Uchaguzi mkuu 2015 : Mgombea binafsi akipitishwa katika katiba mpya Lowassa na Zitto watasheherekea.

mbeyaman

Member
Sep 28, 2013
97
28
Kutokana na hali ya hewa kuwaendea vibaya ktk vyama vyao wanasiasa wawili maarufu,waziri mkuu mstaafu mh.Edward Lowassa na mh.Mbunge Zitto Zuberi Kabwe (CHADEMA) tumaini pekee lilibaki kwa wanasiasa hawa ni kugombea nafasi ya urais kwa Lowassa,ubunge au urais kwa Zitto ni ugombea binafsi.Kauli mbalimbali zinazotolewa na viongozi wa wanasiasa hawa kuwashutumu na kuwapinga waziwazi ni dalili mbaya kwa wanasiasa hawa.Kauli hizo zinazotolewa na viongozi wao CCM na CHADEMA zinawahusisha na uchu wa madaraka makubwa ya kuongoza nchi hii na kusambaratisha vyama vyao. Tumemsikia naibu katibu mkuu wa CCM,ndugu Philipo Mangula akiwashutumu baadhi ya wanachama wa CCM kuanza kampeni za urais mapema kinyume na taratibu za chama.Hata katibu Mwenezi wa CCM ,Ndg.Nnape Nnauye akemea hali hiyo akimlenga Lowassa.Iwapo bunge la katiba likipitisha mgombea binafsi kuna uwezekano mkubwa wanasiasa hawa kugombea urais kwa upande wa Lowassa au ubunge / urais kwa upande wa ZZT. Rai yangu ni kwamba bunge la katiba liwe makini sana katika kujadili kipengele cha mgombea binafsi.Tunatambua mchango wa vyama siasa katika maendeleo na mustakabali wa nchi yetu.Vyama hivi vinaongozwa na sheria,taratibu na kanuni mbalimbali zinazopelekea kuwapata viongozi waadilifu kutumikia taifa hili.Tumeona viongozi waadilifu waliolitumikia taifa hili kutokana na vyama vya ASP na Afro Shiraz baadae CCM.Hata baadhi ya vyama vya upinzani vimetoa baadhi ya wabunge walioleta changamoto kubwa bungeni.Iwapo mgombea binafsi akipitishwa EL na ZZT yaweza ikawa neema kwao.
 
Viongoz wanatokana na kura za wananchi uadilifu wao unapimwana mawazo ya watanzania kwenye box la kura....mgombea binafsi ni muhimu kwa ukuaji wa demokrasia..maamuz ya kupitisha yasilenge watu ila maslah mapana ya taifa...kuchaguliwa kama mgombea binafsi ni ishara ya kuaminika pia
 
Itawafaidia nini kama mgombea binafsi akipitishwa huku wao hawakubaliki kwa wapiga kura? Hasa zzk
 
Kutokana na hali ya hewa kuwaendea vibaya ktk vyama vyao wanasiasa wawili maarufu,waziri mkuu mstaafu mh.Edward Lowassa na mh.Mbunge Zitto Zuberi Kabwe (CHADEMA) tumaini pekee lilibaki kwa wanasiasa hawa ni kugombea nafasi ya urais kwa Lowassa,ubunge au urais kwa Zitto ni ugombea binafsi.Kauli mbalimbali zinazotolewa na viongozi wa wanasiasa hawa kuwashutumu na kuwapinga waziwazi ni dalili mbaya kwa wanasiasa hawa.Kauli hizo zinazotolewa na viongozi wao CCM na CHADEMA zinawahusisha na uchu wa madaraka makubwa ya kuongoza nchi hii na kusambaratisha vyama vyao. Tumemsikia naibu katibu mkuu wa CCM,ndugu Philipo Mangula akiwashutumu baadhi ya wanachama wa CCM kuanza kampeni za urais mapema kinyume na taratibu za chama.Hata katibu Mwenezi wa CCM ,Ndg.Nnape Nnauye akemea hali hiyo akimlenga Lowassa.Iwapo bunge la katiba likipitisha mgombea binafsi kuna uwezekano mkubwa wanasiasa hawa kugombea urais kwa upande wa Lowassa au ubunge / urais kwa upande wa ZZT. Rai yangu ni kwamba bunge la katiba liwe makini sana katika kujadili kipengele cha mgombea binafsi.Tunatambua mchango wa vyama siasa katika maendeleo na mustakabali wa nchi yetu.Vyama hivi vinaongozwa na sheria,taratibu na kanuni mbalimbali zinazopelekea kuwapata viongozi waadilifu kutumikia taifa hili.Tumeona viongozi waadilifu waliolitumikia taifa hili kutokana na vyama vya ASP na Afro Shiraz baadae CCM.Hata baadhi ya vyama vya upinzani vimetoa baadhi ya wabunge walioleta changamoto kubwa bungeni.Iwapo mgombea binafsi akipitishwa EL na ZZT yaweza ikawa neema kwao.

wewe unaonekana ungekuwepo wakati wa YESU Yuda Iskarioti ungemchagua kuwa RAISI, Mtu ameonyesha true clour wewe unakuja na thred ya kumhusudu!
 
Watafute uwaulize usikie maoni yao. Mgobea binafsi mziki mwingine....waulize wenye uzoefu Marekani watakueleza.
 
Nadhani malengo yao ya kuweka historia kuwa WALISHAWAHI KUGOMBEA URAIS YATATIMIA! Lakini kushinda ni ndoto kwao,wote wananuka mmoja ufisadi na wizi,mwingine ana dhambi mbaya ya usaliti ambayo itamtafuna hadi kaburini.
 
Back
Top Bottom