munirah
JF-Expert Member
- Mar 13, 2015
- 551
- 224
Wanajamvi
Kwanza poleni na hekaheka za uchaguzi mkuu 2015 (UM) ambapo kwa sisi ambao tulikuwa hatujui maana ya siasa za ushindani tunaishia kujifunza mambo mengi sana kipindi hiki!
Niwapongeze walioteuliwa kuwakilisha vyama vyao kwa nafasi mbali mbali ambapo naamini wanatekeleza wajibu wao kama raia wema wa nchi yao kama katiba yetu inavyoruhusu!
Baada ya hayo niwe mkweli na muwazi kuwa mada yangu italenga uchaguzi mkuu 2015 hasa kiti cha rais na hatma ya Tanzania mpya yenye mabadiliko ya kimaendeleo kwa nyanja mbalimbali!.
Tunashuhudia mengi kupitia UM huu lakini katika kupitia nyuzi nyingi humu sijaona hata moja inayogusia hatma ya watumisi wa umma waandamizi katika kada mbalimbali zikiwemo Usalama wa taifa Majeshi ya ulinzi na usalama Wakuu wa vyuo vikuu watumishi wa wizara zote Wakuu wa Mikoa na wilaya na Watumishi wengine mbalimbali ambao walikuwa wakitekeleza wajibu wao kwa mwavuli wa Chama Tawala!
Wazungu wanasema ''Changes are inevitable'' na maana ya kuwa na demokrasia ya vyama vingi ni kuamini kuwa vyama mbalimbali vitashiriki UM kusimamisha wagombea watakaoungwa mkono na wananchi ili kuwaongoza kwa vipindi tofauti tofauti! kama ambavyo maana halisi ya demokrasia inavyojipambanua kwa ufasaha!
Ikiwa mabadiliko katika nchi ni jambo la lazima! Je kwa jicho la Tanzania mpya.....ni ipi hatma ya watumishi hawa ikiwa kutatokea mabadiliko? Huu ni wakati wa mashaka kwa watumishi wa umma ambao wanajihisi au wanatajwa kama watu wabovu kusimamia taasisi mbalimbali za serikali kwa makusudi ama kwa kutekelea amri ya watawala! Je kipi kitatokea iwapo mabadiliko yatatokea pia?
NB: Mimi siko upande wowote but neutral kwa mustakabali mpana wa Taifa! hivyo tujadili kwa nidhamu kabisa tafadhali.