Uchaguzi mkuu NCCR Mageuzi

mambo ya ngoswe!............................................

Couldnt put it better but unfortunately, this is not jambo la ngoswe. We are talkinh here aboput a political party whose one of its major ambitions ni kuchukua uongozi wa nchi-hili linatugusa wananchi wote wa Tanzania. Therefore, we need to kujadili hili extensively, otherwise, tutakuwa hatujitendei haki wenyewe
 
Waridi,
tunazungumzia nafasi ya mwenyekiti wa taifa wa chama cha siasa cha NCCR, nafasi ambayo ni kubwa na nyeti.Itawezekana vipi mtu asiyefahamika kabisa katika ulingo wa siasa, tena siasa zenyewe hizi za bongo aweze kumwangusha mwenyekiti anayetetea nafasi yake?manake usisahau kuwa wapiga kura ni watanzania hawa tunaowajua.Kama kweli ni wengi hatumjui huyo bura hata hao wapiga kura wa NCCR hapana shaka watakuwa hawamjui, sasa watawezaje kumpa uenyekiti mtu wasiyemfahamu?Je alishawahi kuwa kiongozi wa kisiasa kwenye ngazi yoyote,kama una ufahamu wowote juu ya hili nisaidie.
Hiyo competence unayoizungumzia inawezaje kuthibitishwa?nani atakayeithibitisha?
au unazungumzia competence kwa upande wa kitaaluma au mi sijakuelewa?hebu nisaidie kuifahamu hiyo competence unayoizungumzia.

Ngoja nifuatilie nione kama nitapata CV yake/zao nikuleteeni.
 
Ngoja nifuatilie nione kama nitapata CV yake/zao nikuleteeni.

ahsante kwa bidii yako.
nitashukuru sana kama ukiipata CV yake, itatusaidia kumfahamu kidogo huyo Bura na pia itawasaidia na wadau wa NCCR ambao kwa namna moja ama nyingine walikuwa hawamjui au hawamjui vizuri.Huwezi jua lyawezekana kuna wapiga kura wa NCCR humu jamvini!!!!
 
Mimi sioni tatizo katika upya wa Bula, badala yake naona ishara njema kwani mtu mpya kajitokeza na kwa mantiki hiyo huenda ana jipya.
Kwa taarifa nilizo nazo Bula ni candidate anayetokea upcountry, ni changamoto hasa kwa Mbatia ambaye 'katokea' Uholanzi kuja kutetea kiti chake.
Nani kamuweka nani hapo sijui na sidhani. kila mmoja wao kajaza fomu kwa wakati wake.

Waridi,

Nitashukuru kama utaturushia CV fupi ya bwana Bula. Huwezi kujua huenda wana JF wanamjua zaidi ya anavyojulikana kwenye siasa za upinzani.

Miaka 5 iliyopita ya NCCR imepotea bure, Mbatia ameshindwa ku deliver kabisa.

mafanikio mema kwenye uchaguzi wenu.
 
Yamkini kesho magazeti yatakava habari za wagombea, masaa mawili yaliyopita kaimu katibu mkuu ameongea na waandishi wa habari kuhusu uchaguzi huu.
Kwa walioko bongo, chekini local papers hiyo kesho
 
Waridi,

Nitashukuru kama utaturushia CV fupi ya bwana Bula. Huwezi kujua huenda wana JF wanamjua zaidi ya anavyojulikana kwenye siasa za upinzani.

Miaka 5 iliyopita ya NCCR imepotea bure, Mbatia ameshindwa ku deliver kabisa.

mafanikio mema kwenye uchaguzi wenu.

Je,kati ya Mbatia na watangulizi wake, nani alikuwa bora angalau?

Marando?
Mrema?
Maguto?
 
Je,kati ya Mbatia na watangulizi wake, nani alikuwa bora angalau?

Marando?
Mrema?
Maguto?

MREMA kwa kuwaacha mbali sana wenzake. Ubora wa kiongozi wa chama cha siasa unatokana na mafanikio yake kisiasa. Mrema alileta viti kibao vya uchaguzi NCCR.

Huyo Maguto aliongoza lini mpaka lini?
 
Huyo Maguto aliongoza lini mpaka lini?

Huyo Maguto, kwa sasa marehemu, alishikiria uenyekiti kwa kipindi cha takribani mwaka- kati ya 1999 Mrema alipochomoka na 2000 mauti yalipomkuta mzee huyo.
 
Katika kuangalia alichoandika Waridi, sijaona alipotoa wasifu wa John Bula Dodo.

Kifupi Bula aliyezaliwa mwaka 1966 ana elimu ya Kidato cha Sita, ni mwenyekiti wa NCCR Mageuzi anayemaliza muda wake katika jimbo la Karatu.

Mpaka sasa tunafuatilia kwa karibu uchaguzi huu na taarifa zinadai wajumbe bado wanajieleza mbele ya NEC ya NCCR Mageuzi.

Nitakufahamisheni nini kimejiri kadiri kitakavyotokea. Hata Kahangwa aliitwa na naambiwa yumo ndani ya mkutano huu.
 
