Wananchi wa Malawi wanatarajiwa kupiga kura Septemba 16, 2025 kuchagua rais mpya, wabunge na madiwani, ikiwa ni baada ya miaka mitano tangu uchaguzi uliopita ambapo vyama 17 vitashiriki huku wagombea wenye mchuano mkali wakitajwa kuwa ni:
1. Lazarus Chakwera – Mgombea wa The Malawi Congress Party (MCP) na Rais wa sasa, anayewania muhula wa pili
2. Peter Mutharika – Mgombea wa The Democratic Progressive Party (DPP) na Rais wa zamani, anayetaka kurejea madarakani
3. Joyce Banda – Mgombea wa People’s Party (PP) na Rais wa zamani, anayesisitiza ajira kwa vijana na uwezeshaji wa wanawake
4. Dalitso Kabambe – Mgombea wa United Transformation Movement (UTM), anayepigia debe mabadiliko ya kiuchumi na uwajibikaji.
5. Michael Bizwick Usi – Mgombea wa Odya Zake Alibe Mlandu (OZAM)
Michael Usi atachuana vikali na Chakwera pamoja na Mutharika, ambao wote wana misingi ya kisiasa imara na wafuasi wengi. Hata hivyo, Usi ana mvuto kwa wapiga kura wanaotafuta mabadiliko, uwajibikaji na kupunguza rushwa.
Uchaguzi huu unatazamiwa kuwa miongoni mwa yenye ushindani mkubwa katika historia ya Malawi, huku kuingia kwa Usi kukiongeza mvuto katika uwanja uliojaa wanasiasa wakongwe na wapinzani wapya. Lakini kwa upande mwingine wachambuzi wanaona kama Usi anatamaa na kuwa ni Msaliti kwani anashindana na aliyempa nyadhifa ya umakamu rais.
Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya Malawi (MEC) kwa uchaguzi wa mwaka 2025, jumla ya wapiga kura 7,200,905 wamejiandikisha, sawa na asilimia 65.7% ya wananchi wenye umri wa kupiga kura kulingana na makadirio ya Shirika la Takwimu la Taifa. Kati yao, wanawake waliojiandikisha ni 4,113,342 (takribani 57.1%), huku wanaume wakiwa 3,087,563 (42.9%).
Fuatilia Mubashara mchakato wa kupiga kura unavyoendelea nchini humo
=============
Malawians are set to vote on September 16, 2025, to elect a new president, members of parliament, and local councillors, five years after the last election. A total of 17 parties will take part, with the main contenders being:
1. Lazarus Chakwera– Candidate of the Malawi Congress Party (MCP) and the incumbent president, seeking a second term
2. Peter Mutharika– Candidate of the Democratic Progressive Party (DPP) and former president, aiming to return to power
3. Joyce Banda– Candidate of the People’s Party (PP) and former president, emphasizing youth employment and women’s empowerment
4. Dalitso Kabambe– Candidate of the United Transformation Movement (UTM), campaigning on economic reforms and accountability
5. Michael Bizwick Usi– Candidate of Odya Zake Alibe Mlandu (OZAM)
Usi is expected to face stiff competition from Chakwera and Mutharika, both of whom command strong political bases and large followings. However, Usi appeals to voters who are seeking change, accountability, and a reduction in corruption
This election is projected to be one of the most competitive in Malawi’s history, with Usi’s entry adding momentum to a race otherwise dominated by veteran politicians and new challengers. On the other hand, some analysts view Usi as overly ambitious and even a betrayer, since he is running against the president who appointed him to be vice president.
According to the Malawi Electoral Commission (MEC), a total of 7,200,905 voters have registered for the 2025 election, representing 65.7% of eligible citizens based on estimates from the National Statistics Office. Among them, 4,113,342 are women (57.1%) and 3,087,563 are men (42.9%)
-------------
Zoezi la Kuhesabu kura linaendelea Malawi
Kuhesabu kura kumeanza baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa saa 14:00 GMT katika uchaguzi muhimu wa urais nchini Malawi. Rais aliyepo madarakani, Lazarus Chakwera, anawania muhula wa pili akichuana na mtangulizi wake, Peter Mutharika, huku wote wakiahidi kulifufua taifa kiuchumi. Ikiwa hakuna mgombea atakayepata zaidi ya nusu ya kura, duru ya marudio inaweza kufanyika
Takribani kura milioni 3.7 zimepigwa leo licha ya changamoto zilizojitokeza kwenye baadhi ya vituo kutokana na hitilafu za mashine za kuchukua alama za vidole. Tume ya Uchaguzi ya Malawi imesema itatangaza matokeo ya urais kufikia Septemba 24, huku matokeo ya ubunge yakitarajiwa ifikapo Septemba 30. Tume hiyo imethibitisha kuwa changamoto za foleni zilitokea lakini ziliweza kudhibitiwa
Pamoja na changamoto hizo, hatua za dharura zilichukuliwa kuruhusu wapiga kura wasioweza kuandika kuweka alama ya kidole chenye wino, huku wengine wakitumia kalamu za kawaida. Ingawa kinyang’anyiro kinachukuliwa kama cha watu wawili kati ya Chakwera na Mutharika, wagombea wengine 15 pia wameshiriki, wakiwemo marais wa zamani akiwamo Joyce Banda, mwanamke pekee aliyewahi kuongoza taifa hilo
View: https://youtu.be/XyFg-iIF_w8?si=mV5B1Ia8-JSOmlFD
==========
Taarifa ya Matokeo ya awali, Rais wa zamani Peter Mutharika anaongoza katika Majimbo 45
Tume ya uchaguzi Malawi inaendelea na zoezi la kukusanya na kuhesabu kura ambapo Septemba 16, 2025 Wananchi walipiga kura kuchagua Rais, wabunge pamoja na Madiwani. Uchaguzi uliohusisha ushiriki wa vyama 17 katika kinyanganyiro ya kiti cha Urais ambapo mchuano mkali ulikuwa kati ya Rais wa zamani Peter Mutharika na Rais anayemaliza muda wake Lazarua Chakwera
Kwa mujibu wa Taarifa za Matokeo ya awali ya uchaguzi Rais wa zamani Peter Mutharika anaongoza katika Majimbo 45 huku akifuatiwa na Lazarus Chakwera Rais anayemaliza muda wake.
