Muhammad Buhari alichukua madaraka katika mapinduzi yaliyomuondoa Raisi Shehu Shagari.
Sidhani kama kuna Raisi wa Nigeria aliyepambana na rushwa kama Gen.Muhammad Buhari.
Tukio ambalo sitalisahau ni jaribio la serikali ya Buhari kumteka nyara Umaru Dikko ambaye alikuwa waziri wa petroli au nishati katika serikali ya Shehu Shagari.
Umaru Dikko alikimbilia mafichoni Uingereza. Sasa Gen.Buhari akaamua kukodi majasusi ambao walimteka nyara Dikko, wakamdunga madawa ya usingizi, na kumpakia kwenye mzigo wa serikali wenye hadhi ya kidiplomasia.
Kwa bahati mbaya majasusi wa Scotland Yard wakashtukia "mchezo", wakapuuza mikataba ya kimataifa na kidiplomasia na kulazimisha mzigo[diplomatic bag] huo ufunguliwe katika uwanja wa ndege kabla haujapakiwa kwenye ndege kuelekea Nigeria.
Ndani ya sanduku hilo akapatikana Umaru Dikko na jasusi lililokuwa likimuongezea dawa ya usingizi!! Tukio hilo lilizusha mgogoro mkubwa wa kidiplomasia kati ya Nigeria na Uingereza.
Pamoja na jitihada hizo, Gen.Buhari naye hakudumu ktk nafasi hiyo kwani alipinduliwa na Gen.Ibrahim Babangida.
Sasa hivi Buhari yuko katika harakati kurudi madarakani kupitia sanduku la kura.
cc Mwawado, Mag3, Pasco, Jasusi, Ben Saanane, Sangarara, Nguruvi3, EMT, Kimweri, Kobello, Mwigulu Nchemba, Dr.W.Slaa, Zitto, Mzee Mwanakijiji, NasDaz