Uchaguzi mkuu NCCR Mageuzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi mkuu NCCR Mageuzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Waridi, Dec 31, 2008.

 1. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  WanaJF,
  Hii ni kutaka kukuhabarisheni kwamba ndani ya chama cha NCCR-Mageuzi kinachondelea kwa sasa ni hatua za mwisho mwisho za kuhitimisha mchakato wa uchaguzi mkuu wa viongozi wa kitaifa wa chama.
  Kama ilivyo ada, kila baada ya miaka mitano unafanyika uchaguzi wa namna hii.
  Itakumbukwa kwamba hadi sasa NCCR imekwisha kuwa chini ya uongozi wa wenyeviti wanne tofauti kwa nyakati tofauti
  • alianza Mhe.Mabere Marando
  • akafuatia Mhe.Agustine Mrema
  • akaja Mhe.Aidari Maguto(marehemu)
  • na wa sasa Mhe.James Mbatia

  Katika uchaguzi huu, habari za ndani zinatonya kwamba wanaowania Uenyekiti ni wawili (sijajua kama wote watapitishwa)

  Vile vile yaelekea nafasi nyinginezo kv. makamu mwenyekiti,katibu mkuu,naibu katibu mkuu,mweka hazina zitakamatwa na sura mpya kabisa kwa sababu wengi wa waliogomea nafasi hizo na wenye mwelekeo wa kushinda si wale waliokuwa wakizishikiria.
  Wachunguzi wa mambo wanasema, mwelekeo huo ni ishara kwamba chama hiki kimepania kujijenga upya kabisa, ya kale yatapita...

  Tega sikio, soon nitakuhabarisheni nani kang'olewa, nani kashinda, nani kawaje.
  Duru zinasema mtanange huu ni Jumapili ya juma hili.
   
 2. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #2
  Dec 31, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Tunashukuru kwa taarifa mkuu Waridi,

  Vipi hakuna nafasi ambazo wadau hapa wanaweza kurusha kete zao au "Too late to catch the train?"
   
 3. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mkuu,
  Pazia la kurejesha fomu litafungwa soon, any interested mdau aseme nimuunganishe kwa mkuu wa idara husika, kuna kitu kama 60 hours to go
   
 4. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawana mvuto hao wameshachelewa!!
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Dec 31, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mbona mambo yao yamekuwa ni kimyakimya sana?
   
 6. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #6
  Dec 31, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Sina hakika kama wameishachelewa,
  wamechelewa kufanya nini?
  na kumbe nani kawahi, wapi?

  Yamkini unazungumzia lengo la kila chama cha siasa... kuongoza dola?
   
 7. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #7
  Dec 31, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kama waandishi wa habari wako hapa JF watusaidie kujibu hilo swali, maana nijuavyo mimi NCCR kilitangaza wazi mara kadhaa kupitia press release kwamba kiko katika mchakato wa uchaguzi mkuu, na hata wagombea kadhaa baada ya kuchukua fomu walijieleza mbele ya waandishi wa habari.
  Vile vile ofisi ya katibu mkuu ilisambaza waraka nchi nzima kuwataarifu wanachama wajitokeze kugombea na wamejitokeza.
  Nahofu watu wasianze kudhani iko namna ya usiri, hata kama ingekuwepo ni vema sasa nimekuleteeni taarifa hizi. Kama nilivyodokeza nitakuhabarisheni developments time after time.
   
 8. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #8
  Dec 31, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Ndio maana ya uchaguzi. Huenda wakaja watu wenye speed kali na wenye mvuto.
   
 9. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #9
  Dec 31, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chaguzi zenyewe za kibongo mkuu?Watu wanapanga safu kabla hata ya uchaguzi mwenyekiti mpaka wajumbe wanajulikana.
  Subiri hao nccr wataje matokeo utaona sura ni zilezile tu Mbatia,Mvungi...
   
 10. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #10
  Dec 31, 2008
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,262
  Likes Received: 4,236
  Trophy Points: 280
  Vipi MBATIA anatetea kiki chake?
   
 11. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #11
  Dec 31, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  The question ni kuwa kitakuwa chama kweli cha siasa, au kitaendelea kuwa kile kile kinachotumiwa na kina Marando ku-weaken na ku-destabilize opposition, au kufuga majasusi wanaokiyumbisha kila kukicha? Kama wameamua kufanya mambo kimya kimya ili kukisafisha na kutowapa nafasi wanaokiharibu well and good, tusubiri nini kitaendelea.
   
 12. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2009
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Wakuu,
  Kutoka jikoni NCCR naambiwa jua la kurejesha fomu limekuchwa na wafuatao ndio fomu zao ziko mezani kuwania nafasi kuu saba za uongozi wa chama.