Sasa wanajieleza wagombea umakamu M/Kiti na watapigiwa kura hapo hapo. Itafuatia zamu ya mwenywekiti.
 
nasikia huyu Dodo hata hakuja mwenyewe, katuma mwakilishi tu!!!
Yeah mkuu MN,

Bula hakuwepo katika mkutano na alikuwa anapigiwa debe na mwakilishi wake tu. Huyu ndo unaweza kutegemea atoe ushindani kwa Mwenyekiti anayetetea kiti chake? NCCR can't be serious at all. Hii imenifanya nikate tamaa hata kuendelea kuwafahamisha nini kinaendelea. Inakatisha tamaa kuona madude ya hivi
 
Matokeo katika kura za uenyekiti (NCCR Mageuzi Jan 04, 2009) ni kama ifuatavyo:

John Bula Dodo- Kura 11

James Francis Mbatia - Kura 159.

Kura za kuchagua Katibu mkuu zitapigwa kesho
 
Nilisema hakuna cha uchaguzi hapa zitarudi figure zilezile tu.Chama kama hiki eti nacho mwakani kinasimamisha mgombea wa urais.Kinaamini kina uwezo wa kuking'oa CCM 2010.
Kazi kwelikweli!
 
Katika kuangalia alichoandika Waridi, sijaona alipotoa wasifu wa John Bula Dodo.

Kifupi Bula aliyezaliwa mwaka 1966 ana elimu ya Kidato cha Sita, ni mwenyekiti wa NCCR Mageuzi anayemaliza muda wake katika jimbo la Karatu.

Mpaka sasa tunafuatilia kwa karibu uchaguzi huu na taarifa zinadai wajumbe bado wanajieleza mbele ya NEC ya NCCR Mageuzi.

Nitakufahamisheni nini kimejiri kadiri kitakavyotokea. Hata Kahangwa aliitwa na naambiwa yumo ndani ya mkutano huu.
Ahsante mkuu.
 
Matokeo katika kura za uenyekiti (NCCR Mageuzi Jan 04, 2009) ni kama ifuatavyo:

John Bula Dodo- Kura 11

James Francis Mbatia - Kura 159.

Kura za kuchagua Katibu mkuu zitapigwa kesho

Nafasi ya Katibu Mkuu ina mgombea pakee, Sam Ruhusa kutoka jimbo la Ngara, mgombea ubunge 2005, ana Stashahada ya Business Management na ni mfanyabiashara.
 
Nafasi ya Katibu Mkuu ina mgombea pakee, Sam Ruhusa kutoka jimbo la Ngara, mgombea ubunge 2005, ana Stashahada ya Business Management na ni mfanyabiashara.
Mbona bwana Dodo hakutokea kwenye mkutano wakati anajua amegombea nafasi nyeti?
 
Mbatia mwenyekiti tena NCCR- Mageuzi
Na Fidelis Butahe

MWENYEKITI wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia amefanikiwa kutetea nafasi yake ya uenyekiti wa taifa wa chama hicho.

Msimamizi wa uchaguzi huo, Samwel Ruhuza akitangaza matokeo ya uchaguzi huo alisema Mbatia alishinda uchaguzi mkuu wa chama hicho kwa kura 170 dhidi ya mpinzani wake John Dodo aliyepata kura 11.

Alisema kuwa nafasi ya makamu mwenyekiti wa chama hicho (Bara) itashikiliwa na Haji Khamis aliyeshinda kwa kura 170 dhidi ya mpinzani wake, Hashim Spunga aliyepata kura 81. Na nafasi ya makamu mwenyekiti (Visiwani) itashikiliwa na Rukia Hassan aliyepata kura 168.

Alisema kuwa nafasi ya wanawake halmashauri kuu Zanzibar walikuwa wagombea saba na nafasi zilikuwa tatu ambazo zilichukuliwa na Mariam Juma kura 98, Salma Juma kura 86 na Mose Fakhi kura 118.

Kwa upande wa nafasi za wanawake Halmashauri Kuu (Bara), watu 10 waligombea nafasi tano na walioshinda ni Agripina Buyongera kura 151, Lucy Fulgence kura 126, Dorice Kidera kura 127, Tabu Said kura 134 na Fatma Omary kura 133.

Nafasi nane za ujumbe wa Halmashauri Kuu Taifa zigombewa na watu 27 na waliotangazwa kushinda ni Sengondo Mvungi (161), Beat Mpitabakana (127), Faustine Sungura (136), Hashim Rungwe (138), Sebastian Thomas (92), Yusuf Nyamgenda (93) Joseph Selasini (125) na Fulgence Malangalila (92).

Nafasi mbili za ujumbe wa Halmashauri Kuu Vijana ziligombewa na watu watatu nafasi washindi walikuwani Raphael Tweve (148) na James Bazista(84).
 
jana,

alichaguliwa Sam Ruhuza kuwa katibu mkuu

naye Raurent Tara kuwa naibu katibu mkuu

hawa wawili ndilo tegemeo la mabadiliko makubwa yaliyopangwa kufanyika ili kukiimarisha chama

Wakati huo huo Makamu Mwanyekiti kwa upande wa Zanzibar ametengaza nia yake ya kuwania urais wa Zanzibar 2010 kama chama kitamruhusu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom