMA lini?

ni vizuri kutaka kujua juu ya suala hili muhimu katika kutimiza demokrasia ndani ya chama.lakini pia usisahaua kuwa kuna mambo ambayo ni mipango ya ndani ya chama.kwa mfano suala la uchaguzi ndani ya chadema kikatiba linapaswa kuwa mwaka 2014 lakini chama kikaamua kwamba ni muhimu uchaguzi ufanyike mwaka 2013 ili kujiandaa na uchaguzi wa seuikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka 2015.kwa hiyo chama kina fursa ya kutafakari kwaa mazingira ya sasa pamoja na mchakato wa katiba mpya ambayo ni muhimu kuliko mambo yote kwa sasa itakuwaje?kwa kifupi chama kikifanya uchaguzi mwaka huu au mwakano hakuna kosa la kikatiba ilimradi tu maamuzi yote yatie kwenye vikao na kupata Baraka za wajumbe wa vikao husika.
wana jf
mwanzoni mwa mwaka huu kulikuwa na tetesi kwamba uchaguzi wa ndani wa viongozi wa chadema utafanyika kuanzia mwezi wa nne 2013, cha ajabu hivi sasa ni mwisho wa june lakini kimya na hakuna kinachoendelea.

Demokrasia iko wapi ndani ya chadema??? kuna rafiki yangu nlikuwa naongea naye kuhusu hili akasema uchaguzi wa nini wakati viongozi wapo?? je hilo jibu ni sahihi kwamba mfumo wa kifalme umerudi Tanzania? Tumezoea kumsikia Augostino Lyatonga Mrema akiwa mwenyekiti wa TLP tangu ahamie chama hicho miaka zaidi ya 15, John cheyo wa UDP na Prof Lipumba ni mwenyekiti wa kudumu wa CUF.

Je hivi vyama ni wale wale??
 
ni vizuri kutaka kujua juu ya suala hili muhimu katika kutimiza demokrasia ndani ya chama.lakini pia usisahaua kuwa kuna mambo ambayo ni mipango ya ndani ya chama.kwa mfano suala la uchaguzi ndani ya chadema kikatiba linapaswa kuwa mwaka 2014 lakini chama kikaamua kwamba ni muhimu uchaguzi ufanyike mwaka 2013 ili kujiandaa na uchaguzi wa seuikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka 2015.kwa hiyo chama kina fursa ya kutafakari kwaa mazingira ya sasa pamoja na mchakato wa katiba mpya ambayo ni muhimu kuliko mambo yote kwa sasa itakuwaje?kwa kifupi chama kikifanya uchaguzi mwaka huu au mwakano hakuna kosa la kikatiba ilimradi tu maamuzi yote yatie kwenye vikao na kupata Baraka za wajumbe wa vikao husika.
ok, ahsante kwa maelezo yako mazuri sasa tueleze UCHAGUZI CHADEMA NI LINI?

  • Thanks
Reactions: kdc
hii demokrasia tunayoizungumzia chadema ipo wapi.?ndio kusema muda umebana hadi uchaguzi usifanyike? Hapo tu ninapoamini siasa mchezo mchafu wa kucheza na akili za watu.
 
mpaka Nyerere wa CHADEMA(mzee Mtei) atake ndiyo uchaguzi utafanyika.
 
Mbona uchaguzi unaendelea hadi sasa,kwa mfano ktk jimbo la Njombe Kaskazini ngazi ya misingi na matawi tumeshamaliza na kuanzia tarehe 27/09/2013 tunaanza ngazi ya kata na majimbo,kumbuka hizi ngazi za chini za chama zinasimamiwa na kanda na ratiba zinatofautiana kila kanda ,lkn uchaguzi unaendelea sehemu mbalimbali .haya swali lingine
 
Nafikiri ndugu yangu kama ni mwanachama hai na unakadi ya chama utakuwa unajua uchaguzi nilini! Nataka nikwambie na nikutahadhalishe! Husiwaamishe WATANZANIA kwenye mada ya KATIBA MPYA! Nakuwapeleka kwenye mada nyingine,najua nyie ni watoto wa Lumimba mnatumwa na Nape mnyauye!

