Kutokana na hali ya hewa kuwaendea vibaya ktk vyama vyao wanasiasa wawili maarufu,waziri mkuu mstaafu mh.Edward Lowassa na mh.Mbunge Zitto Zuberi Kabwe (CHADEMA) tumaini pekee lilibaki kwa wanasiasa hawa ni kugombea nafasi ya urais kwa Lowassa,ubunge au urais kwa Zitto ni ugombea binafsi.Kauli mbalimbali zinazotolewa na viongozi wa wanasiasa hawa kuwashutumu na kuwapinga waziwazi ni dalili mbaya kwa wanasiasa hawa.Kauli hizo zinazotolewa na viongozi wao CCM na CHADEMA zinawahusisha na uchu wa madaraka makubwa ya kuongoza nchi hii na kusambaratisha vyama vyao. Tumemsikia naibu katibu mkuu wa CCM,ndugu Philipo Mangula akiwashutumu baadhi ya wanachama wa CCM kuanza kampeni za urais mapema kinyume na taratibu za chama.Hata katibu Mwenezi wa CCM ,Ndg.Nnape Nnauye akemea hali hiyo akimlenga Lowassa.Iwapo bunge la katiba likipitisha mgombea binafsi kuna uwezekano mkubwa wanasiasa hawa kugombea urais kwa upande wa Lowassa au ubunge / urais kwa upande wa ZZT. Rai yangu ni kwamba bunge la katiba liwe makini sana katika kujadili kipengele cha mgombea binafsi.Tunatambua mchango wa vyama siasa katika maendeleo na mustakabali wa nchi yetu.Vyama hivi vinaongozwa na sheria,taratibu na kanuni mbalimbali zinazopelekea kuwapata viongozi waadilifu kutumikia taifa hili.Tumeona viongozi waadilifu waliolitumikia taifa hili kutokana na vyama vya ASP na Afro Shiraz baadae CCM.Hata baadhi ya vyama vya upinzani vimetoa baadhi ya wabunge walioleta changamoto kubwa bungeni.Iwapo mgombea binafsi akipitishwa EL na ZZT yaweza ikawa neema kwao.