Uchaguzi Kenya: Nani atakuwa rais mpya

Uchaguzi Kenya: Nani atakuwa rais mpya

Imebaki siku moja tu ya kesho wananchi wa kenya wafanye uchaguzi wa kumpata rais wao mpya. Swali langu kwa wana jf ni hili, nani atashinda na kuwa rais mpya wa kenya kati ya wagombea wote waliopo?. Mwaga maoni yako sasa!.

Bila shaka Kenyatta atashinda.ameonyesha nitishio kwa Raila hadi akapakaziwa kesi.
 
jamani Mungiki Tunaomba mdumishe Amani tuuuu..... Kama mnapenda sna machafuko nendeni Silia Wakenya kazi ni kwenu kuchagua kiongozi mnayemwamini kwa sababu Nguvu ya kiongozi ipo Kwa waongozwaji. All the best
 
Nasikia Kinana anagombea ubunge huko,ni kweli?
 
hata nape yuko huku thika maeneo ya gatundu anampigia kampeni uhuru nasikia mwigulu pia anakuja kuongeza nguvu ya matusi na lusinde pia mobimba diwani wake.....
 
Imebaki siku moja tu ya kesho wananchi wa kenya wafanye uchaguzi wa kumpata rais wao mpya. Swali langu kwa wana jf ni hili, nani atashinda na kuwa rais mpya wa kenya kati ya wagombea wote waliopo?. Mwaga maoni yako sasa!.

Who cares
 
Ni Uhuru Muigai Kenyatta Rais wa jamhuri ya kenya kuanzia jmanne. Anaepinga na apingekama hukuridhika weka hela mezani tubishane kwa tija.
 
Mungu atawapa wakenya kiongozi wao....
 
opions polls zote zilizoendeshwa mpaka muda wa mwisho kabisa inaonesha hakutakuwa na mshindi kwenye first round of voting. Kwa maana ya kwamba Bwana Raila na Uhuru wanategemewa kupata kupata kura zaidi ya asilimia 40% lakini hazizidi asilimia 50%.

Ila ajabu ni kwamba Bwana Mudavadi consistently amekuwa akitabariwa atapata kura za asilimia kati ya 4% mpaka 5%.

ikumbukwe kuwa uchaguzi wa Kenya hakuna issu of Simple Majority lazima mshindi apate zaidi ya asilimia 50%.

Kwa maana hiyo wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema Bwana Mudavadi ana hodhi mtaji TOSHA kwenye siasa za Kenya. IKumbukwe kuwa muungano wa Jubilee walimtapeli Bwana Mudavadi kuwa angekuwa mgombe wao. Vile vile Bwana Mudavadi baada ya kuhisi kuwa asingepita kwenye chama cha ODM cha Raila kuwa mgombea Uraisi aliamua kuondoka mapema kabla ya michakato ya uchaguzi ndani ya chama haijaanza.

Sasa swali ni kuwa kwenye second round of voting Bwana Mudavadi ataenda PANDE IPI?

JUBILEE ya UHURU ambao walimpateli kuwa angekuwa MGOMBEA WAO WA URAIS au CORD ambako aliondoka mapema baada ya kuhisi kuwa asingekuwa na nafasi ya kupata TIKETI ya kugombea URAISI.

Ila Afrika ina miujuza mingi you never know lolote laweza kutokea kwenye FIRST ROUND OF VOTING !
MPUNGA upo sahihi.....

Leo Uhuru Kenyatta na JUBILEE walikua Uhuru park na Raila Odinga na CORD walikua Nyayo stadium

Uhuru Kenyatta na timu yake wamejaza watu wengi sana na hata hivyo walimaliza kampeni vizuri.Kitu nilichojifunza ni kwamba uhuru kenyatta (ingawa sikupenda ashinde uchaguzi huu) anajua kucheza na emotions za vijana na wananchi.Akiwa kwenye midahalo anajua jinsi ya kuhitimisha na hata kwenye mkutnano wa leo amehitimisha vizuri na kwa mbwembwe zinazovuta kura(vote attraction).

Ninachoona sasa uchaguzi huu utaenda raundi mbili na katika raundi ya pili ndipo Musalia Factor(excuse me,sio MASALIA so be atttentive please) itakapo-apply.

Musalia Mudavadi anaunga mkono na former president Daniel Arap Moi.Most likely Musalia akamuuunga mkono Uhuru Kenyatta ila inabidi moi afanye kazi sana kumshawishi Mwanae Gideon na Nicholous Biwott wa chama cha KANU wapatane na Uhuru Kenyatta maana hawako in good terms.Hata hivyo kwa tishio la kufukua upya kashfa ya Goldensberg,Anglo Leasing na kashfa ya mauaji Dr.Robert Ouko inabidi akina Biwott(mfanyabiashara tajiri na mwanasiasa kutoka Kalenjin) wakubaliane na Moi ili kumnusuru Moi ambaye amewabeba kisiasa na hawakukutana barabarani na ukizingatia pia historia ya Moi na willium Ruto(kutoka kalenjin/rift valley) tangu akiwa Umoja wa vijana wa kANU na Role aliyo-play since 1992.

Pia tusisahau Uhuru Kenyatta ndiye aliyekua chaguo la Moi miaka 10 iliyopita hata kuiweka KANU rehani.Ilikua kama kulipa fadhila

Kwa upande Mwingine Odinga ana historia na Mudavadi na pia kwa heshima ya watu wa Nyanza na Western inabidi Mudavadi aone aibu ingawa hili kwa wanasiasa wa kiafrika ni nandra.