=========
Tume ya uchaguzi Malawi (MEC) yatoa onyo kwa Vyama vya Siasa kutangaza ushindi kabla ya Matokeo Rasmi
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Malawi, Annabel Mtalimanja, amezionya vyama vya siasa kutotangaza ushindi kabla ya matokeo rasmi. Onyo hilo limetolewa baada ya kambi za wagombea wakuu wa urais, Rais wa sasa Lazarus Chakwera na mtangulizi wake Peter Mutharika, kudai ushindi katika uchaguzi uliofanyika Septemba 16, 2025
Akizungumza na wanahabari Septemba 18, 2025 Mtalimanja alisisitiza kuwa ni tume pekee yenye mamlaka ya kutangaza matokeo, na yatawekwa wazi baada ya kura zote kuhesabiwa na kuthibitishwa ili kuepusha changamoto za kisheria
Wananchi wa Malawi wanasubiri matokeo kwa hamu, huku kukiwa na kumbukumbu za uchaguzi wa mwaka 2019 uliofutwa na mahakama kutokana na dosari nyingi, hali iliyompa Chakwera ushindi mkubwa katika marudio yaliyomuinua kuwa rais
*************
The parties of the two main candidates in Malawi's presidential election declared victory Thursday, drawing rebukes from the electoral commission which is yet to announce results.
Tuesday's vote is expected to be a close race between President Lazarus Chakwera and challenger Peter Mutharika, the former president who was beaten by Chakwera in the last elections five years ago.
Officials from Chakwera's Malawi Congress Party and Mutharika's Democratic Progressive Party held separate news briefings and said their candidates had won.
The Malawi Electoral Committee says it has counted more than 99% of the votes but hasn't declared any results, keeping a country struggling through an economic crisis and soaring inflation on edge.
“The commission will not hurry the results management process just because some political party leaders and candidates are piling up pressure,” said MEC chairperson Justice Annabel Mtalimanja.
She told parties and their candidates to respect the counting procedures.
Election officials must declare the results of the presidential election within seven days of polling stations closing on Tuesday.
Malawians voted for president, but also for the makeup of Parliament and more than 500 local government representatives in a largely rural country of 21 million in southern Africa.
The presidential race had 17 candidates, but analysts say it was likely to be a close contest between Chakwera, 70, and Mutharika, 85. A candidate must get more than 50% of the vote to win. If no one does there will a runoff election.
Source: ABC NEWS
=========
Polisi Malawi Wakamata Watu 8 kwa Tuhuma za Udanganyifu wa Uchaguzi
Polisi nchini Malawi wamewakamata watu nane kwa tuhuma za udanganyifu wa uchaguzi wakati taifa hilo likisubiri matokeo ya mwisho ya uchaguzi mkuu uliofanyika Septemba 16, 2025
Mkuu wa Jeshi la Polisi, Merlyne Yolamu, alisema watuhumiwa hao waliokuwa wakifanya kazi kama waingiza takwimu, walikuwa wakijaribu kuchakachua matokeo.
Uchaguzi wa mwaka 2019 nchini Malawi ulikumbwa na utata baada ya mahakama kuu kufuta ushindi wa Rais wa wakati huo, Peter Mutharika, ikibainisha kuwepo kwa udanganyifu mkubwa.