  Mwenyekiti
  1. John Bula Dodo
  2. James Francis Mbatia

  Makamu Mwenyekiti- Bara
  1. Mama Rakia Abubakari Hassan
  2. Hashim Rungwe
  Makamu Mwenyekiti - Zanzibar
  1. Haji Hambari Khamis

  Katibu Mkuu
  1. Sam Ruhuza

  Naibu Katibu Mkuu- Bara
  1. Raurent Tara
  2. Joseph Serasini

  Naibu Katibu Mkuu- Zanzibar
  1. Musa Kombo Musa
  2. Ali Juma Omari

  Mweka hazina
  1. Mama Mariam Mwakingwe
  2. Sebastian Thomas
  Majina haya yatahakikiwa kesho katika kikao cha halmashauri kuu ya taifa kabla ya kupelekwa mkutano mkuu, a day later
   
 13. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #13
  Jan 2, 2009
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Angalia list ya wagombea, no Marando, no Mvungi, No Mwaiseje... katika safu ya juu ya uongozi unaomaliza muda wake, ni wawili tu wamegombea tena... sawa na 28.5%, obviously safu itakuwa na upya.
   
 14. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #14
  Jan 2, 2009
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Katika hii miaka mitano inayoishia, Mbatia ameshindwa kuinusuru NCCR.
  Chama kimeendelea kudorora kila siku, sasa huyo John Bula mbona mgeni masikioni mwangu katika duru za kisiasa, ataweza kweli kuinusuru NCCR?
  NCCR inatakiwa kurudi kwenye chati kama zamani ili kuongeza ushindani na kutanua wigo wa demokrasia.Kwahiyo basi kama Mbatia atashinda tena anwajibika kubadilisha mikakati ya kukiongoza chama chake ili kiweze kushindana badala ya kusindikiza ama kutumiwa na mahasidi kuivuruga demokrasia.
  Mi naamini kabisa kuwa mwenyekiti ndiye anayetoa taswira ya chama husika.
  Au Bula amewekwa kumsindikiza Mbatia?Kwangu mimi bado sioni kama Bula atatoa ushindani wa kutosha kwa Mbatia.Labda kama mimi ndiye simfahamu vizuri bw.Bula naomba kufahamishwa.

  BTW mbona mgombea urais mwanasheria Edmund Sengondo Mvungi hajawania nafasi yeyote?au yeye ni maalum na uraisi tuuu!!!????
   
 15. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #15
  Jan 2, 2009
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mwita,
  Sidhani kutofahamika kwa Bula kunaweza kuwa sababu pekee ya kumwangusha, itategemea competence yake. Aidha kama unavyosema, endapo ni kweli Mbatia hakufanya vizuri basi Bula anaweza kutumia upenyo huo kushinda.
  Kuhusu Mvungi, sidhani kama ana umaalum wa kugombea urais, usishangae akijitokeza mtu/watu wapya kabisa kuwania urais kwa tiketi ya NCCR come 2010
   
 16. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #16
  Jan 2, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ni kweli huyu jamaa ni mgeni hata kwangu mimi katyika siasa za upinzani. Au amewekwa kama kanyabwoya kuonyesha kuwa Mbatia alikuwa na mshindani?
   
 17. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #17
  Jan 2, 2009
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mimi sioni tatizo katika upya wa Bula, badala yake naona ishara njema kwani mtu mpya kajitokeza na kwa mantiki hiyo huenda ana jipya.
  Kwa taarifa nilizo nazo Bula ni candidate anayetokea upcountry, ni changamoto hasa kwa Mbatia ambaye 'katokea' Uholanzi kuja kutetea kiti chake.
  Nani kamuweka nani hapo sijui na sidhani. kila mmoja wao kajaza fomu kwa wakati wake.
   
 18. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #18
  Jan 2, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Si tatizo wiapo siasa zetu zisingekwua na mizengwe. katika mfumo wa siasa safi, jambo kama hili ni zuri tu. lakini katika mfumo huu tulioujenga wa mizengwe, inakuwa vigumu sana kuamini kuwa mwenyekiti wa chama wa wilaya anaweza kumshinda mwenyekiti wa taifa anayetetea kiti chake.
   
 19. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #19
  Jan 2, 2009
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Waridi,
  tunazungumzia nafasi ya mwenyekiti wa taifa wa chama cha siasa cha NCCR, nafasi ambayo ni kubwa na nyeti.Itawezekana vipi mtu asiyefahamika kabisa katika ulingo wa siasa, tena siasa zenyewe hizi za bongo aweze kumwangusha mwenyekiti anayetetea nafasi yake?manake usisahau kuwa wapiga kura ni watanzania hawa tunaowajua.Kama kweli ni wengi hatumjui huyo bura hata hao wapiga kura wa NCCR hapana shaka watakuwa hawamjui, sasa watawezaje kumpa uenyekiti mtu wasiyemfahamu?Je alishawahi kuwa kiongozi wa kisiasa kwenye ngazi yoyote,kama una ufahamu wowote juu ya hili nisaidie.
  Hiyo competence unayoizungumzia inawezaje kuthibitishwa?nani atakayeithibitisha?
  au unazungumzia competence kwa upande wa kitaaluma au mi sijakuelewa?hebu nisaidie kuifahamu hiyo competence unayoizungumzia.
   
 20. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #20
  Jan 2, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135

  mambo ya ngoswe!............................................
   
Loading...