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Mbona uchaguzi unaendelea hadi sasa,kwa mfano ktk jimbo la njombe kaskazini ngazi ya misingi na matawi tumeshamaliza na kuanzia tarehe 27/09/2013 tunaanza ngazi ya kata na majimbo,kumbuka hizi ngazi za chini za chama zinasimamiwa na kanda na ratiba zinatofautiana kila kanda ,lkn uchaguzi unaendelea sehemu mbalimbali .haya swali lingine
Hii kweli NGO.kwa hiyo kila kanda ikiamua kufanya inajifanyia tu, wengine septemba,octoba, novemba,mwakani? 2015? hakuna mpangilio?
 
Hapo itakuwa hakuna tofauti na matawi ya timu za mpira ya Simba na Yanga ya "mpira pesa" "ubungo terminal" wakiamua tu wanafanya uchaguzi hajui Rage wala Manji.

ni chama cha kifalme hakuna uchaguzi by the way hakuna mtu mwingine chadema mwenye uwezo wa uongozi .

Alitegemewa zito but naye ni kirusi ndani ya chadema.
wacha umbulula, chukua historia ya ccm iliongozwa na mtu mmoja kwa miaka mingapi? :A S angry:
 
uchaguz wa nn? hawa waliopo wanafaa au mnataka kutupandikizia mamiluki wenu kina shibuda
 
Mkuu maneno yale yalimlenga zitto zuberi kabwe kweli zitto hafahamikimndani ya chadema au kunani chadema.

Zitto hatoshi kwenye nafasi zaidi ya aliyonayo kwa sasa CHADEMA

Ili uweze kuwa kiongozi wa juu wa CHADEMA unapaswa uwe muumini kindakindaki wa sera na misimamo ya za chadema

CHADEMA hatutaki kuongozwa na mtu ambaye baadaye atakuja kukisumbua chama na kuvuruga muelekeo wake eti kisa Demokrasia

CHADEMA tumefukuza baadhi ya wanachama na viongozi kwa kukiuka misingi na taratibu za CHADEMA, CHADEMA hatuko tayari kuingia kwenye mgogoro wa kiuongozi Taifa eti kuwaridhisha CCM wanaotaka uongozi ubadilike ili uje wakununulika

Sisemi Zitto ananunulika, ila nataka kusema inapaswa awe muumini wa CHADEMA kindakindaki na ajiepushe na vikao vya mara kwa mara na watu wa CCM kwani vinamuondolea imani mbele ya wanachama na wapenzi wa CHADEMA

Freeman Mbowe na Dr W. Slaa, ni kiini cha uchangamfu na kukubalika kwa CHADEMA, hao wanaoulizia uchaguzi wanapaswa waseme wamechukizwa na nini na viongozi hawa?

Dua zao ni sawa na dua za mchawi anayeomba usiku uwahi kufika ili aje kukujambia,

Usiku mwema rafiki

Joash Mussa
CHADEMA member
 
Mkuu maneno yale yalimlenga zitto zuberi kabwe kweli zitto hafahamikimndani ya chadema au kunani chadema.

dogo kwani ww CHADEMA inakuhusuje wakati wewe uko na elephant dentist?nyie kauzen malignant cabbanco,na comelina bigalensis...uku cdm tuachie wahusika..
 
Appriciator na Watanzania,
Nimefuatilia mjadala kwa ujumla. Kwa manufaa ya wengi naomba nitoe taarifa ifuatayo:
1. Awali narudia kauli niliyotoa na imetolewa Mara nyingi na viongozi wa Chadema kuwa ndani ya Chadema hakuna mwenye hati miliki ya Chama, na hivyo maamuzi ya Chadema, kwa mambo yanayohusu chama au nje ya Chama hufanywa kufuata Katiba ya Chama, Kanuni ya Chama na au maazimio ya vikao vya maamuzi yaani Kamati Kuu, Baraza Kuu na Mkutano Mkuu.
2. Tumekwishasema kutangaza Mara kadhaa kwenye Press Conference mbalimbali baada ya vikao hivyo, kuwa Chadema imeamua kutekeleza sera yake ya Kanda/Majimbo ndani ya Chama wakati inajiandaa kutekeleza sera hiyo katika muundo wa utawala wa Taifa letu wakati utakapofika. kanda 8 za Bara zimekwisha kuundwa, na Kanda 2 za Zanzibar zinasubiri kuundwa baada ya kujua mwelekeo wa Katiba Mpya. chaguzi za viongozi wa Kanda zilikamilika mwezi Augusti, 2013. Uundwaji huo wa Kanda ambao ulisimamiwa katika Kanda zote na Mhe. Freeman Mbowe ulisimamiwa na Freeman Mbowe(MP), Mwenyekiti wa Chama na uchaguzi wa Viongozi wa kisiasa umefanyika katika ngazi zote. Hatua inayoendelea kukamilika sasa ni uteuzi wa viongozi watendaji yaani Mratibu wa Kanda na Afisa wa Kanda na viongozi wasaidizi. Nafasi hizo zote zimetangazwa kwenye vyombo vya habari na kwenye maeneo yote ya Kanda husika. Ofisi ya Katibu Mkuu imekwisha kuletewa mapendekezo mbalimbali kwa uteuzi wa mwisho, na kazi hii inategemewa kukamilika kufuatana na speed ya kila kanda kukamilisha taratibu zilizo chini ya mamlaka yake.
3. Nilikwisha kutangaza Mara kadhaa, lakini nafafanua ten a kwa manufaa ya watanzania wengi wanaoweza kukwazwa na upotoshwaji unaoendelea.
a) Tulipanga kutoa mafunzo ya kina kuanzia ngazi ya Taifa, Kanda, majimbo na Kata kwa viongozi wetu wapatao 36,000 watakaokuwa injini ya kujenga na kuimarisha mtandao wa chama kwa nchi nzima. Nilitoa Taarifa kuwa kaxini ya wakufunzi hao ni kuunda timu za kufungua misingi ya Chadema ( kwa ccm ni Mashina) ipatayo 250,000 nchi nzima yaani kuwa na msingi wa Chadema kwa kila shina la ccm. Aidha baada ya kutoka kwenye misingi watafanya kazi hiyo pia kuunda na au kuimarisha pale ambapo tayari kuna matawi. Lengo ni kuwa na matawi 18,000 kwa nchi nzima. Yaani kuwa na tawi kila palipo na tawi la ccm, ili tubanane huko huko vijijini. Kazi ya mafunzo ikifanyika kwa ufanisi, na sasa kazi iliyoko ni kufungua misingi na matawi, kaki ambayo kwa formation iliyoko inategemewa kukamilika mwezi wa October. Ni kweli kazi hii imechelewa kwa mwezi mmoja kutokana na mwingiliano wa shughuli mathalan uchaguzi mdogo wa madiwani, zoezi la ukusanyaji wa maoni ya Katiba, mambo ambayo chadema hatuna mamlaka ya ratiba yake.
C) Baada ya kuunda misingi na matawi uundaji na uchaguzi katika ngazi ya kata, majimbo wilaya hadi Taifa itafuata, na ngazi hizo hazina kazi kubwa Kama ngazi ya msingi na matawi kwa vile zina idadi kubwa, lakini pia indigo walk wanachama. Ngazi ya kata kwenda juu ni ngazi za uongozi tu, na wanaohusika kwenye ngazi hizo ni viongozi hivyo kaki inakuwa rahisi zaidi.

Hivyo, watanzania muelewe kuwa Chadema ni chama makini, inafanya kaki zake kisayansi siyo kwa propaganda. Huwezi kuzungumzia uchaguzi bila kufanya kazi ya kujenga chama. Wengi hawajui uzito wa kazi hiyo, kumbukeni Mwl. Nyerere Aliwahi kujiuzulu ili avenge mtandao wa Tanu. Ndipo baada ya kukamilisha kaki hiyo akarudi kuwa Raisi wa kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika. Uchaguzi unafanyika baada ya kuwa na chama imara. Ndiyo kazi inayofanyika, na ninawapongeza wale makamanda wote wanaofanya kaki hiyo katika mazingira magumu sana. Nina hakika wote hao wataingia katika historia ya ukombozi wa pili wa Taifa letu.

Ni Imani yangu kuwa baada ya ufafanuzi huu watakaopenda kubishana na kufanya propaganda ni juu Yao. Mwenye kutaka kupokea elimu hii naomba aeleze na kwa wengine pia ili kuwasaidia. Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Chadema.

Ni jambo la kujiuliza mkuu iwapo kila siku tunapiga kelele

juu ya katiba na demokrasia kisha kwenye vyama hatufanyi uchaguzi tunaonyesha picha gani kwa wananchi? kama kweli tunataka kuonyesha njia ni vizuri uchaguzi ukafanyika.

If this can be done soon, hopping to cover the gap that exists in villges...we need to that happening Dr Slaa!
 
Back
Top Bottom