Kutokana na hali hiyo, tume ya uchaguzi ya Malawi iko makini zaidi kuhakikisha hakuna dosari. Taarifa za awali za matokeo zinaonyesha Mutharika anaongoza kwenye kinyang’anyiro cha urais, huku Rais aliyepo madarakani, Lazarus Chakwera, akiwa nafasi ya pili
Source: BBC
=======
Rais wa zamani Peter Mutharika anaongoza kwa kura Asilimia 66% hadi sasa
Rais wa zamani wa Malawi, Peter Mutharika, ameibuka kinara katika uchaguzi wa urais uliofanyika Septemba 16, baada ya matokeo ya awali kutoka katika takribani theluthi mbili ya mabaraza 36 ya kitaifa kuonyesha anaongoza. Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi, Mutharika amepata karibu asilimia 66 ya kura halali, huku Rais aliyepo madarakani, Lazarus Chakwera, akishika nafasi ya pili kwa asilimia 24.
Matokeo haya ya awali yametolewa Septemba 22, 2025 na yanaonyesha Mutharika, mwenye umri wa miaka 85, yuko kwenye nafasi nzuri ya kushinda moja kwa moja endapo ataendelea kudumisha wingi wa kura, kwani mshindi anahitajika kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura halali. Endapo hakuna mgombea atakayefikisha kiwango hicho, basi duru ya pili ya uchaguzi itafanyika
Wachambuzi wa kisiasa walikuwa wametabiri kuwa Mutharika, ambaye aliwahi kuwa madarakani kati ya mwaka 2014 na 2020, angekuwa mpinzani mkubwa wa Chakwera katika jaribio lake la kurejea Ikulu. Uchaguzi huu unafuatiliwa kwa karibu kwani unahusisha kinyang’anyiro cha siasa na historia ya uongozi nchini Malawi
Source: Reuters
=========
Rais Chakwera akubali kushindwa uchaguzi dhidi ya mtangulizi wake Peter Mutharika
Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera, amekubali kushindwa katika uchaguzi wa urais uliofanyika Septemba 16, 2025 dhidi ya mpinzani wake na mtangulizi wake Rais wa zamani Peter Mutharika. Malawi ni taifa la Kusini mwa Afrika linalokabiliwa na gharama kubwa za maisha na uhaba mkubwa wa mafuta
“Itakuwa ni sahihi nikubali kushindwa kwa heshima ya matakwa yenu kama wananchi na kwa heshima ya katiba,” alisema Chakwera mwenye umri wa miaka 70 katika hotuba yake
“Ilikuwa wazi kuwa mpinzani wangu, Peter Mutharika, ana uongozi mkubwa usioweza kushindaniwa,” aliongeza
Chakwera pia aliahidi kukabidhi madaraka kwa amani, huku Tume ya Uchaguzi ikitarajiwa kutangaza matokeo kamili Jumatano. Hadi sasa matokeo rasmi yaliyotolewa yanaonyesha kuwa Mutharika anaongoza kwa kiwango kikubwa dhidi ya Chakwera
Source: Reuters & Aljazeera
========
Rais wa zamani Peter Mutharika (85), ashinda kwa kishindo kwa kura asilimia 57%
Rais wa zamani wa Malawi, Peter Mutharika, ametangazwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika Septemba 16, 2025 hatua inayomrejesha madarakani akiwa na miaka 85
Matokeo rasmi yanaonyesha Mutharika amepata asilimia 57 ya kura, huku Rais Lazarus Chakwera, mwenye miaka 70, akipata asilimia 33
Chakwera, ambaye aliwahi kuwa mchungaji kabla ya kuingia siasa, alikubali kushindwa hata kabla matokeo ya mwisho hayajatangazwa rasmi na kumpigia simu Mutharika kumpongeza kwa "ushindi wa kihistoria"
Mutharika, ambaye ni mwanasheria na profesa wa zamani, aliongoza Malawi kuanzia mwaka 2014 hadi 2020, kabla ya kushindwa na Chakwera kwa tofauti kubwa ya kura.
Anarejea madarakani wakati ambapo uchumi wa Malawi unakabiliwa na mtikisiko mkubwa, ukiwa na upungufu wa mafuta na fedha za kigeni. Kiwango cha mfumuko wa bei kimeripotiwa kufikia karibu asilimia 30. Katika mji mkuu wa Lilongwe, kuku aliyegandishwa supermarket unauzwa kwa karibu dola 20, wakati wananchi wengi wanaishi kwa chini ya dola 2 kwa siku.
Tume ya uchaguzi imesema ilitumia siku zote nane zilizoruhusiwa kisheria kutangaza matokeo ili kuhakikisha ukaguzi wa kina na kushughulikia malalamiko yote.
Mara ya mwisho Mutharika kushinda, mwaka 2019, matokeo yalifutwa na mahakama kuu baada ya kubaini udanganyifu mkubwa, ikiwemo kutumia correction fluid kubadilisha matokeo. Uchaguzi huo ulirudiwa mwaka uliofuata ambapo Chakwera alishinda kwa kishindo.
Hii imekuwa mara ya nne wawili hawa kukutana kwenye kinyang’anyiro cha urais. Ni vyema pia kukumbuka kuwa kaka yake mkubwa, Bingu wa Mutharika, aliwahi kuwa rais kabla ya kufariki akiwa madarakani mwaka 2012
Source: Reuters, BBC & Aljazeera