Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,997
- 1,163
mambo ya ngoswe!............................................
Waridi,
tunazungumzia nafasi ya mwenyekiti wa taifa wa chama cha siasa cha NCCR, nafasi ambayo ni kubwa na nyeti.Itawezekana vipi mtu asiyefahamika kabisa katika ulingo wa siasa, tena siasa zenyewe hizi za bongo aweze kumwangusha mwenyekiti anayetetea nafasi yake?manake usisahau kuwa wapiga kura ni watanzania hawa tunaowajua.Kama kweli ni wengi hatumjui huyo bura hata hao wapiga kura wa NCCR hapana shaka watakuwa hawamjui, sasa watawezaje kumpa uenyekiti mtu wasiyemfahamu?Je alishawahi kuwa kiongozi wa kisiasa kwenye ngazi yoyote,kama una ufahamu wowote juu ya hili nisaidie.
Hiyo competence unayoizungumzia inawezaje kuthibitishwa?nani atakayeithibitisha?
au unazungumzia competence kwa upande wa kitaaluma au mi sijakuelewa?hebu nisaidie kuifahamu hiyo competence unayoizungumzia.
Ngoja nifuatilie nione kama nitapata CV yake/zao nikuleteeni.
Mimi sioni tatizo katika upya wa Bula, badala yake naona ishara njema kwani mtu mpya kajitokeza na kwa mantiki hiyo huenda ana jipya.
Kwa taarifa nilizo nazo Bula ni candidate anayetokea upcountry, ni changamoto hasa kwa Mbatia ambaye 'katokea' Uholanzi kuja kutetea kiti chake.
Nani kamuweka nani hapo sijui na sidhani. kila mmoja wao kajaza fomu kwa wakati wake.
Waridi,
Nitashukuru kama utaturushia CV fupi ya bwana Bula. Huwezi kujua huenda wana JF wanamjua zaidi ya anavyojulikana kwenye siasa za upinzani.
Miaka 5 iliyopita ya NCCR imepotea bure, Mbatia ameshindwa ku deliver kabisa.
mafanikio mema kwenye uchaguzi wenu.
Je,kati ya Mbatia na watangulizi wake, nani alikuwa bora angalau?
Marando?
Mrema?
Maguto?
Yeah mkuu MN,nasikia huyu Dodo hata hakuja mwenyewe, katuma mwakilishi tu!!!
Ahsante mkuu.Katika kuangalia alichoandika Waridi, sijaona alipotoa wasifu wa John Bula Dodo.
Kifupi Bula aliyezaliwa mwaka 1966 ana elimu ya Kidato cha Sita, ni mwenyekiti wa NCCR Mageuzi anayemaliza muda wake katika jimbo la Karatu.
Mpaka sasa tunafuatilia kwa karibu uchaguzi huu na taarifa zinadai wajumbe bado wanajieleza mbele ya NEC ya NCCR Mageuzi.
Nitakufahamisheni nini kimejiri kadiri kitakavyotokea. Hata Kahangwa aliitwa na naambiwa yumo ndani ya mkutano huu.
Matokeo katika kura za uenyekiti (NCCR Mageuzi Jan 04, 2009) ni kama ifuatavyo:
John Bula Dodo- Kura 11
James Francis Mbatia - Kura 159.
Kura za kuchagua Katibu mkuu zitapigwa kesho
Mbona bwana Dodo hakutokea kwenye mkutano wakati anajua amegombea nafasi nyeti?Nafasi ya Katibu Mkuu ina mgombea pakee, Sam Ruhusa kutoka jimbo la Ngara, mgombea ubunge 2005, ana Stashahada ya Business Management na ni mfanyabiashara.