Kambi ya Mudavadi ndiyo itakaoamua mshindi raundi ya pili.Najua peter Kenneth atamuunga mkono Uhuru na Martha Karua hatabiriki ila anaweza kuamua neutral kwamba kura ziende popote au kwa kuwa ni hardliner atataka Raila apigiwe kura kwa kuwa msimamo wake ni kuwa washtakiwa wa ICC hawatakiwi kugombea nafasi yoyote.

Raund ya pili raila Odinga atashinda kwa kuwa ni mzoefu wa siasa za allliance
 
Last edited by a moderator:
mambo ya siasa hayana utabili, subilini kura zipigwe, zihesabiwe ndiyo tutajua nani kashinda! msianze kutabili kama ilivyotabiliwa chadema 2010 alafu ikaangukia pua na kutokukubali matokeo na kutomtambua rais na kuanza kurusha ngumi!
 
opions polls zote zilizoendeshwa mpaka muda wa mwisho kabisa inaonesha hakutakuwa na mshindi kwenye first round of voting. Kwa maana ya kwamba Bwana Raila na Uhuru wanategemewa kupata kupata kura zaidi ya asilimia 40% lakini hazizidi asilimia 50%.

Ila ajabu ni kwamba Bwana Mudavadi consistently amekuwa akitabariwa atapata kura za asilimia kati ya 4% mpaka 5%.

ikumbukwe kuwa uchaguzi wa Kenya hakuna issu of Simple Majority lazima mshindi apate zaidi ya asilimia 50%.

Kwa maana hiyo wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema Bwana Mudavadi ana hodhi mtaji TOSHA kwenye siasa za Kenya. IKumbukwe kuwa muungano wa Jubilee walimtapeli Bwana Mudavadi kuwa angekuwa mgombe wao. Vile vile Bwana Mudavadi baada ya kuhisi kuwa asingepita kwenye chama cha ODM cha Raila kuwa mgombea Uraisi aliamua kuondoka mapema kabla ya michakato ya uchaguzi ndani ya chama haijaanza.

Sasa swali ni kuwa kwenye second round of voting Bwana Mudavadi ataenda PANDE IPI?

JUBILEE ya UHURU ambao walimpateli kuwa angekuwa MGOMBEA WAO WA URAIS au CORD ambako aliondoka mapema baada ya kuhisi kuwa asingekuwa na nafasi ya kupata TIKETI ya kugombea URAISI.

Ila Afrika ina miujuza mingi you never know lolote laweza kutokea kwenye FIRST ROUND OF VOTING !

good analysis!
 
Wewe utakuwa rais wa kenya kwa kuwa utashinda umesharidhika. Tutabiri tumekuwa watu wa nyota au hali ya hewa kama unatuona watabiri wewe ndio tunaona utashinda
 
Wana Jamvi,

Nimewasili Nairobi Kenya leo asubuhi kama sehemu yawaangalizi wa kimataifa. Nimepata nafasi ya kutembelea kampeni za mwisho za wagombea urais kati ya Uhuru na Laila. Kusema ukweli sio rahisi kusema nani ataibuka mshindi ingawaje Uhuru Kenyatta alikuwa na watu wengi zaidi pale viwanja vya uhuru Park. Lakini ukizingatia kwamba Uhuru hapa Nairobi ndio kwao (anatoka Kiambu ambayo is just an outskirt of Nairobi), umati ule ulikuwa halali yake. Laila alikuwa pale Nyayo Stadium ambayo is like less 2 kilometers kutoka Uhuru ParK. Yeye kwao ni Kisumu lakini inaelekea ana support ya kutosha hapa Nairobi.

Nitajitahidi kuwaletea update kama nitakavyoweza lakini bila kuhadhiri utendaji wa aliyenituma. Tafadhali msinitake niwaletee picha kwani kwa nafasi yangu siruhusiwi kupiga picha.

N.B Sijatumwa na serikali ya Tanzania bali shirika binafsi. Kumbuka some 2 years back, niliwaletea update za uchaguzi kutoka Haiti.

Tiba
 
Kama unauchukia ukabila, bila shaka utaungana na mimi kuwa kila la heri raila amolo odinga, umedhulumika sana, mungu atakuwa nawe wakti huu
 
Wana Jamvi,

Nimewasili Nairobi Kenya leo asubuhi kama sehemu yawaangalizi wa kimataifa. Nimepata nafasi ya kutembelea kampeni za mwisho za wagombea urais kati ya Uhuru na Laila. Kusema ukweli sio rahisi kusema nani ataibuka mshindi ingawaje Uhuru Kenyatta alikuwa na watu wengi zaidi pale viwanja vya uhuru Park. Lakini ukizingatia kwamba Uhuru hapa Nairobi ndio kwao (anatoka Kiambu ambayo is just an outskirt of Nairobi), umati ule ulikuwa halali yake. Laila alikuwa pale Nyayo Stadium ambayo is like less 2 kilometers kutoka Uhuru ParK. Yeye kwao ni Kisumu lakini inaelekea ana support ya kutosha hapa Nairobi.

Nitajitahidi kuwaletea update kama nitakavyoweza lakini bila kuhadhiri utendaji wa aliyenituma. Tafadhali msinitake niwaletee picha kwani kwa nafasi yangu siruhusiwi kupiga picha.

N.B Sijatumwa na serikali ya Tanzania bali shirika binafsi. Kumbuka some 2 years back, niliwaletea update za uchaguzi kutoka Haiti.

Tiba

Mkuu Tiba tupatie updates
 
Ni kwamba mpaka sasa asubuhi hii, Uhuru anaongoza kwa tofauti ya karibu kura 400,000.

Update zaidi kwenye ile thread nyingine iliyonzishwa na mdau Kenyan.

Tiba
 
Back
Top Bottom